Madiwani Arusha kuanza vikao kwa mvutano

Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,975
9,566
Na Omari Moyo, Arusha

KIKAO kwanza cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Arusha kinaanza tayari kuunda Kamati za kudumu za halmashauri, huku kambi ya
upinzani ikisema hawatakubali hadi nafasi ya naibu meya ijazwe.

Akizungumza mji hapa jana Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Bw. Estomih Chang’a amlisema kwamba tofauti kati ya madiwani wa CHADEMA na halmashauri zimemalizika kupitia semina elekezi iliyofanyika Februari 6 na 7, mwaka huu.

Alisema kuwa katika semina hiyo, yalizungumzwa mambo mengi muhimu kwa ajili ya maendeleo ya wananchi, na kukubaliana na mambo ya msingi na kwamba kikao cha madiwani cha leo ni cha kuunda kamati za kudumu za halmashauri.

Mkurugenzi Chang’a alisema kwamba, katika uundwaji wa kamati hizo utashirikisha madiwani wa pande zote, ili kamati hizo ziwe na nguvu na kuleta ufanisi wa kiutendaji kwa ajili ya maendeleo ya mji wa Arusha.

“Hiki ni kikao cha baraza la madiwani cha kuchagua kamati za kudumu za halmashauri..ambazo ni lazima ziteuliwe kabla ya kuanza kwa baraza la madiwani hivi karibuni,â€� alisema Chang’a.

Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Bw. Estomiah Mallah (CHADEMA) alisema kwamba watahudhuria kikao hicho bila na kusikiliza hoja zitakazotolewa ila hawatakubaliana na ajenda yeyote mpaka atakapochaguliwa naibu meya.

Bw. Mallah alisema kwamba haiwezekani kuteuliwa kwa kamati za kudumu za halmashauri wakati nafasi ya naibu meya ipo wazi, na kwamba ijazwe kwanza ndiyo shughuli hiyo iendelee.

“Hatuwezi kukubaliana na lolote kuhusiana na kuteuliwa kwa kamati hizo, mpaka nafasi ya unaibu itakapojazwa..na hilo ndilo jambo la msingi,â€� alisema Bw. Mallah.

Aliyekuwa Naibu Meya wa Jiji hilo, Bw. Michael Kivuyo alijiuzulu kutokana na mgogoro wa umeya unaondelea mjini hapa.

Source: majira
 
Back
Top Bottom