Madawa ya kulevya yakamatwa Mirerani

esther mashiker

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
616
Reaction score
555
Polisi mkoani Manyara wamewakamata watu 2, kwa makosa ya kujihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya ambayo kwa Tanzania ni kinyumke cha kisheria .

Akitibitisha kukamatwa kwa madawa hayo kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Augustino Senga amesema, huko katika wilaya ya Kiteto amekamatwa Ramadhani Kombo mwenye umri wa miaka 20 akiwa na Kete 24 za Bangi wakati anapekuliwa ili kuingizwa mahabusu kwa kosa la uvunjaji ikiwa ni kosa la lingine la aina hiyo kwa mtuhumiwa huyo.

Aidha katika mji mdogo wa Mirerani katika geti la kuingilia kwenye machimbo ya Tanzanite wakati wa upekuzi wa kawaida walimkamata Jacob Ngoti mwenye umri wa miaka 43 akiwa na misokoto 1248 yenye uzito wa kilogram 2.740 akiwa ameiweka kwenye begi la nguo la mgongoni ili asiweze kugundulika kirahisi.

Madawa hayo, alikuwa anakwenda kuwauzia wachimbaji wanaofanya kazi za uchimbaji ndani ya Ukuta wa Madini maarufu kama ukuta wa Magufuli.

Kamanda wa Polisi Augustino Senga amesema kuwa jeshi hilo lipo makini na halitamvumilia mtu yeyote anaejishugulisha na uuzaji au utumiaji wa madawa ya kulevya.
 
Hapa nimechanganyikiwa Mimi navyoelewa bangi ni bangi na madawa ya kulevya ni unga! Sasa bangi nayo kumbe pia ni madawa ya kulevya?
 
Sikuisoma muda mrefu nilijua tu kama sio milaa ni bangi sema kiki tuu kila shimo kuna bangi za kutosha watu wanawezaje kushuka chini kama wapo sawa...mtakosa Madini kisa kuzuia bangi isipelekwe chini ya ardhi...
 
Sikuisoma muda mrefu nilijua tu kama sio milaa ni bangi sema kiki tuu kila shimo kuna bangi za kutosha watu wanawezaje kushuka chini kama wapo sawa...mtakosa Madini kisa kuzuia bangi isipelekwe chini ya ardhi...
Si ndy hapo

Ova
 
Hii mambo ya kuweka bangi kwenye kundi la madawa ya kulevya sijui wanawaza nini


Ule mmea uachwe ulivyo jamani au utafutiwe kundi lingine la kuwekwa

Mererani unakaaje bila kula kaya ?
 
Mimi nikajua wamekamata vitu konki kumbe bangi tu..
Sasa bangi ni madawa ya kulevya?
 
Mirerani hasa wanaapolo bila kuvuta bangi kazi hawafanyi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…