Madereva Watanzania 51 wakutwa na maambukizi mpakani mwa Kenya na Tanzania. Visa vya Coronavirus Kenya vyafikia 912

If we keep acting normally
This disease will act Abnormally

Kama unashindwa kuzuia waliopata ugonjwa wasisambae Tanzania unatagemea nini kifuatacho?
Hiyo ni sample ya Truck drivers tu
Think BIG
 
Wananchi wa Kenya wanamlaani sana Rais wao wanaomba hata tubadilishane na viongozi wao wa juu wote tuwape Magufuli wetu!! Chuki zao hazisaidii wao wanawaza kupiga hela za IMF na Mikopo ya Corona ya World Bank ambayo haimfikii mwananchi wa chini zaidi ya kumpima tu na kumfungia ndani na kutuma idadi kwa mabwana wakubwa wao wawape hela zingine huku walala hoi wakifa kwa njaa!! Mungu anawaona kwa kweli
Lol dude. Uache kupiga propaganda hapa. Hakuna mahali wanamlaumi rais wao. They know kwamba wkt huu lazima wafunge mkanda.
Unlike us.. wao malalamiko huyasikii kabisa.

Halaf hayo masuala sijui ya mkopo.. propaganda za kijinga. Mbona hata sisi tuna deni la IMF tena kubwa tu..
Hilo hulioni?

Uwe unahusisha logic kwenye mada zako. Kupimwa kusiwe ni uadui.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Safi sana, pima wote wanaong'ang'ania kuingia Kenya, ingekua hawa Watanzania ndio wanapima Wakenya na kugundua wengi kiasi hiki sasa hivi wangekua wanalialia eti Kenya ina ajenda ya kuwaambukiza, yaani juzi waligunduliwa 78 wote kwa siku moja, leo 51 yaani wanataka kuja mamia yao wakiwa na kirusi, kama vipi maafisa waongezwe kwenye huo mpaka, hawa watatumaliza.

Niliskliza hotuba ya mkulu wao nikachoka, eti anadai dereva hana haja ya kupimwa kisa kaendesha lori mwenyewe kilomita zaidi ya 1,000. Ukweli rais Magufuli kuna mambo anafanya mazuri ila kuna maneno humtoka mpaka unasshindwa kweli kama alihudhuria darasa hata moja la sayansi, au labda ana washauri wabovu sana kuwahi kutokea.

Wataalam wameeleza jinsi hiki kirusi kinaambukiza na kusambaa, uwezekano upo mkubwa kwa dereva kuendesha lori kilomita zote hizo bila kugundua, maana kawaida wengi husafiri kama siku nne au tano, ila kirusi hadi kijitokeze vizuri kinahitaji siku kama kumi hivi, sasa mheshimiwa rais anataka mamia ya madereva wake walioathirika waachiwe waingie kwenye mataifa majirani kisa wamejiendeshea malori wenyewe.

Hotuba zake zimejaa kejeli dhidi ya mataifa ambayo yamechukua hatua za tahadhari, halafu watu wanahoji kwanini Tanzania inatengwa na SADC na EAC, maana hivi kwa kweli wakikutana marais wote wanajadili mikakati halaafu mmoja wao hana mikakati zaidi ya kukejeli wenzake, ni dhahiri hawataendana, hapa inabidi Watanzania wafungiwe wabaki huk huko kwao watajuana wenyewe, wakujifia atajifia na wa kupona atapona. Yeyote kati yao anayetaka kuvuka mpaka apimwe tena sana na kuhakikisha yuko salama, au raia yeyote anayetokea Tanzania hata iwe mtalii, mzungu, Mchina wote wapimwe mara mbili mbili na hata ikitokea hawana, zchukuliwe namba zao za simu na wenyeji wao, na wapi wanakwenda, wafuatiliwe huko hadi ziishe siku 14.
 
Hizo mashine zao ziko na faults.
Itabidi kupeleka mabeberu na yale mapapai yetu ili tuthibitishe hilo.

#DeadMenWalk
 
Tunachojua ni kwamba hao madereva hawan Corona kama Kenya inavyotaka kuiaminisha dunia,nyinyi endeleeni,sisi hatuna haraka,just inferiority complex ina wasumbua!
 
Hii hali mbona inatusha, hii ni segment ndogo tu yenye kuwahusu madereva wa malori peke yake. Je! Ndiyo tuseme jirani zetu wanatusingizia ama COVID-19 ilikuwepo nchini tokea kipindi kile cha mwaka jana wakati wa yale tuliofikiria kuwa ni mafua makali na serikali kuyatolea tamko?

Ama pia ndiyo kusema tumeamua tuingie kimya kimya katika "herd immunity" pasipo tamko lolote kutoka serikalini?

Ee Mola wetu tukuangamia na kutubu dhambi zetu kama taifa, tunajuta kutokana na uovu wetu mbele ya macho yako, tunakiri kuwa tumekukukosea wewe Muumba wetu, kwa mawazo, kwa maneno, kwa vitendo na kwa kutokutimiza wajibu wetu. Tunakuomba utunusuru na gonjwa hili, ambao si cho chote kile mbele ya uweza wako ulio mkuu sana. Ameni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Madereva wa malori ni wahanga wa magonjwa ya mlipuko
Wamesambaza sana ukimwi njia ya Dar - Mbeya
 
Kumbe bado wanang'ang'ania kuingia nchini Kenya? Tena kabla ya kukubaliwa kuingia lazima wapanue midomo yao hadi jino la mwisho lionekane ili wahudumu wa afya waweze kuokota sampuli. Kuna uzi humu ambao unadai kwamba wana mpango wa kusitisha usafirishaji wa bidhaa kuingia nchini Kenya. Vipi joto la jiwe, DC wa Longido amelegeza kamba au ni wenye bidhaa ndio wanataka hela liwe liwalo?
 
KANYAGIA HAPO HAPO KENYATA..MPAKA NYOKA ATOKE MAPANGONI HUKO CHATO KUOMBA POO!

WAKENYA SIO WATANZANIA WANAODANGANYWA KAMA WATOTO WA CHEKECHEA...ETI CORONA IMEISHA.
tapatalk_1589575901484.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wawe na corona halafu wameendesha safari nzima hadi mpakani hawajaanguka? WaKeii acheni hizo mambo 😂😂😂
 
Back
Top Bottom