esther mashiker
JF-Expert Member
- May 29, 2018
- 616
- 555
MADINI ya vito yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 363 yamekamatwa katika mashine za kukagulia mizigo ya mpakani mwa Tanzania na Kenya, katika forodha ya Namanga kati ya Februari na Machi,
Madini hayo yalikuwa yanavushwa bila kufuata utaratibu wa usafirishaji nje ya nchi, yaligunduliwa katika Kituo cha Forodha cha Pamoja (OSBP), upande wa Tanzania. Ofisa Mfawidhi Idara ya Ukaguzi wa Madini, katika Forodha ya Namanga, Anold Francis, alisema, tukio la kwanza lilitokea Februari mwaka huu kwa madini yenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 329, kugundulika ndani ya mzigo wa mmoja ya wasafiri.
Alisema madini hayo yalikuwa ya aina tisa tofauti na mtuhumiwa alipaswa kulipia kodi ya asilimia saba ya thamani ya madini hayo. Francis alisema tukio la pili lilitokea mwanzoni mwa Machi mwaka huu, pakiti nne za madini aina ya Rhodolite yenye thamani ya Sh milioni 34 kukamatwa yakiwa ndani ya mzigo wa
msafiri aliyekuwa anaelekea nchini Kenya. Akifafanua kuhusu matukio hayo, Francis alisema kuwa kwa utaratibu wa usafirishaji wa madini kwenda nje ya nchi taratibu zinaelekeza kwamba eneo la forodha mpakani siyo sehemu ya kupatia vibali.
"Tunachofanya mpakani ni kuhakiki taratibu za kusafirisha madini kama zimefuatwa, ikiwamo ya vibali vinavyotakiwa pamoja na kodi inayopaswa kulipiwa na unapofika mpakani lazima uwasilishe nyaraka zote na siyo kupita kwa kificho," alifafanua.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ASP), Jonathan Shana, alithibitisha kutokea kwa matukio hayo yote mawili, alisema kuwa katika tukio la kwanza madini husika yamepelekwa ofisi za idara ya madini, ili kujua ni ya aina gani pamoja na uzito wake. Aidha, katika tukio la pili Kamanda Shana alimtaja mtuhumiwa wa tukio hilo kuwa ni Mathew Mrema (46), mfanyabiashara, mkazi wa Njiro, jijini Arusha.
Wakati huo huo, Ofisa Mwandamizi wa Uhamiaji katika forodha ya Namanga Emmanuel Kajura, alisema idadi ya wageni walioingia nchini kupitia mpaka huo, waliongezeka kutoka 118,041 huku waliotoka wakiwa 106,109 kwa mwaka 2017, wakati kwa mwaka jana 2018 walioingia walikuwa 119,180 na waliotoka 106,122.
Aidha, kwa upande wa Watanzania walioondoka kupitia mpakani hapo kwa mwaka 2017, walikuwa 96,521 na walioingia walikuwa 78,328 wakati mwaka jana wa 2018 walioondoka walikuwa 77,003 na walioingia walikuwa 63,487.
Kajura alisema baada ya kuanzishwa kwa kituo cha pamoja cha forodha OSBP hivi sasa mihuri ya kuingia na kutokea nchini inagongwa katika pasi za kusafiria, katika eneo moja na hivyo kupungua muda wa kuhudumia na kuwa kati ya dakika moja mpaka dakika tatu. Aidha, alisema hata mapato ya Visa yameongezeka kutoka dola za Marekani 836,840, kwa mwaka 2016/2017 hadi kufikia dola za Marekani 934,770, kwa mwaka wa fedha 2017/2018. Kajura alisema idadi ya wahamiaji haramu nayo imepungua kutoka 59 waliokamatwa mwaka 2017 huku 23 wakikamatwa mwaka