Madereva kukimbia baada ya Ajali

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,562
21,570
Wadau wana Jamiiforums;

Kuna hili swala la madereva wengi kukimbia baada ya ajali, labda inaeleweka kidogo kwa wale wanaokimbia hasira za wananchi japo tujiulize kidogo, kwanini wananchi wanamshambulia dereva au gari lake kwa kuchukua sheria mkononi badala ya kumfikisha kwenye vyombo husika?

Lakini pia kuna wale wanaokimbia mazima hasa kama gari sio lake 'mali ya tajiri'. Hapa chini ni ajali imetokea Kigoma Kasulu ambapo gari iligongana na pikipiki, dereva wa pikipiki alivunjika mguu na dereva wa gari aliamua kukimbia na kuacha gari.

Si ajabu dereva wa gari angebaki na kuamua kutafuta suluhisho la kumuwahisha mwenzake hospitali haraka lakini najiuliza hili zimwi la madereva kukimbia, tatizo ni 'wananchi wenye hasira kali' au madereva kuogopa kuyakabili matatizo ya ajali hasa wenye mabosi.
fp-eIw7dfHd8OsULrGYpXp06oGZEGRsTpRoF2Tjsr7wJiF9KDbIjjZr0-vgC2tnkq8CQ3Dun8ZjXEHkVGpLzhqOBPgLb2u-52ouj0f2Vgv0p-Wm9mzWN1U7S2Z8asc-hyEgkyCk4MxWpvSZS-c8S5rc8GX8BNrn99_eqga3kFdOl9UnA1Qhq6vP8FIBflnzJ=s0-d-e1-ft

BKcwakUWJc145ITg0HkQZChS8wJxu1lTeZQnhTTp36xUIkXYvpBTtmva7s5Q55EQuNeUBfdC4NiASpxKdWINvunmNa_ojLaVMeZU98m5tw_-WRrS-EaH33BoaUnvVpsQT8UTc9uV22rUyzWjgY6fO-tQsFpYRBvNvgOk8OLuqLqJNyPLcw7gtwWxRVXv8GLe=s0-d-e1-ft

Ukibaki wananchi wanaweza kukuchoma moto kama huna cha moto kuwatawanyisha. Wengi wao huwa si waelewa, tena fanya ufanyalo usigonge hao waendesha pikipiki
 
Wadau wana Jamiiforums;

Kuna hili swala la madereva wengi kukimbia baada ya ajali, labda inaeleweka kidogo kwa wale wanaokimbia hasira za wananchi japo tujiulize kidogo, kwanini wananchi wanamshambulia dereva au gari lake kwa kuchukua sheria mkononi badala ya kumfikisha kwenye vyombo husika?

Lakini pia kuna wale wanaokimbia mazima hasa kama gari sio lake 'mali ya tajiri'. Hapa chini ni ajali imetokea Kigoma Kasulu ambapo gari iligongana na pikipiki, dereva wa pikipiki alivunjika mguu na dereva wa gari aliamua kukimbia na kuacha gari.

Si ajabu dereva wa gari angebaki na kuamua kutafuta suluhisho la kumuwahisha mwenzake hospitali haraka lakini najiuliza hili zimwi la madereva kukimbia, tatizo ni 'wananchi wenye hasira kali' au madereva kuogopa kuyakabili matatizo ya ajali hasa wenye mabosi.
fp-eIw7dfHd8OsULrGYpXp06oGZEGRsTpRoF2Tjsr7wJiF9KDbIjjZr0-vgC2tnkq8CQ3Dun8ZjXEHkVGpLzhqOBPgLb2u-52ouj0f2Vgv0p-Wm9mzWN1U7S2Z8asc-hyEgkyCk4MxWpvSZS-c8S5rc8GX8BNrn99_eqga3kFdOl9UnA1Qhq6vP8FIBflnzJ=s0-d-e1-ft

BKcwakUWJc145ITg0HkQZChS8wJxu1lTeZQnhTTp36xUIkXYvpBTtmva7s5Q55EQuNeUBfdC4NiASpxKdWINvunmNa_ojLaVMeZU98m5tw_-WRrS-EaH33BoaUnvVpsQT8UTc9uV22rUyzWjgY6fO-tQsFpYRBvNvgOk8OLuqLqJNyPLcw7gtwWxRVXv8GLe=s0-d-e1-ftWananchi wenye hasira kali bila kusahau sheria wanazimiliki mikononi mwao.
 
Na kuna huu utaalamu wa kugongesha gari hadi halitamaniki, watu wengi kama sio abiria wote kufariki lakini unasikia dereva kakimbia, kuna mkanganyo wa mambo wakati mwingine!
 
Ndio maana wachina mabasi yao wanayotuletea bongo hayana mlango wa dereva. Angalia YUTONG, ZHONG TONG BUS n.k. Dereva kushuka hadi apitie mlango wa abiria
 
Kuna wale wanaokimbia kwa makusudi baada ya kutokea ajali ndio waliosababisha haya yote kufanya wengine wakimbie kwa ajili ya kujiokoa usalama wao
 
Mara nyingi ajali inapotokea watu huangalia sana athari za ajali yenyewe na alio au walioathirika ndio huonekana wasio kua na makosa kumbe inawezekana kabisa kua waathirika Wa ajali bila kujali majeruhi ama vifo kua ni wenye makosa na ndio chanzo cha ajali husika!kwa maana hiyo basi uelewa wa wananchi ndio uliosababisha madereva kukimbia na si wote ambao hukimbia hufanya kwa makusudi!siku hizi hukimbia kwa ajili ya kujiokoa!
 
Kheri umgonge mtembea kwa miguu kuliko mwendesha bodaboda.My friend hawa jamaa wanamshikamano sijawahi ona,uking'aang'aa sharubu eneo la tukio unaR.I.P

Mob justice ndo kisababishi cha madereva kutokomea.
 
Back
Top Bottom