Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
UTEUZI WA WAKURUGENZI WA HALMASHAURI ZA WILAYA, MIJI, MANISPAA NA MAJIJI.
Katika ngazi ya wilaya tulizoea kuona Raisi akiteua DC pekee huku nafasi zingine za makatibu tawala na wakurugenzi wakichaguliwa na watu wengine.
Nafasi ya Mkurugenzi ni nafasi muhimu sana na inatakiwa kupewa kwa njia ya “promotion” kwa watumishi wa umma wenye uzoefu na kazi za utumishi wa umma kwa muda mrefu. Watumishi wengi wa umma kwenye ngazi za wilaya walikuwa wakifanya kazi kwa weledi na uadilifu mkubwa ili waje kuwa wakurugenzi. Kiu hii ya wafanyakazi wengi wa umma imeanza kuvurugwa kwa kuanza kuajiri makada kwenye hizi nafasi.
MADHARA YA KUTEUA MAKADA KWENYE NAFASI ZA UKURUGENZI WA HALMASHAURI.
i) Madhara ya muda mfupi
Badala ya kupiga kazi ili halmashauri zilete maendeleo kwa wananchi makada hawa watajikita kujenga chama.
Watumishi wengi wa umma wataanza kujiunga na siasi ili waje kuchaguliwa kuwa wakurugenzi kwani kwa hali ilivyo sasa uwezekano wa kuwa mkurugenzi kwa njia ya kawaida haupo.
Madiwani wa vyama vya upinzani watapata wakati mgumu sana kudeal na hawa makada.
Watumishi wengi wa umma wamekuwa “discouraged sana” wamevunjwa moyo sana utendaji wao wa kazi utateteleka hasa Halmashauri ambazo wakurugenzi walioletwa ni makada.
Nchi iingie gharama kubwa ya kuwafanyia “orientation” hawa viongozi gharama ambazo zingepelekwa kwenye maendeleo
Issue ya kubana matumizi ya serikali haipo kwani asilimia chache sana ya wakurugenzi wamestaafu wengine wameachishwa ukurugenzi ili makada wajazwe tunaingia gharama zingine za kulipa mishahara makada.
ii) Madhara ya muda mrefu:
1) Kwa kuwa wasimazi wa uchaguzi wa diwani, mbunge na raisi ni hawa wakurugenzi naona kurudishwa nyuma kwa demokrasia hapa nchini hasa kwenye uchaguzi wa mwaka 2020.
2) Kwa kuwa wakurugenzi wengi waligombea ubunge 2015 wakakosa ndani au nje ya CCM; tusitegemee mapya kwenye halmashauri zetu kutoka kwa hawa wakurugenzi ambao watajikita kujiimarisha kwenye mawindo yao ya ubunge 2020
Unaweza kuendeleza na ww juu ya madhara haya...
MAGANGA SAMBO
diwani wa Kata ya Mlabani