Madini ya Chuma ya Liganga na Mchuchuma mkoani Njombe kuibadili Tanzania kuwa kitovu cha bidhaa za chuma Duniani

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,775
Baada ya kusubiria Kwa miaka Mingi Hatimaye uchimbaji wa Madini ya chuma kuanza Rasmi Mkoani Njombe.

It is a game changer Kwa Tanznania.

=======

Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amesema Dunia imekuja na uhitaji mkubwa wa Madini ya Kimkakati kutokana na uhitaji wa mabadiliko ya teknolojia ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa betri za magari ya umeme, vifaa vya maabara, vifaa vya kutengezea simu, laptop na vifaa vya kutengenezea ndege.

Dkt. Kiruswa ameyasema hayo, leo Novemba 08, 2023 jijini Dodoma kwenye mahojiano maalumu katika kipindi cha Good Morning kinachorushwa na kituo cha Runinga cha Wasafi TV na Wasafi FM.

Aidha, Dkt. Kiruswa amesema mradi wa kuzalisha Madini ya Chuma wa Liganga na Mchuchuma utakapoanza Tanzania itabadilika kutokana na utajili wa madini hayo yaliyopo nchini humo.

Akijibu swali la mtangazaji, Dkt. Kiruswa amesema Utafiti wa Madini umeanza tangu mwaka 1925 ambapo ilikuwa kipindi cha wakoloni na mnyororo mzima wa thamani ya madini ni pana ambapo unaanzia kwenye hatua ya Utafiti, uchimbaji kisha uchenjuaji, uongezaji thamani madini na mwisho ni biashara ya Madini.

Kwa upande wake, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Madini Msafiri Mbibo, akijibu swali la Mtangazaji kuhusu maonesho ya Madini nchini Thailand amesema, ziara iliyofanywa na Wizara ya Madini pamoja na Wachimbaji wa Wadogo wa Madini Madini nchini Thailand ilikuwa ni kujifunza namna ya kuendesha minada ya Madini pamoja na mnyororo mzima wa madini ya Vito.

Aidha, Mbibo amesema kutokana na ziara hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya Bankoko ujumbe kutoka Tanzania ulifanikiwa uzoefu na kujifunza namna bora ya uongezaji thamani Madini ya vito pamoja na biashara ya Madini ya vito hususan bidhaa za usonara.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Dkt. Mussa Budeba, amesema taasisi hiyo ina miaka 98 tangu kuanzishwa kwake na inafanya kazi za kiutafiti ikiwemo kufanya tafiti za kijiolojia, wataalamu wanakwenda sehemu mbalimbali nchini Tanzania kufanya utambuzi wa miamba na mipasuko iliyopita sehemu mbalimbali, Aidha, ameongeza kuwa, Taasisi inafanya tafiti za kijiokemia kwa kuangalia hali ya tabaka la uso wa dunia kwa kuchukua sampuli ya Udongo na Maji.

Kitenge Updates
 
Back
Top Bottom