Madiwani CCM, Chadema nusura wazipige kikaoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madiwani CCM, Chadema nusura wazipige kikaoni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, May 2, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  May 2, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,644
  Likes Received: 82,373
  Trophy Points: 280
  Madiwani CCM, Chadema nusura wazipige kikaoni Sunday,

  01 May 2011 07:19
  Mwananchi

  Madiwani wa CCM na Chadema jana nusura wageuke wanamasubwi katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni,


  VURUGU kubwa ziliibuka katika kikao cha Baraza la Madiwani la Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam jana baada ya madiwani wa Chadema kuhoji matumizi ya Sh44 milioni zilizodaiwa kutengwa kwa ajili ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

  Vurugu hizo ziliibuka mwishoni mwa kikao baada ya madiwani wa Chadema kuhoji na kutaka kubadilishwa matumizi ya fedha katika Bajeti ya Halmashauri ya mwaka 2011/2012 walizodai kuwa zimepangwa kwa ajili ya kuandaa Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

  Kauli ya madiwani hao iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee na madiwani wa CCM wakiwa na jazba walikuja juu na kutaka mjadala huo ufungwe.

  Wakati kelele zikiwa zimetawala ukumbi huo wa Manispaa, Diwani wa Kata ya Kibamba, Issa Mtemi (CCM) alisema haiwezekani kikao hicho kuendelea kujadili bajeti ambayo imeshajadiliwa.

  "Mheshimiwa tumia kanuni kuruhusu kura zipigwe, anayepinga apinge na anayeunga mkono afanye hivyo, la sivyo hapa zitapigwa ngumi,"alisema Mtemi kwa jazba.

  Mara baada ya kauli hiyo madiwani wa Chadema waliinuka na kuhoji sababu za vitisho na kumlalamikia Meya kuwa kupitisha bajeti hiyo bila hoja zao kujibiwa.

  "Mheshimiwa Meya unakiuka kanuni za vikao, unapitishaje bajeti wakati hatujapata majibu ya maswali tuliyouliza? Na wewe unayesema unataka kupiga ngumi unamtisha nani? Njoo unipige," alisema Janeth Rithe, Diwani Kata ya Kunduchi (Chadema).

  Kauli hizo za madiwani wawili ziliwafanya madiwani wengine ukumbini kusimama kwa hasira huku wakitoa kauli za vitisho dhidi ya upande mwingine.
  Wakati hali ikiwa hivyo Diwani wa Kata ya Saranga kupitia Chadema alichana nakala ya bajeti na kuitupa.

  Katika hatua nyingine, Diwani mmoja wa CCM alisimama na kusema: "CCM oyeee!" na kuitikiwa, "Oyeeeee!"
  Diwani wa Chadema naye akasimama na kusema: " peoples! " na kuitikiwa, "power...!"

  Naibu Meya wa Manispaa hiyo, Songoro Mnyonge alilazimika kuondoka mezani kuelekea upande walikokuwa wameketi madiwani wa CCM na kuwatuliza madiwani.

  "Ninyi tulieni waacheni wao waendelee. Tulieni, kaeni chini," alisema Mnyonge huku wakiwagusa bega diwani mmoja baada ya mwingine.
  Wakati vurugu zikiendelea Mwenyekiti aliruhusu bajeti hiyo ipitishwe kwa kuuliza wanaounga mkono waunge. Hata hivyo, waliounga mkono walikuwa wengi hivyo bajeti ikapita.

  Bajeti hiyo imetenga jumla ya Sh89.4 bilioni kwa ajili ya shughuli za maendeleo, kati ya hizo Sh23 bilioni zitatokana na mapato ya ndani.
  Akizungumzia hilo baada ya vurugu hizo, Mbunge wa Jimbo la Kawe, Halima Mdee alisema bajeti iliyopitishwa katika kikao hicho ni nzuri na wala haina matatizo, lakini wao walitaka kujua sababu za fedha kutengwa kwa ajili ya CCM.

  "Katika bajeti nzuri, hii ni nzuri na hakuna hata diwani mmoja wa Chadema aliyekuwa na mpango wa kuikataa, lakini sisi tulitaka kujua kwa nini Sh44.3 milioni zilitengwa kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ifikapo Juni 2012," alisema Mdee.

  Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo, Yusuf Mwenda alisema hayo ni matokeo ya washiriki wa kikao hicho kutojua kanuni na kwamba wote waliohusika katika vurugu hizo watachukuliwa hatua.

  Kuhusu madai ya Sh44.3 milioni kutengwa kwa ajili ya kuandaa Mpango wa Ilani ya Uchaguzi wa CCM uliolalamikiwa, Meya alisema madiwani wa Chadema wamekosea kutaja kiasi hicho, bali zilizotengwa ni Sh10 milioni ambazo ni kwa ajili ya kuandika taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

  Katika hatua nyingine, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imetangaza bajeti yake ya mwaka 2011/2012 kuwa ni Sh91 bilioni .

  Akitangaza bajeti hiyo jana katika kikao cha Baraza la Madiwani Meya wa Manispaa hiyo, Jerry Silaa alisema bajeti hiyo ni ongezeko la asilimia 50 ya bajeti ya mwaka 2010/ 2011 ambayo ilikuwa Sh60.4 bilioni.
  Jerry alisema kati ya hizo Sh20.1 bilioni zitatokana na mapato ya ndani na Sh Sh69.8 bilioni ni ruzuku kutoka Serikali Kuu.

  Imeandikwa na Geofrey Nyang'oro, Haika Kimaro, Elizabeth Ernest na Minael Msuya
   
Loading...