Madawa ya kulevya yapo Dar Es Salaam peke yake?

iCode

JF-Expert Member
Oct 16, 2013
762
446
Nawasalimu Watanzania Wenzangu,

Polenii na Hongereni kwa wafuatiliaji na wahabarishaji nguli katika sakata hili la madawa ya kulevya. Binafsi nampongeza Rais wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda kwa kuthubutu angalau kuanzisha hili. Japo ushirikiano anaoupata bado ni hafifu na hauridhishi.

Bila shaka Dar es Salaam ni jiji kubwa zaidi nchini na mambo mengi yanayoendelea nchini yanaanzia huko.. Lakini nimekuwa nikipata kigugumizi katika mikakati ya Rc Makonda dhidi ya mapambano haya.

Kwetu sisi wa huku kijijini ukitaka kumkamata ndege anayemaliza mazao shambani inabidi umnyemelee na kumkamata, ukimpigia kelele unampa mda wa kutosha kukimbia ili arudi tena. Mfano huu Unaendana sana operesheni hii. Ni wazi kwamba kiasi cha madawa kilichokamatwa ni kidogo mno ukilinganisha na kiasi kinachofikiriwa kuwepo. Hii ni kwa sababu unamtangaza mhusika kabla ya kujiridhisha na upelelezi uliofanyika. Ndio maana walioitwa wengi wanajiamini mno. Na wametoka mikononi mwa polisi tayari (wengi wao)
Swala la madawa ya kulevya ni zito na linahitaji deep analysis kabla ya kumtangaza mhusika/mdhaniwa hadharani.

NI DSM TU?
humu nyote mnajua kwamba hata huku mikoani matumizi ya madawa ya kulevya ni makubwa sana. Mikoa kama Arusha, Mbeya pamoja na Mwanza kwa mnaosafiri mnaona hali halisi ya vijana waishio maeneo ya stendi. Ni waathirika wakubwa.

Arusha bangi inaitwa '' kitu cha Arusha' maana yake kinatumika mpaka imekuwa normal. Naona makonda amewakurupua wauzaji na waingizaji, kuwakamata ni kazi ngumu mno kwa sasa. Ataishia kuwataja clouds.

RAI YANGU
~opération hii ikija mikoani ma Rc watumie mbinu za kisasa zaidi, wapate alibi kabla ya kumtangaza mtu.
~Rc wa dsm lazima atambue sasa kuwa mbinu yake ya kuwatangaza hadharani inafeli vibaya, awe na plan B ya kupambana na madawa hayo.
~Ni lazima Watanzania wote watambue kuwa hii vita si ya Makonda na ya Dar es Salaam peke yake, hii iende kwenye ngazi ya familia
~Tusiwe na mihemuko ya kisiasa yunapodili na hili hata kama waanzilishi wake wana dalili ya kuwa na malengo hayo ya kisiasa

RC GAMBO wa Arusha anza operation hii kwa mbinu za kisasa zaidi. Maana mkoani kwako kuna mitaa haipitiki ikishafika saa 12. Sitilii mashaka jitihada zako.
 
Asante YEHODAYA ila promo ipo dsm peke yake... 17?? Hongera mh Rc wa Shinyanga
 
Back
Top Bottom