Kiwango cha posho ya Tsh 5000 kwa siku kwa mwanachuo kwa mazingira ya sasa kwa Tanzania, ni kiwango kinachoweza msaidia kama anaakili ya kupanga vizuri bajeti yake. Kama wanachuo wanataka kuishi kwenye hoteli za gharama au kifahari ni jukumu lao na wazazi wao kuongeza pesa za kujikimu kifahari. Kiwango cha Sh laki moja na nusu kwa mwezi kama yuko makini na kufikiria zaidi future yake anaweza panga vizuri bajeti na akaishi bila tatizo kubwa. Ila kama anataka awe anakwenda kula Hamburgers McDonalds ni juu yake na familia yako kuongeza matumizi.
Tumepitia vyuo vya Tanzania na tumepitia vyuo vya mataifa makubwa, kwa ulinganifu katika masuala ya posho naweza sema kumbe Tanzania ni bora mwanafunzi anaweza pata posho hiyo kuliko vyuo vya nchi tajiri. Watu hatukulala usingizi ni darasa na kazi. Uwapo kazini wakati wa mapumziko ndo unafanya homework, hakuna kulaza damu.
Tusiwe watu wa kulaumu serikali katika kila kitu, tulaumu yale ya msingi lakini katika hili mimi binafsi nasema hapana.
Watanzania tuko wavivu mno wa kujituma na kufikiri. Mazingira yako huru mno kujishughulisha Tanzania kuliko mataifa yaliyoendelea.
Utakuta walimu wanakimbilia kufundisha shule za mijini, kumbe shule za vijijini zina nafasi zaidi kwa kujiongezea pato kwa kujishughulisha na kilimo au kufungua biashara ndogo ndogo kusaidia wanavijiji kupata bidhaa ambazo wanapata taabu kuzifuata mbali. Mshahara wake ungezalisha zaidi kuliko mijini anamalizia kwenye starehe na gharama kubwa ya maisha.
Athari wanazopata wanachuo katika migomo yao ni kubwa kwao wanafunzi kuliko viongozi wanaowanyooshea vidole wakati wanaishi maisha ya starehe, na waendapo vyuoni ni kwenda kuwapiga msasa wa kisiasa tu. Kinachofanyika sasa vyuoni ni kama cheer ambayo ni kufuata mkumbo tu na kulazimisha wasiotaka lazima wafanye vinginevyo watadhurika, huku ni kuwanyima wengine uhuru wao wa kujiamulia wanavyotaka. Haki ya uhuru ni uamuzi wa dhamira safi baada ya upembuzi yakinifu.
Serikali ina mengi ya kufanya si wanafunzi tu, elimu, mawasiliano, afya, na huduma nyingine za jamii. Hata Chama kingine kikitawala hakitamaliza matatizo hayo kwa siku moja.
mchanganuo wako ni mzuri lakini uko more theoretical.
Mfano tuchukulie matumizi ya mwanafunzi ya kila siku.
1.chai na chapati 2=600/-
2.sahani ya wali na nyama=2000/-(mchana)
3.chipsi mayai=1500/-(jioni)
4.maji madogo 2,soda 1=1500/-
5.fedha ya chumba kwa siku=500/-
Jumla =6100/-
hapa unaona ile fedha wanayopata kwa ajili ya meal na accomodation(5000/-) haitoshelezi hata ujaribu kujibana kiasi gani,yaani usinywe bia wala humberger.
Si hivyo tu,ukweli uliopo mtoto wa mkulima kutoka tandahimba anapochaguliwa kuja chuo anatarajiwa kuchangia ada ya mdogo wake pale kijijini.kuna gharama nyingine za msingi ambazo mwanafunzi anakabiliana nazo mfano nauli ya kwenda chuoni kwa wale wanaoishi nje ya campus,stationaries kwani hela wanayopewa kwa mwaka ina uwezo wa kununua kitabu cha course ya semester 1 tu,radio hata ya mkulima tu,simu na vocha kwa mawasiliano,surawili na tai ili uonekane mwanachuo kweli.
Tanzania haijaweka mazingira ya wanafunzi kufanya part time job.hakuna viwanda vinavyofanya kazi usiku,lakini pia mwanafunzi wa chuo(form vi leaver) hana ujuzi wowote wa yeye kuweza kufanya kazi.kuna mradi kama mlimani city ungeweza kuajiri wanafunzi but sidhani kama unafanya hivyo.
Sidhani kama unafurahia kuona watoto wetu wa kike wanachuo wakijiuza pale posta.
Kwa ufupi madai ya wanafunzi yana msingi na yanahitaji kuangaliwa kwa umakini bila ushabiki wa kisiasa.
Mapendekezo:badala ya kutoa fedha ya meal&accomodation serikali kupitia board ya mikopo ikopeshe fedha ya KuJIKIMU ambayo itajaribu kuadress mahitaji muhimu ya mwanachuo.lakini hii isiwe kwa wanafunzi wooote isipokuwa wale wachache waliofaulu vizuri(div one na two).hii itaondoa migomo ya mara kwa mara.