Macho kutokuona vizuri kwa muda ikifuatiwa na maumivu ya kichwa, nini tatizo?

BALIKUMI

Member
Mar 13, 2015
27
45
Doctor naomba msaada juu ya tatizo la macho kutokuona vizuri kwa mda kama wa dakika kumi halafu baada yahapo kichwa huanza kuuma sana. Kwangu mimi limenichanganya hivyo naomba msaada wenu madaktari.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,592
2,000
Presha ya macho, hii ni hatari sana inaweza kukuletea upofu wa ghafla. Nenda Ccbrt au New Vision Eye Clinic iliyopo kituo cha general tire kama waenda msasani.
Pole.
 

ivunya

JF-Expert Member
Sep 18, 2015
1,911
2,000
Aisee nenda hospital nzuri, nilikuwa na matatizo kama yako lakini Mimi yalisababishwa na mwanga mkali wakati wote nilipokuwa shule chumba chetu kilikuwa na matatizo ya bulb tukichelewa kuwasha ila taa haiwaki solution ni kuacha ile taa iwe on masaa yote week mpaka mwenzi nzima. wakati wa mchana nikiangalia mbele siona kitu mpka MTU anikaribie Jiran ndo namuona. nilopo enda hospital wakanipima wakanipa dawa ya vitamin B nitumia baada ya 2week nirudi tena. Baada ya kupona kwa kutumia zile dawa sikurudi tena hospital ndo tabia za mwafrica. wahi mapema kwa kuwa macho yana stage unapozidi kuchelewa utakuta mewani inakusubili.
 

tebweta

JF-Expert Member
Jun 12, 2016
206
250
Kama huna presha
Kisukari
au kuziba kwa misuri midogo midogo ya damu
basi hizo ni dalili za kuwa na mnyama mwilini (jini
Dalili jichunguze afya yako
1) ndoto zako
2) mwili wako hauna mabadiliko yeyote ?
3) ukiona kichwa kinauma ovyo ovyo bila mpangilio wowote nenda kwenye maombi au duaa
 

MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
40,602
2,000
Doctor naomba msaada juu ya tatizo la macho kutokuona vizuri kwa mda kama wa dakika kumi halafu baada yahapo kichwa huanza kuuma sana. Kwangu mimi limenichanganya hivyo naomba msaada wenu madaktari.
Fuata ushauri wa wenzangu na pia matatizo yako yanachangia upungufu wa Vitamin A mwilini mwako pendelea kunywa juisi ya karoti ambayo imechanganywa na nanasi usiiwekee maji Kunywa kila siku asubuhi kabla ya kula kitu kunywa juisi ya Karoti na nanasi glasi 1 na wakati wa jioni. Fanya zoezi hilo kwa siku 7 au zaidi ya hapo utakuja kuniambia.

juisi ya karoti.jpg
karoti kwa ajili ya macho.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom