Ndege zina iwezo wa kujirudisha nyuma kama ulivyoelezea, lakini watengeneza ndege hawashauri matumizi ya reverse thrusts kurudishia ndege nyuma kwa sababu ni hatari kwa usalama wa injini hasa hizi kubwa za jet zilizofungwa chini ya mabawa. Ni kawaida sana kwenye turbo props hasa ATRs kuona wakitumia kirudishia ndege nyuma na boeing C17 za kijeshi ambazo injini zake ziko juu kuliko kawaida.JE, NDEGE INARUDI NYUMA?
Ndege nyingi za sasa zina mfumo wa kurudi nyuma #reverse' ambao mara nyingi hutumika kupunguza kasi wakati ikitua (#Braking).
Kwa baadhi ya ndege za 'Mapangaboi' #Propeller hutumia panga zake kubadili umbile (#angle) hivyo badala ya kuvuta hewa kwenda nyuma inasukuma kuelekea mbele na kusababisha ndege kupunguza kasi yake pale inapotua.
Hali kadhalika na kwenye injini zenye mfumo wa #Jet huwa zinafungua injini katikati na kubadili uelekeo wa hewa inayosukumwa nyuma kuvuja na kulazimishwa kuelekea mbele.
Baadhi ya Injini za mfumo wa 'jet nyingine zinafungua vimilango vyake vidogo katikati au nyuma ya injini.
Ndege nyingi kubwa zina mifumo mitatu ya kupunguza mwendo #braking ikiwemo
1>#Reverse' ya Injini au #Reverse_Thrust
2>'Brake' za matairi na
3> #Ground_Spoilers au #Speedbrake' ambazo ni bapa zinazo nyanyuka juu ya mbawa.
Hivi vyote mara nyingi hufanya kazi kwa pamoja ili kupunguza kasi ya ndege inapotua ili kusimama haraka kwakuwa hutua na kasi kubwa sana.
Kasi ya kutua ndege kama #MD11 ikiwa imejaa mzigo hata Gari yako yenye speed 260km/h haifukuzi.
Brake zote za kukinzana na upepo {spoilers na reverse thrust} husaidia kutozipa mzigo mkubwa 'brake' za matairi ambazo huweza kupasua tairi, kuharibika, kuwaka moto au mda mwingine kuteleza kama barabara #Runway ikiwa imetuama maji endapo kama zitatumika pekee bila msaada wa #brake' nyengine.
Licha ya kukinzana na upepo juu ya mbawa, 'spoilers/speedbrake' pia husaidia kukandamiza ndege chini hivyo tairi kushika barabara vizuri wakati zinakamata 'brake kupunguza mwendo.
Sasa kwanini ndege haitumii 'Reverse' kujitoa kwenye Maegesho?
badala yake inasukumwa kurudi nyuma (#Pushback) na vigari maalumu #Tow_Truck/#Tug
1>Kuepuka kelele kali za 'reverse'
2>Kuepuka ulaji mafuta
3>Kuepuka hatari ya ndege kugongana na vitu vingine nyuma.
4>Kuepuka uharibifu wa injini kwa kunyonya taka na vumbi kwasababu upepo wa 'reverse' hutokea pembeni ya injini kwa kasi kubwa kuelekea mbele ya injini.
5> Reverse ni mfumo wa dharura ambao kiufundi haishauriwi kutumika hovyo kwasababu hewa yake inapitia sehemu za injini ambazo ni rahisi kupata uharibifu.
#Admin
Credit
#boldmethodView attachment 2620053
Ni cash? Au ni utaratibu wa kawaida?View attachment 2896459B737-9 MAX ya pili, 5H-TCQ inaweza kuwasili wakati wowote ndani ya mwezi huu.[emoji115][emoji115][emoji115]
Tutajua tu, Lakini imechelewa kutoka.
Hii habari haiko sawasawa na uhalisia. 5H-TCG ndiyo iliyorudi, na ilikaa kule kuanzia October 8 hadi November 22. 5H-TCJ uliyosema imerudi iliharibika August 12 Guanzhou China na ikasafirishwa kwenda matengenezo ya Malaysia November 9. Ipo huko hadi sasa.. AirTanzania ndege mbili (2) za masafa marefu, Boeing 787-7 (Dreamliner) zilikwenda (kwa mujibu wa ATCL) katika Matengenezo ya kawaida (maintenance schedule) Malaysia tangu September 2023,
Ndege hizo zina usajili wa 5H-TCG (Mt. Kilimanjaro) na 5H-TCJ (Rubondo Island). Tangu wakati huo, ni ndege moja (5H-TCJ) imerudi kutoka katika matengenezo ya kawaida (maintenance schedule).
AirTanzania, kwa kuwa ndege hizi zilinunuliwa kwa fedha zetu, tunahitaji kufahamu, ndege yetu Boeing 787-7 5H-TCG (Mt. Kilimanjaro) ipo wapi tangu September 2023 ilipokwenda nchini Malaysia?
Lakini, tukitazama picha ya ndege ya Boeing 787-7 (Dreamliner) 5H-TCJ (Rubondo Island) ikiwa katika matengenezo Malaysia, inaonekana hadi madirisha yamefunikwa. Mmekwenda kuichapa rangi upya?
Boeing 787-8 Dreamliner bei ni $224.6M sawa na BILIONI MIA TANO na MILIONI MIA SITA na zaidi.. (TZS 562.5 bilioni). Lakini ndege inashinda muda mwingi katika matengenezo kuliko angani.
Kwa mujibu wa taarifa ya CAG kwa mwaka wa fedha wa 2020/2021, ndege hizi mbili zilihesabu hasara yenye thamani ya TZS 23.6 bilioni wakati ATCL ikipata hasara ya jumla ya TZS 36.5 bilioni.
Gharama za uendeshaji Boeing 787-7 (Dreamliner) zilizidi mapato na kusababisha hasara ya TZS 23.6 bilioni. Bombardier Dash-8 Q300 imekwama kwa zaidi ya miaka mitatu kutokana na matengenezo.
Bombardier Dash-8 Q300 yenye usajili wa 5H-MWF inabeba abiria 50. imetupwa nchini Malta kwa miaka 3 tangu mwaka 2020 ilipokwenda kwa ukarabati ambao unagharimu zaidi ya TZS 13.9 bilioni.
MMM, Martin Maranja Masese
Asante kwa ufafanuzi na masahihishoHii habari haiko sawasawa na uhalisia. 5H-TCG ndiyo iliyorudi, na ilikaa kule kuanzia October 8 hadi November 22. 5H-TCJ uliyosema imerudi iliharibika August 12 Guanzhou China na ikasafirishwa kwenda matengenezo ya Malaysia November 9. Ipo huko hadi sasa.