Madaraka Nyerere anaomba kueleweshwa

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Vitu viwili sijavielewa:
1. Kuzuwia watu kuombea wagonjwa wapone
2. Dhana ya kwamba Mwenyezi Mungu hatapokea sala nikimuomba peke yangu chumbani.

My Take;
Kaka Madaraka jitokeze hadharani ukemee matendo maovu yanayofanywa na serikali. Hii ya mbinu ya kimafumbo haitoshi. Simama uhesabiwe. Naamini baba yako angekuwa hai asingechelewa hata dakika moja kupinga matendo haya ambayo hayakubaliki. Mtendee haki Julius Kambarage
 
0ed3414f19c37493a3e72c9284f2398e.jpg
 
Nyerere kama unafikiri alitenda haki umepotea sana tena sana maana mengi ya yaliotokea aliweka yeye misingi
Ameongoza nchini kwa miaka karibu 25. Alikosea. Naye alikiri kuwa kuwa kuna sehemu alikosea. Na kuomba msamaha kwayo..tena toka mwaka 1985. Lakini, 1995 aliwaambia "tatizo lenu mnaacha mazuri (mambo ya msingi) mnachukia ya kipumbavu"
Leo 2017, bado hamfundishiki hata baada ya darasa lile la 1995.
 
Babako alifungia vyama vya upizani ili kuunganisha nchi. Watu watumie makanisa Na misikiti kuomba. Ukumbuke babako alifungia makanisa ya kilokole. Hadi Mzee Mwinyi kurusu kuingia nchini. Uwadanganye watoto wa 1980/2000 wanatumia SIMU siku hizi
 
CCM ni chama cha laana. Mbele ya camera utasikia mniombee... halafu huku anawanyanyasa wanaoliombea taifa
 
Mkuu alianza vizuri mwanzoni kutumbua majipu na kuzunguka kukagua miradi kwa kushtukiza.
Mpaka kila mtu akajua kuwa kufukia 2020 hakutakua na haja ya kampeni mana hata mitandaoni mijadala ilikuwa imepotea kabisa.
Kosa kubwa lilianzia pale bunge lilipoanza kuzuiwa. Watu wakaanza kujiuliza kunani mpaka mawaziri hawataki kupigwa maswali magumu na kutupiwa lawama live wakati wameajiriwa kwa kodi ya watanzania?
Watu wakaanza kupata mambo ya kupigania. Hoja ya bunge LIVE ikaanza. Watu wakapata mahali pa kushika. Sababu za mapungufu zikaanza kutajwa kwa kurejea na bunge live. Laite wangeshtuka na kuliweka Live mkuu wa nchi angehamishia udhaifu wa serikali kwa wabunge wanao lala bungeni.

Mambo ya mpasuko wa kisiasa kule Zanzibar nalo pia lilikua ni jambo la kuliundia tume kama alivyofanya Mkapa na JK sio kwa lengo la kumwondo aliyeapishwa la hasha bali kwa lengo la kumfariji aliyekosa kwa shingo upande. Wote ni watanzania na wazanzibar tulipaswa tusiishi kwa namna hiyo bali upendo hata kama mmoja hajaridhika ni watoto wa baba mmoja tulitakiwa tuwaite kwa pamoja na kuwapatanisha.
Biblia natuambia kuwa heri wapatanishi maana hao wataitwa wana wa Mungu. Hili nalo likaleta visababu ambavyo wala havikuwa na umuhimu kama taifa moja.

Akaja tena na katazo la mikutano ya kisiasa.
Ikaleta tena sababu za udhaifu wa serikali. Hili likaibua tena mijadala. Watu wakawa hawafuatilii tena masuala ya utendaji bali haya mapungufu ambayo hayakuwa na sababu yoyote mana yapo kikatiba.

Wakaja tena na makatazo ya kutembeleana kati ya wanachama wa chama kikubwa na vile vinavyopingapinga. Watu wa chama kikubwa wakajikuta wanalazimika kujionyesha kuwa wanafuata kauli hizo kwa speed kubwa na kuonyesha misimamo mikali kama gia ya kwenda na speed.

Watanzania wakakatazwa tena kutembeleana kwenye majimbo kwa lengo la kuhamasisha maendeleo kama hawajachaguliwa na watu wa eneo lake.
Yani kama wewe ni mtu kutoka X ubaki huko huko X ukionekana unazungumza na watu wa Y basi inakuwa ni kosa la kukuweka ndani masaa 48 na kupelekwa mahakamani ukatokee huko . Chuki ikaingia miongoni mwa watanzania.Watu wakawa hawatembeleani wala kusalimiana kama tulivyoona wakati mmoja mtu akipewa mkono na kuukataa.
Na wito ukatolewa kuwa alipaswa asisainiwe hata fomu zake za matibabu . Lilikua ni jambo jepesi tu la kufanya kazi ya wana wa Mungu ya kuwaita na kuwapatanisha kwa kumwambia hii hapana kwa nini unakataa kusalimiana na mwenzako. Unajenga taswira gani kwa wananchi. Bila shaka mambo yangeenda vizuri sana.

Ubinadamu ukaanza kutoweka taratibu. Watu wakawa hawaoni tena thamani ya binadamu. Kule kibiti watu wakawa wanaua kwa makusudi kabisa.

Wengine wakawa wanapotea.

Leo hii watu tena hawafuatilii nani kafanya zuri lipi bali nani aliyefanya baya lipi?

Haya yote yamepoteza uelekeo wetu wa kuelekea kwenye nchi ya viwanda na sasa watu wanaishi kwa jazba na kukimbizana na vikundi vya wanamaombi wanaomlilia Mungu kuhusu kesho yao.

Nchi ikimwaga damu zisizo na hatia kinachofuata ni watu wema wasio na nguvu kulesha na kumwomba mana hawajui siku wala saa ya damu yao kumwagwa.

Wachamungu tusimame na kumwomba Mungu aturejeshee amani ya mioyo yetu. Watu wabishane kwa upendo na baada ya kubishana washikane mikono.
Wakati ule wa kuitana mafisadi kuna watu walitukanwa sana tena kwa maagizo lakini walikua wanasamehe na kucheka wanapokutana iwe kwenye shida au raha.

Naamini kwamba tunaweza kupambana na ufisadi na uzembe bila kuuana. Tuwaondoe wale viongozi wanaotuhumiwa wakae pembeni sio kuwaondoa wanasiasa wasio na hatia ili washindwe kufanya kazi zao.

Tuwatishe wanaoiba mali za umma sio kuwatisha watu wanaosoma dua. Ni ajabu kabisa kama tutaona watu waliovaa tisheti za kuhamasisha maombi wakifungwa ili hali walioiba mali za umma wakila bata mitaani.

Kuvaa nguo yenye nembo na maandisho ya kumwomba mwenyezi Mungu sio kosa lakini kuna watu wanaitangazia na kuionya jamii kuwa wajiepusha na nguo hizo na kuachana na kumwomba Mungu aponye wagonjwa na aiepushe nchi yetu dhidi ya wauaji na watu wabaya wasiojulikana.
 
Nyerere kama unafikiri alitenda haki umepotea sana tena sana maana mengi ya yaliotokea aliweka yeye misingi

Kweli kabisa na hata baadhi ya hotuba zake zinachangia huu upumbavu wa CCM
 
Vitu viwili sijavielewa:
1. Kuzuwia watu kuombea wagonjwa wapone
2. Dhana ya kwamba Mwenyezi Mungu hatapokea sala nikimuomba peke yangu chumbani.

My Take;
Kaka Madaraka jitokeze hadharani ukemee matendo maovu yanayofanywa na serikali. Hii ya mbinu ya kimafumbo haitoshi. Simama uhesabiwe. Naamini baba yako angekuwa hai asingechelewa hata dakika moja kupinga matendo haya ambayo hayakubaliki. Mtendee haki Julius Kambarage

Baba yake Madaraka alikuwa Mafya hatareee Magu cha Mtoto

Wapi Karume wapi Sokoine!

Alipomkosa kosa Oscar Kambona aliekimbilia Uingereza Kama Mkimbizi wa Kisiasa alitaifisha kila kitu chake mpaka Nyumba zake za Dar na ile ya Kule Nyasa kwa Wazee wake.

Kusomeka tu Rafiki wa Kambona ilikuwa Uhaini, Mzee John Lifa Chipaka na Emanuel Makaidi walifungwa Maisha kwa Uhaini Kama sio Mahakama ya EA wangefia kule
 
Back
Top Bottom