Madaktari shirikianeni wote msidanganyike | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Madaktari shirikianeni wote msidanganyike

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiumbe duni, Jan 27, 2012.

 1. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #1
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ushauri wangu kwa maktari waliogoma wasidanganyike na ahadi waliyopewa na serikali kwamba waingie kazini wakati serikali inashughulikia madai yao. Kinachoshangaza wabunge walijiongezea posho kimya kimya bila kujadiliwa, lkn madaktari wanapotadai maslahi yao serikali inawatisha na wengine kuwahamisha, juna haki kweli hapa? Naju wanaoathirika ni wananchi wa kipato cha chini kwa sababu vigogo pamoja na familia zao hawatibiwi kwenye hospitali za serikali, lkn ni uzembe wetu wenyewe tungeingia barabarani kama kuishinikiza serikali isikilize kilio cha madaktari. Tumekuwa waoga sana kudai haki zetu kwa kuogopa virungu vya FFU lkn tukiendelea kufa kwa kukosa mtibabu woga utatutoka. Madaktari shikilieni msimamo wenu huohuo msidanganyike. Nawasilisha
   
 2. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  "Kwani kwa kuungana kwenu hakuna mtakacho poteza zaidi ya Minyororo Mliyofungwa kwa muda mrefu" Shime madaktari
  Mkitaka kujua hawawajali jiulizeni Kikwete yupo wapi na Kwanini jana Pinda Mizengo Hakukutokea kwenye mkutano wenu.
   
 3. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #3
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tulikuwa gizani, sasa tumezinduka ni lazima umuhimu wetu ujulikane.
   
 4. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Mi naona JF tukahamasishe wagonjwa waliolazwa MNH, MOI na ORCI wajifunge mashuka ya hospitali waandamane kwenda ikulu kudai wapewe tiba.
   
 5. K

  Kiumbe duni Senior Member

  #5
  Jan 27, 2012
  Joined: Dec 3, 2011
  Messages: 100
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo nalo neno
   
 6. Dr.Chichi

  Dr.Chichi JF-Expert Member

  #6
  Jan 27, 2012
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 2,336
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  ngojja tudischarge vichwa vya milembe vikafanye tour bungeni labda ndo tutasikilizwa
   
 7. Mromboo

  Mromboo JF-Expert Member

  #7
  Jan 27, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 728
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 45
  Ndugu zangu wanaJF, huku Moshi madaktari wanagonga supu tu kwenye migahawa huku wagonjwa wanalia mno. Ila ni halali yao kabisaaaa. hivi fikiria nchi iko kwenye matatizo ya maslahi ya wafanyakazi then JK anapanda ndege PRIVATE kwenda kula bata huko ulaya. Nauliza! JE, HUU NI UNGWANA NDUGU ZANGUNI? Garama ni 300,000,000. only for 4 days. Nawashauri na madaktari bingwa wakanywe supu pia huko mitaani. Ni taifa gani lenye rasimali nyingi hivi watu tunaonewa then tunakaa kimya kama karunguyeye alishikwa miiba yake? wana JF kuna uwezekano hato WBONGO tukiingiliwa ndoa zetu tunakaa kimyaaaaa!!!!!!!!!!!!!! Hebu fikiria Jana Kinana yuko Dar anaongelea masuala ya uchaguzi wahati watu wanakufa huko MNH. Nauliza tena ndugu zanguni HUU NI UNGWANA? sisi wana JF tusipochukua jukumu la kuielimisha hii jamii nani atafanya? I will never be the same again. Naomba kuwasilisha.
   
Loading...