Madereva wa Magari ya kusafirisha Magazeti wana roho ya Binadamu kweli?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
59,949
119,212
Kama kuna wenzangu ambao tulishawahi kuyapanda haya magari na mpaka tupo hai kabisa basi nadhani ni jambo la kumshukuru sana Mwenyezi Mungu na kufanya hata ibada.

Kwa nilichokiona Jumamosi kwa haya Magari ya Vyombo vya Habari yanayosafirisha Magazeti usiku ni bora tu hata kama nina shida au haraka ya kusafiri kwenda Mikoani basi nisafiri na Mabasi ya kawaida nifike huku roho yangu ikiwa na amani.

Nimepatwa mno na wasiwasi kama kweli hawa Madereva wa haya Magari ni Wanadamu wa kawaida na kama basi kuna kilevi wanakitumia sidhani kama ni Bange ( Pombe ya Makaratasi ) au Shisha au Gongo na labda tu ni aina mpya ya ulaibu ( kilevi ) ambacho naamini hata Serikali bado haijakitambua.

Juzi Jumamosi nilikuwa na appointment na Mtu Mkoani Arusha muda wa Saa 3 asubuhi na bahati mbaya kulikuwa na jambo la msingi sana na alinitaarifu wakati muda umeshaenda kama Saa 11 za jioni siku ya Ijumaa.

Nilipopata tu huo mwito nikawa sasa nahaha jinsi ya kupata usafiri ili hiyo Jumamosi asubuhi inikutie Mkoani Arusha hivyo basi Watu kadhaa wananishauri kuwa niyavizie yale Malori ya Mizigo na Mafuta yaendayo Kilimanjaro na Arusha yanayopita Ubungo mida ya Saa 2 au 3 Usiku lakini hapo hapo tena nikapata wazo nadhani huyu aliyenipa hili wazo ni mzoefu ambapo akaniambia kuwa niende pale Mwenge Kituo cha Daladala niyavizie Magari ya Magazeti ya NIPASHE au yale ya MWANANCHI na MAJIRA kwani nitawahi.


Kweli kwakuwa nilikuwa na haraka halafu muda nao ulikuwa una taradadi ilipofika tu Saa 5 usiku nikasogea pale Mwenge na ukweli nililikuta gari la Kampuni ya Magazeti ( kwa usalama wa Ajira ya dereve sitotaja ni Kampuni gani hasa ) ambapo aliniambia kuwa alibaki tu abiria mmoja kisha aanze safari.

Ndipo kidume nikajitosa na kupanda. Nilipopanda tu mule ndani na kukuta wale abiria wenzangu walivyopangwa utadhani Magunia ya Viazi vya Mbeya au Mananasi ya Kiwangwa nikajua tu kuwa leo shughuli ipo. Wakati safari hata bado haijaanza nikamuuliza yule Dereva kuwa kama muda ule ulikuwa ni Saa 5 inaenda Saa 6 usiku je anadhani Arusha tutafika Saa ngapi? Nae bila hiyana akanijibu kistaarabu tu kama siyo kiungwana kuwa Saa 10 au tukichelewa sana basi Saa 11 alfajiri tutakuwa Arusha kwani yeye mwenyewe anatakiwa kuwa Dar Saa 5 ( yaani asubuhi yake ) ili gari likafanyiwe service.


Kiukweli pale pale nilianza kujihoji je naongea na JINI au kitu gani? Wakati Mimi nikijiuliza juu ya aina ya mwendo atakaoutumia huyo Dereva abiria wenzangu walikuwa wala hawana wasiwasi tena wengine kwa kunionyesha kuwa wao wameshazoea niliwasikia wakiwaambia wenza wao kuwa nanukuu " Jamani Mke wangu hakikisha unaandaa Daku mapema kwani Saa 9 au Saa 10 nitakuwa hapo Moshi ", mwingine nilimsikia akisema namnukuu " Wewe Mwanamke karibia nafika hapo Majengo sasa ole wako nimkute Mwanaume humo ndani " na wa mwisho nikamsikia akisema namnukuu " Oya anza kabisa kuchemsha maji ya moto kwani nakuja na bonge la Kuku nataka umtengeneze haraka na ninywe supu yake pia nafika muda si Punde ".

Niliogopa lakini nikajikaza tu kisabuni na hata nilipompigia yule Kaka aliyenielekeza pale na kumwambia hofu yangu juu ya muda ambao dereva aliniambia tutakuwa tumefika Arusha na yeye akaniambia kuwa kwa huo muda ambao Dereva ameniambia yeye anaona kama vile Dereva amechelewa kwani alisema kuwa Yeye siku tatu tu zilizopita alisafiri nae na kutoka Dar Saa 5 usiku na walifika Arusha Saa 8 na nusu.

Jamani tulianza safari yetu pale Mwenge Saa 5 na nusu na kwa aina ile ya Spidi na Mimi nilivyo mwoga wa mwendokasi ilinibidi tu niutafute usingizi kwa lazima ili tu nisione Gari yetu ile ilivyokuwa ikikimbia. Hivyo basi nakumbuka tulipofika tu maeneo ya Msata kwani tulipitia hii njia ya Bagamoyo nikaupata usingizi na nakumbuka wakati Mimi nautafuta usingizi wangu nilioupata Bagamoyo wale abiria wenzangu wao usingizi wao walikuwa wameshaupata tayari Makonde, wengine Tegeta kwa Ndevu na wengi wao wakaupata maeneo ya Boko Basihaya.


Nisiseme uwongo ilipofika tu Saa 10 yule Dereva alituamsha wote na Binafsi niliposhtuka tu nikajikuta nipo maeneo ya Mianzini pale Arusha kitendo ambacho kilinitisha mno na siyo SIRI ilibidi tu nimtafute Dereva Teksi pale anipeleke Hospitali ya karibu kucheki " Presha " kwani nilishikwa mno na butwaa!

Na hatimaye nikawahi appointment yangu na yule jamaa na Saa 5 nikawa nimeshamalizana nae nikaanza kutembea pande za A town pale mjini kimtindo na jioni nikaenda zangu kukata tiketi yangu ya Basi na hatimaye jana Jumapili jioni hivi nikawa nimefika " Changanyikeni Brains City " Dar es Salaam.


Mwisho naomba tu kuuliza je Wahusika akina SUMATRA, TANROADS na TRAFFIC POLICE hii " kitu " wanaijua? Na kwa habari za " chini chini " ambazo nimezipata zinasema kuwa kila Mwezi au hata Wiki hawa Madereva wanapinduka huku njiani ila TAARIFA zao za AJALI huwa zinafichwa na kuna Mtu mmoja alinidokeza kuwa wao wakipokea tu Simu kuwa kuna Gari ya Kusafirisha Magazeti imepata AJALI huwa hawaulizi imekuwaje na badala yake huuliza tu ni Maiti ngapi zimepatikana au zimeharibikaje ili wakazifuate kwani anasema kwa aina ya mwendo ambao Madereva wa hizi Gari huwa nao wakipata AJALI uwezekano wa kumkuta Mtu akiwa hai ni ( - 0 ).

Ni hayo tu Wanajamvi ila ningependa tu kufahamu kuwa hawa Madereva wa hizi Gari za kusafirisha Magazeti ya Mikoani ni Wanadamu kweli na je wana roho kama hizi tulizonazo sisi wengine?

Wahusika chukueni hatua za kuwaokoa wengine kwani ni HATARI na INATISHA mno na Namshukuru Mwenyezi Mungu alinilinda ila cha moto Mwanamume nilikiona.
 
"we mwanamke karibia nafika hapo majengo sasa ole wako nimkute mwanaume hapo ndani"

Nimeipenda hii jamaa anaonekana anampenda sana mke wako hata akimfumania anaonekana hawezi kumuacha ndio maana anatoa taarifa mapema.

Kuna msemo unasema " usimuwekee mitego mingi ya kumfumania kama huna uwezo wa kumuacha" ndio maana wazee wa zamani wilikuwa wanapiga mrusi au kuimba imba akiwa anakaribia maeneo ya nyumbani ili kama mgoni akimbie.
 
Hayo maandishi yako mara herufi kubwa..mara marangirangi yananikera sana utakuwa unavuta bange ww sio mzima ni mwehu

Hujakosea Mkuu na naivuta kweli. Nyingine Chalii wa Arusha walinipa juzi nilipokuwa huko na ni kitu cha Longido. Ninachofurahi ni kwamba nikivuta hiyo Bange ndiyo nakuwa na AKILI na UWEZO MKUBWA sana wa KUFIKIRI sijui kwanini? Vipi nikuletee kidogo " jani " na Wewe ushtue Mkuu kwani stock ipo ya kutosha.
 
Back
Top Bottom