Madhara ya Television na ulimwengu wa digital

Madhara ya Television na ulimwengu wa digital

Alex jairo

Member
Joined
Jun 13, 2013
Posts
17
Reaction score
3
Leo Ninawaletea Mada nzuri sana kwa wale wenye familia na hata wasio na familia ili tujifunze jinsi mataifa yenye nguvu yanavyofanikiwa kutuaribia mila na desturi ya mwafrika kupitia kifaa kinaitwa TELEVISHENI..

Televisheni ni adui wa Jamii, na pia itakupa faida kama itatumika ipasavyo... Serekali yetu ilitenga mabilioni ya mapesa eti kwenda kwenye digitale na ukitazama hali ya miundombinu mashuleni inasikitisha. Hakuna madawati wala Maabala na sijui hili ni shinikizo kutoka mataifa makubwa na lengo lao nalijua ni kumwalibu mwafrika katika kila nyanja kuanzia tamaduni, Elimu na Imani.

Ngoja nikupe siri ya Television(TV). Hii ni mind control Device, Kama ulikua hujui hili basi tambua na Amini ninayokwambia na fanyia kazi.

TV inahalibu vipi Jamii?

Nilitoka mkoani mwangu Msoma mjini nikiwa na miaka 12- kule mwanamke kuvaa suruali sikuona..mwanaume kutoboa masikio sikuona... Mwanaume kusuka nywele sikuona.. Kunyoa viduku sikuona.. Ushoga sikuona!!! Lakini miaka ya sasa kila kitu kimearibika sababu ya TELEVISION... Tunaiga vitu vinavyofanywa kwenye TV.

Television inaongoza jamii baada ya jamii kuongoza Television. Nahisi Mataifa makubwa yanahonga Viongozi wetu ili tu kutimiza malengo yao ya kuiharibu Afrika na tuwe mazezeta. Unatazama show na mwanao sebuleni then msanii wa kiume anajitangaza kua yeye ni shoga au katoto kadogo kanaangalia video music watu wamevaa mavazi ya ajabu(nusu uchi). Siku hizi kasichana kadogo kanajua mapenzi sababu ya DVD chafu na Tamthilia za mapenzi, imefikia wakati ukioa binti mwenye bikira unabahati!!!

kweli Wazungu wamefanikiwa kuvuruga kichwa cha Mwafrika. Ushauri wangu kwako kwa wewe mzazi wa baadae - Sebuleni kwako weka au mtengenezee Library mwanao na sio Luninga
 
Ni kweli kabisa mkuu yan miaka 10 ijayo sijui utakuwaje savabu sio watoto; vijana au wazazi wote wameshavurugwa na tv na utandawazi wa ngozi nyeupe.....
 
Back
Top Bottom