Madaktari semeni tu tusile nyama sio kila siku mnabadili masharti ya ulaji nyama

The Evil Genius

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
6,002
19,449
Doctors wekeni wazi kama vipi watu tusile nyama kabisa ieleweke, sio jila kukicha mnaleta masharti ya ulaaji nyama.

Mmesema tusile nyama nyekundu, tumekubali, tumeacha, mkasema tule nyama nyeupe kama kuku au samaki, tumekubali.

Gafla mnasema kula kuku uondoe ngozi, usile ngozi ule ile nyama yenyewe, hapo ndio ugomvi wangu na nyie ulipo, kuku bila kula ngozi yake hiyo hujala kuku umekula kitu kingine.

Inakoelekea mtakuja kusema hata hata hiyo nyama ya kuku tusile tule utumbo wa kuku na utumbo wa samaki.

Wekeni wazi ijulikane moja hamtaki tule nyama au mseme kabisa watu tusile nyama sio kila siku kuja na masharti mapya, kuku bila ngozi sio kuku..

I respect you doctors, tusitaftane ubaya.
 
Wamasi mbona wanakula nyama tena nyekundu kwa muda wote lkn haileti madhara yoyote kwao.
 
Hujawaelewa madaktari..Hawajasema usile red meat..Ibanike kwanza upunguze kiwango cha lehemu ambacho kinaweza kukuletea maradhi ya moyo na mishipa ya damu.Altenatively unaweza kula nyama nyeupe yenye kiwango kidogo na kisichodhuru cha lehemu.Na kwa sababu nyama nyeupe zinazopatikana kwa wingi ni samaki na kuku wa kizungu,unapokula kuku wa kizungu usile ngozi na mifupa kwa sababu hizo ndizo sehemu ambazo harmful metabolites za yale madawa mnayowalisha hao kuku ndio zinakuwa concentrated
Kama wala kuku wa kienyeji wa Kibaha au samaki sato wa Nyanza hakuna matata
 
Ok, huwa sili kuku wa kisasa, ni wa kienyeji tu.
 
Ok, huwa sili kuku wa kisasa, ni wa kienyeji tu.
Siku hizi hata hao tunaowaita wa kienyeji wanakuwa ni wa mayai (Layers). Kuna siku nilikutana na washkaji katika bar zetu hizi maarufu Mitaa ya Sinza..nikaagiza mchemsho wa kuku wa kienyeji. Nilipoletewa mezani ile supu ikawa ina viungo (tangawizi na vitunguu saumu) vimezidi sana. Nilifikia kutafuna paja nikakutana na kuku wa mayai. Zamani sana nyumbani mama alifuga kuku wa mayai, mara kwa mara ilikuwa wanapikwa home na ile taste haijawahi kunitoka kinywani mpaka Leo.
 
...dah mimi bila shingo na vipapatio bado sijala kuku!..naanzaje sasa kutoa ngozi kwa mfano!
...sijaja kuishi milele,liwalo na liwe!

Aaaaah aaah. Mkuu subiri ukianza kuugua magonjwa yatokanayo na ulaji wa vyakula hivyo ndipo utausikilizia muziki wake. "Ningejua...." haitakukauka mdomoni.
 
Hawa wataalamu wakati mwingine wanatuchanganya sana na ukisema uwe unausikiliza kila ushauri wa hawa wataalamu unweza kuja kijuua mwenyewe kwasababu kuna wataakamu wengine wanasema unywe maji mengi lakini kuna wengine wanasema kama unakunywa maji mengi wakati unatatizo kwenye mwili wako.
 
Back
Top Bottom