tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Hii hali imekuwa ikijitokeza mara kadhaa, kuanzia dereva hadi kondakta wamekua na utamaduni mbovu sana kwa kuonyesha namna walivyokosa maadili kwa kutumia lugha za matusi na maneno makali kwenye vyombo vyao vya usafiri bila kujali watu walio wapakia na wanajua fika kuwa watu wanaowapakia ni mchanganyiko, kuna watoto kabisa vijana hadi wazee.
Soma pia: Sumatra: Makondakta na Madereva daladala Mbeya wanatoa lugha mbaya kwa abiria
Mathalani kwa siku ya Jana usiku nilipokuwa kwenye usafiri wa umma (daladala) yenye taarifa zilizopo kwenye picha ambatanishwa, dereva na kondakta wake walikuwa wakitumia lugha za matusi wakiwa wanadai nauli na baadaye wakati anapishana na madereva wenzake.
Jambo hilo la matusi lilipelekea daladala hiyo kwa kugongana na daladala nyingine zikiwa zimetokea uelekeo mmoja kutoka Kawe kwenda segerea, hii ni kutokana na kukosa maelewano baina yao.
Tukio hilo la ajali lilipelekea kuleta msongamano na hivyo kutupotezea muda abiria Tukajikuta tunafika kwenye makazi yetu kwa kuchelewa sana. Sehemu ya kutumia nusu saa tumejikuta tumetumia zaidi ya masaa mawaili kisa madereva kukosa ustaarabu.
Swali la kujiuliza katika kuchelewa huko ndani na kwenye Gari kulikuwa na watoto hadi wazee.. Je, wale wanafunzi wameenda kueleza nini kwa wazazi wao kwa kuchelewa kurudi nyumbani? Je, wazazi hao wamewaelewa watoto wao, vipi wake za watu wameeleza nini kwa waume zao kwa kuchelewa kufika nyumbani? Je wake hao wameeleweza na waume zao?
Tunaomba sana mamlaka simamizi za usafiri wa ardhi, litazameni hili, tunahitaji pawe na maadili pamoja na ustaarabu kwa daradara.