Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,118
- 1,565
Eze 7:26 SUV
[26] Madhara yatakuja juu ya madhara, na habari ya shari juu ya habari ya shari; nao watakwenda kwa nabii kutaka maono; lakini hiyo sheria itampotea kuhani, na mashauri yatawapotea wazee.
Dhambi ya uasi kwa Mungu ilisababisha hukumu ya Mungu juu ya taifa la Israeli, ikatangazwa yale yanayokuja juu yao.
Imewekwa wazi vile madhara juu ya madhara yatakavyowapata watu hawa, wakajulishwa kuhusu manabii, makuhani, na wazee, watawatafuta sana lakini hawatawapata.
Ukosefu wa mwongozo wa kiroho ulisabisha madhara, mojawapo ulileta hukumu ya Mungu, jambo ambalo lilisababishwa na manabii kukosa maono, makuhani kukosa neno, na wazee kukosa hekima.
Leo nabii wetu mkuu ni Yesu Kristo, Yeye hutoa maono ya kweli kuhusu maisha yetu, anasema nasi kupitia neno lake, Roho Mtakatifu, na mwenye neno anajua sauti yake.
Mdo 3:22-23 SUV
[22] Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi. [23] Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.
Sivyo hivyo tu, kuhani wetu mkuu ni Yesu Kristo, Yeye ni wa milele, sheria na neema hupatikana kwake, hakuna anayeweza kupotea akiwa kwake.
Ebr 4:14-16 SUV
[14] Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu. [15] Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi. [16] Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.
Na Kristo ndiye hekima ya Mungu, tuliona wazee wa Israeli walipoteza mashauri mema, ila kwa Kristo tunapata hekima ya milele.
1 Kor 1:24, 30 SUV
[24] bali kwao waitwao, Wayahudi kwa Wayunani, ni Kristo, nguvu ya Mungu, na hekima ya Mungu.
[30] Bali kwa yeye ninyi mmepata kuwa katika Kristo Yesu, aliyefanywa kwetu hekima itokayo kwa Mungu, na haki, na utakatifu, na ukombozi;
Ule ukosefu wa mwongozo wa kiroho tuliuona katika agano la kale, katika agano jipya unakamilishwa na uwepo wa Kristo na Roho Mtakatifu.
Roho Mtakatifu ndiye anayetoa maono na mashauri mbalimbali kwa kanisa, tofauti na hukumu ya Ezekieli, kanisa la leo la Kristo halina upungufu wa mwongozo wa kiroho.
Napenda uelewa kwamba, kanisa likiishi maisha ya dhambi na uasi, litapoteza mambo mengi sana kwa Mungu mojawapo ni kukosa sauti ya Mungu kama tulivyoona kwa Israeli.
Kanisa linapaswa kutembea katika njia ya kumtegemea Roho Mtakatifu, si viongozi wao tu, wanapaswa kufuata iliyo kweli bila kujalisha viongozi wao wanapindisha.
Epuka maisha ya dhambi, maana huondoa mwongozo wa kiroho kwa mwamini, utaacha kusikia sauti ya MUNGU, na maisha yako yatakuwa magumu sana.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia na kutafakari
Mungu akubariki sana