WAKUU,
NIMEKUMBUKA
Siku ya kuoa nyakati za mwisho kabisa kabla ya watu kusepa,
Mzee Baba alinipa madini yafuatayo;
"Mwanangu chukua notibuku yako,
Kuna vitu vichache muhimu naomba uviandike.
Nasisitiza,
NI VITU MUHIMU.
1. Mwanangu usibadilike kiasi cha kusahau wengine waliokusaidia au kushirikiana nawe kwenye mambo mema kisa ndoa.
2. Heshimu mkeo,
Ila usizubae ukapelekwa hovyo kama zoba.
3. Mke usimhusudu kiasi cha kumwona yupo sahihi hata akafikia hatua ya kudharau wazazi wako.
4. Mke ana haki ya kukushauri ila asikupangie na kukuamrisha.
5. Mke usimpe nafasi ya kubishana na wewe hata kidogo,
Nasisitiza "HATA KIDOGO".
6. Mke ana mapungufu yake kama ulivyokuwa nayo wewe mwanangu- hivyo akikosea ni vema msuluhishe kwa mazungumzo.
7. Mkeo ni lazima atii maagizo yako, hasa yale yaliyo mema.
Akiwa anapingana na wewe-
Maisha yenu yatayumba sana na utakwama sehemu nyingi.
8. Msamehe makosa mengine, ila kosa la kukusaliti usijliadili hata kidogo-
Ikiwa tu umethibitisha na kuhakikisha,
Mwache,
kwani hatokuja kukuheshimu tena na hatokoma kukusaliti.
Narudia,
MKEO AKIKUSALITI MPE TALAKA KABISA!!!
9. Usigombane na ndugu zako bila sababu za msingi kisa hamasa ya mkeo,
Ndoa ni undugu wa application ambao unaweza kwisha,
Ila
undugu wa damu na ndugu zako hauwezi kwisha.
Zingatia hayo,
Mengine tutazungumza siku zijazo utapokuja Mtwara kutusabahi.
KILA LA KHERI MWANANGU MPENDWA #SENETA_WA_MTWIZ."
FADHA AKANIPA MKONO WA KHERI AKASEPA.