Madaktari wa Tanzania wafanya upasuaji wa kihistoria

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,292
Madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.

Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu.

160525142944_muhimbili_tanzania_bypass_heart_surgery_2_640x360_bbc.jpg

Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa Bashir Nyangasa ameambia BBC kuwa upasuaji huo wa kupandikiza mishipa ya damu nje ya mshine ni wa kihistoria nchini Tanzania.
Mgonjwa anaweza kutolewa mishipa ya damu kutoka miguuni au mikononi baada ya kupewa dawa ya usingizi na mishipa hiyo kupandikizwa kwenye mshipa wa moyo uliokuwa umeziba ili kuruhusu mzunguko wa damu wa moyo kama kawaida bila kutumia mashine,” amesema.

Upasuaji huo wa moyo kwa njia ya kupandikiza umefanyika kwa watu wawili, ambao umeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hali zao zinaendelea vizuri .

Dkt Nyangasa amesema kwa sasa hakuna haja ya Watanzania wenye matatizo ya moyo kwenda nje ya nchi kwa kuwa wao kama wataalam wameweza kufanya upasuaji huo
Anasema madaktari sasa wanaweza kuhudumia wagonjwa wengi zaidi wenye uhitaji na kupunguza gharama kwa serikali ya kusafirisha wagonjwa wa moyo nje ya nchi.

Mwandishi wa BBC aliyepo Dar es Salaam Esther Namuhisa anasema wengi wa wagonjwa wamekuwa wakisafiri hadi India ambapo wengi hukumbana na changamoto nyingi kupata huduma hiyo kifedha na hata kwenye upande wa lugha.

160525143227_muhimbili_tanzania_bypass_heart_surgery_3_640x360_bbc.jpg
 
Bei zao ni nafuu kiasi kwamba kajamba nani tutaweza kuzimudu au ndio kwa ajili ya matajiri?
 
heko madaktari wa Tanzania.. washikeni sana hao wahindi msiwaache waende zao bila kuwapa ujuzi wa kutosha
 
Yaan i am speechless kwa wataalamu wanaelewa zaidi This is one milestone we have achieved .Kama tunafanya bypass surgery hamna sababu kwa mtu kwenda nje kwa matatizo ya moyo labda kwa very complicated if not rare case
 
Hongera mh rais mstaafu dk jakaya kikwete kwa wazo na uanzishwaji wa tasisi hii muhimu kwa nchi yetu.
Taifa litaendelea kukukumbuka kwa mchango wako mzuri kwa taifa hili ikiwemo uanzishwaji wa taaasisi hii.
Mungu akupe afya na umri mrefu

Hongera dk kikwete hongera prof mohammed janabi
 
Madaktari wa Tanzania katika hospitali ya taifa ya Muhimbili, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, wakishirikiana na wenzao wa India wamefanikiwa kufanya upasuaji wa moyo wa aina yake Tanzania.

Upasuaji huo ujulikanao kama ‘bypass surgery’ ulishirikisha kupandikizwa kwa mishipa ya damu kutoka sehemu nyingine ya mwili moyoni bila kutumia mashine ya kusimamisha moyo na mapafu.

160525142944_muhimbili_tanzania_bypass_heart_surgery_2_640x360_bbc.jpg

Kwa kawaida madaktari wanasema upasuaji wa moyo hufanyika baada ya moyo na mapafu kusimama, lakini upasuaji huo ulifanyika wakati moyo na mapafu vikifanya kazi.

Daktari bingwa wa upasuaji wa moyo na mishipa Bashir Nyangasa ameambia BBC kuwa upasuaji huo wa kupandikiza mishipa ya damu nje ya mshine ni wa kihistoria nchini Tanzania.
Mgonjwa anaweza kutolewa mishipa ya damu kutoka miguuni au mikononi baada ya kupewa dawa ya usingizi na mishipa hiyo kupandikizwa kwenye mshipa wa moyo uliokuwa umeziba ili kuruhusu mzunguko wa damu wa moyo kama kawaida bila kutumia mashine,” amesema.

Upasuaji huo wa moyo kwa njia ya kupandikiza umefanyika kwa watu wawili, ambao umeonesha mafanikio makubwa kwa kuwa hali zao zinaendelea vizuri .

Dkt Nyangasa amesema kwa sasa hakuna haja ya Watanzania wenye matatizo ya moyo kwenda nje ya nchi kwa kuwa wao kama wataalam wameweza kufanya upasuaji huo
Anasema madaktari sasa wanaweza kuhudumia wagonjwa wengi zaidi wenye uhitaji na kupunguza gharama kwa serikali ya kusafirisha wagonjwa wa moyo nje ya nchi.

Mwandishi wa BBC aliyepo Dar es Salaam Esther Namuhisa anasema wengi wa wagonjwa wamekuwa wakisafiri hadi India ambapo wengi hukumbana na changamoto nyingi kupata huduma hiyo kifedha na hata kwenye upande wa lugha.

160525143227_muhimbili_tanzania_bypass_heart_surgery_3_640x360_bbc.jpg
Hii tabia ya viongozi wa juu kuazisha miradi kwa pesa za uma Kisha kuibatiza majina yao lazima ikome eg daraja la mkapa, daraja la kikwete, taasisi ya kikwete nk vikemewe, tumuige jk nyerere, hakujikweza bali alikwezwa baada ya kifo chake
 
Back
Top Bottom