Madikteta wa Afrika wataunga foleni kwenda kumpongeza Yoweri Museven!

G Sam

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
11,593
36,012
Kwanza kabisa naungana na Trump kuhusu kuishambulia Uganda! Ningekuwa nina uwezo ningemtokomezea mbali dikteta Yoweri Museven! Nisingeishia hapo, pia Nkuruzinza ningemuondosha!

Pili naunga mkono kauli ya Trump kuwa Afrika bado haijaweza kujitawala! Inahitaji kutawaliwa tena!

Inasikitisha kuona watala au vyama vinavyotawala Afrika kufanya mambo ya kihuni na ajabu! Vinasimama kwenye ulaghai na uhujumu wa hali ya juu! Afrika bado inaonekana changa sana na au bado haiwezi kabisa demokrasia!

Yoweri Museven siku atakapoapishwa tutashuhudia madikteta wa Afrika wakiunga foleni kwenda kula na kunywa huku wakitoa pongezi na hotuba za wizi na ulaghai eti wakimpongeza kwa kushinda! Viongozi wa Afrika wamekuwa wakilindana na kuteteana kwa maovu na uhujumu wa demokrasia! Kwa hakika Afrika inahitaji kutawaliwa tena kwani bado kabisa haijajitambua!
 
..Trumph kwa upande mwingine alikuwa sahihi..Africa inatia aibu..inchi nyingi za kiafrica ni ubabe..wafanye basi kiini macho kama Tz ya CCM..tunaona marais wanabadilishana lakini kwa style yao wenyewe waccm.
 
..ngoja niangalie kwa makini kama JPM atahudhuria shamrashamra za kuapishwa kwa huyu dictator..
 
Wapongezane tu kwa wanayo yafanya ,lakini wakumbuke raia nao sio ng'ombe..Watafikiri namna ya kukabiliana na viongozi madikteta hasa njia wanazo zitumia madikteta hao kuendelea kusalia madarakani.
 
Mugabe na museveni ndio watakuwa wakongwe kwenye hiyo shuguli kuwa marais waliokalia kiti cha urais kwa miaka mingi uku kagame na mkurunzinza wakiwa wanatamani kuwa kama hawo huku chama cha fisiem kikishika nafasi ya kuwa kikongwe
 
Kwanza kabisa naungana na Trump kuhusu kuishambulia Uganda! Ningekuwa nina uwezo ningemtokomezea mbali dikteta Yoweri Museven! Nisingeishia hapo, pia Nkuruzinza ningemuondosha!

Pili naunga mkono kauli ya Trump kuwa Afrika bado haijaweza kujitawala! Inahitaji kutawaliwa tena!

Inasikitisha kuona watala au vyama vinavyotawala Afrika kufanya mambo ya kihuni na ajabu! Vinasimama kwenye ulaghai na uhujumu wa hali ya juu! Afrika bado inaonekana changa sana na au bado haiwezi kabisa demokrasia!

Yoweri Museven siku atakapoapishwa tutashuhudia madikteta wa Afrika wakiunga foleni kwenda kula na kunywa huku wakitoa pongezi na hotuba za wizi na ulaghai eti wakimpongeza kwa kushinda! Viongozi wa Afrika wamekuwa wakilindana na kuteteana kwa maovu na uhujumu wa demokrasia! Kwa hakika Afrika inahitaji kutawaliwa tena kwani bado kabisa haijajitambua!
halafu wanapendana kinoma,nadhan mugabe hatakosA HUKO>halfu ndo walimpa museveni kazi ya usuluhisha mgogoro wa burundi..yaan kesi ya nyani hakimu ngedere
 
Back
Top Bottom