Sasa kama hatuwezi kuyasafisha ndio shida yenyewe hiyo,halafu hivi hujasikia kuwa mito(eg Ruvu) umekauka?
Nadhani Tanzania kila kitu ni shida ,hatuna chenye nafuu hata kimoja.Ndio maana inabidi tuangalie priorities kianze kpi kutatuliwa.[/QUOTE]
Ni kweli mambo mengi ni shida, lakini shida nyingi ni za kujitakia. Kukosa mipango ni kujitakia shida. Maji ya Ruvu lazima yakauke kwa sababu watu wengi wanalima siku hizi huko Morogoro na Pwani ambako mto unakusanya maji. Hii inasababisha mababdiliko ya kiwango cha maji yanayoingia mtoni. pia ikumbukwe kuwa dunia nzima inaongelea kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Huwezi ukaepuka matatizo yanayosababishwa na emissions za Wachina au Wahindi. Cha kufanya ni sisi wenyewe kuwa na MIPANGO ya kuondoa utegemezi bila ya kuwa na njia zetu za kujinasua iwapo hali inabadilika.
Pia mitambo ya kutoka Ruvu ilijengwa kwa ajili ya population ya miaka zaidi ya 30 nyuma, na hakukuwa na kujali kuwa siku za usoni mahitaji jijini yataongezeka.
Tungekuwa na mipango hata tusingang'ang'ana na Ruvu, kukosa mipango ndo kunasababisha tulielie kila siku Ruvu inapokauka.