Madaktari watumbuliwa wilayani Malinyi

Madaktari watumbuliwa wilayani Malinyi

Joined
Jul 19, 2016
Posts
9
Reaction score
5
MADAKTARI WATUMBULIWA - Malinyi

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoa wa Morogoro, Marcelin Ndimbwa amewasimamisha kazi Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Matimbira, Dk Severiana Mayenja, Daktari wa zamu, Dk Evelyne Tenes na Tabibu wa zamu, Nsallu Masembo kwa tuhuma ya kufanya uzembe, mazoea na kutowajibika ipasavyo katika kutoa huduma kwa wananchi kulikokithiri.

Amechukua hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho cha afya kuanzia saa 5:55 hadi 8:45 usiku juzi ambako alimkuta mjamzito, Doreen Konga akiwa katika hali mbaya huku mwili wake ukiwa umeanza kubadilika rangi kwa ajili ya maumivu baada ya kushindwa kujifungua.

Mkurugenzi huyo anadai kuwa mgonjwa huyo alitelekezwa na mganga wa zamu.

Katika ziara hiyo, mkurugenzi huyo alifuatana na Ofisa Utumishi wa Wilaya, Bhango Lyangwa, Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Idd Mujungu na alitaka kujiridhisha na hali ya uwajibikaji ya watumishi kwenye kituo hicho kwani amekuwa akipokea malalamiko ya muda mrefu na mfupi kutoka kwa raia wema na kuangalia namna ya kuyatatua kwa haraka zaidi.

Hii ni mara ya pili kwa mkurugenzi huyo kutembelea kituo hicho kwani alifanya ziara ya kushitukiza Agosti 10, mwaka huu saa 6:00 usiku na hakukuta tabibu yeyote wala muuguzi huku wagonjwa sita wakiwa wameishiwa dripu za dawa kwa zaidi ya saa mbili.

Mkurugenzi huyo alipofika katika kituo hicho akiwa na ofisa utumishi wa wilaya na mganga mkuu wa wilaya, walimkuta muuguzi wa zamu, Martha Hiiti na baada ya mahojiano alimweleza mkurugenzi huyo na ujumbe wake kuwa saa 3:00 usiku alimwita daktari wa zamu kumwarifu habari za mgonjwa huyo, lakini hakuonekana hadi ilipofika 5:15 usiku; na alipofika alitoa fomu ya rufaa na kumwamuru aijaze fomu ya rufaa bila kumhudumia mgonjwa na kuondoka.

Mganga wa zamu, Nsallu Masembo hakuwepo kituoni hapo na alipopigiwa simu, hakupokea hadi alipofuatwa na mlinzi usiku huo nyumbani kwake.

Muuguzi huyo aliwaeleza viongozi hao kwamba aliachwa aendelee na huduma bila kusaidiwa na daktari wala tabibu wa zamu na akishindwa aandike rufaa.

Baada ya jitihada za kuwatafuta madaktari kushindikana na kwa viongozi na muuguzi kupokezana kwa simu, mkurugenzi aliamuru mgonjwa aliyekuwa na hali mbaya, kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Malinyi ya Lugala. Baada hapo, aliamua kuwasimamisha kazi wafanyakazi hao wa kituo cha afya na akaunda tume ndogo ya uchunguzi.
 
Mkurugenzi katoa rufaa..

Haya masuala ya Afya watu tuwe makini sana..

DED ipo siku atakutwa OPD ili naye ainekane anafanya kazi.

Anyway; adhabu hiyo ya kufukuza madakitari ni ukurupukaji!!
 
Wapi umesoma wamefukuzwa? Uzi unasema wamesimamishwa

Nina mashaka kama umesoma huu uzi kama unatetea uzembe wa hao madaktari
 
Mkurugenzi katoa rufaa..

Haya masuala ya Afya watu tuwe makini sana..

DED ipo siku atakutwa OPD ili naye ainekane anafanya kazi.

Anyway; adhabu hiyo ya kufukuza madakitari ni ukurupukaji!!
Kama wamefanya uzembe wametendewa sawa kabisa,hawa waganga na wauguzi mbalimbali walikua na baadhi yao wanafanya mambo kwa kutojali na muda mwingine kutoa huduma chini ya kiwango na watu wanashindwa kuhoji kwasababu ya ujinga.Suala la kuacha hadi mgonjwa anazidiwa na anaanza kubadilika rangi in sawa na jaribio la kuelekea kuua.Sioni ubaya wa hiyo adhabu,uelewa ukikua kwa wananchi wataanza kujua ubovu wa huduma zinazotolewa na baadhi ya matabibu,ngoja awareness iendelee kupanuka miongoni mwa wanajamii.
 
sheria ichukue mkondo wake sie si watu wa mchezo mchezo kwenye mambo ya afya
 
Ukitaka kujua huyu DED alichofanya ukione sawa umwa ghafla afu nenda hospital ya serikari afu hauna unaemjua ndo utaona sawa tu...
Et daktar anakuja anatoa rufaa anasepa hahahahahha ahatari sana

Ile hospitali pale kilimani rock city unaumwa emergency inahudumia utazani we sio wa emergence
Mgonjwa kazidiwa anakaa chini hamna hata nesi anayejali wanampita
Aseeee acha tu
 
Yakiwa hayajakukuta utaona kakosea ila kama yamewahi kukukuta utaona sawa.
 
Mkurugenzi katoa rufaa..

Haya masuala ya Afya watu tuwe makini sana..

DED ipo siku atakutwa OPD ili naye ainekane anafanya kazi.

Anyway; adhabu hiyo ya kufukuza madakitari ni ukurupukaji!!

NDUGU YANGU WEWE MPUUZI..UNAAMBIWA MGONJWA ALIANZA KUBADILIKA RANGI NA HAKUNA WAKUMHUDUMIA SASA ULITAKA MKURUGENZI ASIMUSAIDIE MGONJWA KWA KUPELEKA HOSPITAL ILIYOKO KARIBU ILI KUOKOA MGONJWA.MIE NI CAHDEMA NA SIAMINI KAMA TUNGEPATA MADARAKA TUNGEKUBALI KUFANYA NA KUSAPORT UJINGA WA DR ALIOUFANYA
 
Kuokoa Marsha Ya mgonjwa ni bora,protocol baadae,alichokifanya mkurugenzi ni sahib na hata kama ingekuwa wewe ukiwa na akili timamu bila viroba ungefanya kama alivyofanya mkurugenzi,na ishukuriwe roho ya bwana alimwongoza mkurugenzi kutembelea hospitali na mgonjwa kuokolewa,vinginevyo
angepoteza maisha.
 
MADAKTARI WATUMBULIWA - Malinyi

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Malinyi Mkoa wa Morogoro, Marcelin Ndimbwa amewasimamisha kazi Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Matimbira, Dk Severiana Mayenja, Daktari wa zamu, Dk Evelyne Tenes na Tabibu wa zamu, Nsallu Masembo kwa tuhuma ya kufanya uzembe, mazoea na kutowajibika ipasavyo katika kutoa huduma kwa wananchi kulikokithiri.

Amechukua hatua hiyo baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika kituo hicho cha afya kuanzia saa 5:55 hadi 8:45 usiku juzi ambako alimkuta mjamzito, Doreen Konga akiwa katika hali mbaya huku mwili wake ukiwa umeanza kubadilika rangi kwa ajili ya maumivu baada ya kushindwa kujifungua.

Mkurugenzi huyo anadai kuwa mgonjwa huyo alitelekezwa na mganga wa zamu.

Katika ziara hiyo, mkurugenzi huyo alifuatana na Ofisa Utumishi wa Wilaya, Bhango Lyangwa, Mganga Mkuu wa Wilaya, Dk Idd Mujungu na alitaka kujiridhisha na hali ya uwajibikaji ya watumishi kwenye kituo hicho kwani amekuwa akipokea malalamiko ya muda mrefu na mfupi kutoka kwa raia wema na kuangalia namna ya kuyatatua kwa haraka zaidi.

Hii ni mara ya pili kwa mkurugenzi huyo kutembelea kituo hicho kwani alifanya ziara ya kushitukiza Agosti 10, mwaka huu saa 6:00 usiku na hakukuta tabibu yeyote wala muuguzi huku wagonjwa sita wakiwa wameishiwa dripu za dawa kwa zaidi ya saa mbili.

Mkurugenzi huyo alipofika katika kituo hicho akiwa na ofisa utumishi wa wilaya na mganga mkuu wa wilaya, walimkuta muuguzi wa zamu, Martha Hiiti na baada ya mahojiano alimweleza mkurugenzi huyo na ujumbe wake kuwa saa 3:00 usiku alimwita daktari wa zamu kumwarifu habari za mgonjwa huyo, lakini hakuonekana hadi ilipofika 5:15 usiku; na alipofika alitoa fomu ya rufaa na kumwamuru aijaze fomu ya rufaa bila kumhudumia mgonjwa na kuondoka.

Mganga wa zamu, Nsallu Masembo hakuwepo kituoni hapo na alipopigiwa simu, hakupokea hadi alipofuatwa na mlinzi usiku huo nyumbani kwake.

Muuguzi huyo aliwaeleza viongozi hao kwamba aliachwa aendelee na huduma bila kusaidiwa na daktari wala tabibu wa zamu na akishindwa aandike rufaa.

Baada ya jitihada za kuwatafuta madaktari kushindikana na kwa viongozi na muuguzi kupokezana kwa simu, mkurugenzi aliamuru mgonjwa aliyekuwa na hali mbaya, kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Malinyi ya Lugala. Baada hapo, aliamua kuwasimamisha kazi wafanyakazi hao wa kituo cha afya na akaunda tume ndogo ya uchunguzi.
Dahh.... Hii mpya... Mwili kubadirika rangi kwa ajili ya maumivu kwa kushindwa kujifungua wajuzi wa Tiba mtusaidie.. Obstructed labor.... Premature labor...kwa elimu yangu ndogo niliyonayo sikubali maramoja kuwa Maumivu ya uchungu yaweza sababisha mwili kubadirika rangi.. Labda mgonjwa alipata "hypoxia" au alikuwa "anemic" ila yote kwa kwa yote kama kuna maadaili yalikiukwa basi sheria zifuatwe na wahusika wawajibishwe.
 
Madaktari tushawazoea usiku wanajifanya wanaenda kazini wanasaini then wanaenda kwa michepukooo
 
Back
Top Bottom