Rlechas_3a60
Member
- Oct 4, 2018
- 12
- 27
Madereva wa gari dogo la abiria wanaofanya safari zao kuanzia Mbezi hadi mkoani Morogoro wameiomba serikali kuangalia upya tozo za kuingia na kutoka kwenye vituo vya Kibaha, Mlandizi na Chalinze.
Kauli hiyo ilitolewa na Mratibu wa Umoja Madereva hao, Peter Mbedule, wakati akisoma risala mbele ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Bashir Ally wakati akizindua tawi la madereva hao na wajasiriamali wa Kata ya Msigani.
Mbedule alisema kumekuwa na utaratibu wa tozo tofauti kati ya vituo hivyo ambapo Kibaha, Mlandizi na Chalinzewamekuwa wakitozwa Sh. 500 kila wanapoingia na kutoka katika vituo hivyo.
Mbedule alisema kuwa, kituo cha Mbezi cha jijini Dar es Salaam wanatozwa Sh 1,000 kwa siku nzima huku vituo vya Kibaha, Mlandizi na Chalinze hutozwa Sh. 500.Alisema kuwa, hali hiyo inasababisha kutumia Sh 3,000 hadi 5,000 kwa siku jambo ambalo linasababisha ugumu wa maisha katika maeneo hayo.“Kila tunapoingia au kutoka Mbezi kwenda Morogoro ukiingia unatozwa Sh 500 na ukirudi unatoa hivyo hivyo kwa siku gari moja linaweza kuingia hata zaidi ya mara nane,” alisema.
Mbali na tozo hizo alisema kuwa kutokana na ongezeko la magari hayo yanayoenda mikoa ya jirani wamekuwa na eneo dogo la maegesho jambo linalosababisha kutozwa faini pindi wanapoegesha eneo lisilo rasmi.
Akifungua tawi hilo Dk. Bashiru aliwataka viongozi wa serikali kuwaheshimu na kuwathamini wajumbe wa nyumba kumi kutokana na kazi kubwa wanayoifanya.
“Wakuu wa mikoa na wilaya mnapopigiwa simu na wajumbe wa nyumba kumi pokeeni msiache kupokea na atakayeacha kupokea atawajibishwa hawa ni watu muhimu kwani wanawatambua vizuri wafanyabiashara, wajasiriamali wanaolipa kodi,” alisema.