Madawati na maadili ya watoto wetu

chabusalu

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
8,084
5,208
Wazo la kuandika uzi huu ninalipata nikiwa katika ghorofa ya kwanza ya jengo la ofisi za halmashauri ya wilaya moja mkoani Arusha. Nimesimama nikiwa ninasubiri kuingia kupata huduma katika ofisi mojawapo katika jengo hili. Kwa chini ninaona lundo la madawati yakipakiwa kwenye gari. Nilipododosa baadaye nikaambiwa yanapakiwa kwenye gari hilo ili yasambazwa katika shule mbalimbali katika halmashauri hiyo.

Ninapoyatazama madawati yale ninaona yote yana maandishi kutegemeana na taasisi iliyoyatoa ili kuitikia wito wa mheshimiwa Rais wa kuchangia madawati. Ninaona maandishi kama Kanisa la ..., ....Bar; nakadhalika. Tafakuri yangu inajikita katika madawati haya yaliyoandikwa.....Bar, kwamba madawati yale yamechangwa na bila shaka mmiliki wa bar hiyo ambayo kwa muktadha wa thread hii sina sababu ya kuitaja jina.

Ninafahamu kuwa nchi yetu ni secular state, lakini ninachotaka tuchangie hapa ni mtazamo wangu kwamba je, kwa kuwa tunawafundisha watoto wetu kwamba pombe si kitu kizuri kwao, rejea maandishi kwenye chupa kuwa hairuhusiwi kwa wenye umri wa chini ya miaka 18 (na makanisani na misikitini tunasema kuwa ni dhambi), kukalia madawati yanayosomeka mbele yao kuwa yametolewa na bar fulani haiwezi kuwa na athari kwao?
 
Back
Top Bottom