Kwa ushauri wangu, serikali inatakiwa kuanzisha Agency itakayokuwa inashughulikia taka za aina zote (solid, gaseous and liquid wastes). Ukitembelea sehemu nyingi nchini hari inatisha na mamlaka zilizopo ni kama zimeshindwa kuja na ubunifu wa kuwa na njia za kisasa za kudhibiti taka. Tukipata watu wenye akili timamu taka ni malighafi, kwa sasa nchi zilizoendelea lugha ya takataka inabadilika na kutakuwa hakuna takataka, kwani taka nyingi kwa sasa ni malighafi za aina mbambali kulingana na aina ya taka. Kwani nchi nyingine kwa sasa wanazalisha mbolea, umeme, au recycling kama zile za karatasi, glasses, chuma chakavu na plastics. Hivyo taka imekuwa sehemu kubwa ya ajira. Lakini pia taka zile hatarishi zenye kemikali kutoka viwandani zisipodhibitiwa vizuri zinaweza kuleta madhara makubwa katika jamii, kama vile vifo na ulemavu. Hivyo, kwa unyeti wa suala hili naishauri serikali ianzishe taasisi yenye mamlaka kamili kushughulikia tatizo hili .