Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,348
- 26,144
Chama cha Madaktari Tanzania kimelaani kitendo cha kutupwa miili ya binaadamu kilichofanywa na IMTU. Dr.Primu Saidia,Rais wa chama hicho ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Dr. Saidia amesema kitendo hicho ni kinyume na taaluma ya udaktari,utu na haki za binaadamu. Amesema kitendo hicho kinatosha kabisa kuifungia taasisi iliyohusika.
=======================================================
CHAMA cha Madaktari Tanzania pamoja na Jamii ya Madaktari nchini Mathematical Association of Tanzania (MAT), kimeitaka Serikali kukifungia Chuo Kikuu cha Madaktari, International Medical and Tecknological University (IMTU) cha Dar es Salaam na kuwachukulia hatua wote waliohusika na sakata la utupaji wa masalia ya binadamu kwa kuwa kimekiuka sheria, taratibu, utu, maadili ya ufundishaji na taaluma ya udaktari.
Rais wa Chama Cha Madaktari Tanzania, Dkt. Primus Saidia, amekaririwa na FikraPevu Julai 23, 2014 na akisema miili na viungo vya binadamu hutumika kwa heshima kubwa kwa kufuata taratibu za kuipata, kuisafirisha, kuhifadhi, kuitumia na kusitiri mabaki baada ya matumizi hufanyika, kwa kufuata sheria, maadili na afya ya jamii, utamaduni miiko na utu kwa mwili wa binadamu na jamii husika.
Kwa upande wake Daktari Bingwa wa Afya ya Akili katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prakseda Swai, amesema kitendo kilichofanywa na IMTU kinaweza kuathiri wananchi kisaikolojia na kupata hisia yenye madhara kwa afya ya akili ikiwemo ndoto na msongo wa mawazo unaosababisha kumkosesha binadamu usingizi pamoja na kupoteza hamu ya kula.
Wakati huo huo...
Habari zaidi, soma=> http://www.fikrapevu.com/sakata-la-...ikifungie-chuo-cha-imtu/#sthash.0yLIht9F.dpuf