boyskillz
Senior Member
- Apr 29, 2013
- 109
- 104
Nimesikia kwenye vyombo vya habari kuwa mkuu wa mkoa wa Dar amezuia biashara ya Kuuza DVD zenye picha mnato (movies) zá nje ya nchi, mfano zile za kikorea, kihindi, kifilipino nk.
Nilichunguza lengo la yeye kufanya vile nikatambua kuwa anafikiri hio Ndiyo njia itakayosaidia waigizaji wa muvi za nyumbani maarufu kama bongo movie kuuza zao.
Ningependa kumshauri bure tu, kitendo hiki kamwe sio suluhisho la kumsaidia msanii wa nyumbani. Bali kinaweza kusababisha mtafaruku wa kiuchumi kwa wale watanzania waliokuwa wamekwisha kujiajiri katika biashara hii, mfano wale walioweka sauti ndani ya Hizo muvi kwa lengo la kutafsiri na pia kitendo hiki kitakua fimbo ya kiuchumi kwa wale wanaoziuza mitaani kwani ndio biashara inayowaweka mjini.
Jambo la kwanza nafikiri Mheshimiwa huyu angejiuliza kwanini watanzania wengi wanapendelea hizo muvi za nje, hapo angeweza kuona kwamba pengine muvi za nje zina ubora (HD), ama pengine zina stori tamu nk. Na kama hayo yakiwa Ndiyo majibu basi angeyapeleka kwao Bongo Movie kama changamoto ili kesho na wao waweze kupambana ili kufikia hatua hiyo ya kununulika zaidi sokoni.
Naweza toa mifano ya sinema kama za Merlin, 24legacy na Jumong, hizi ni lazima zizidi kimauzo sokoni ukilinganisha na zile za akina Hemed PHD, na hili halipingiki. Vile vile watazamaji wanatofautiana kwenye interest zao, unakuta huyu anapenda za Hollywood, yule Bollywood na huyo Bongo Movie. Sasa kwa mawazo ya kudhania kuzitoa Hizo zingine sokoni zibaki Bongo Movie Pekee ndio kuisaidia tasnia hii ni kujidanganya, mfano kuna rafiki yangu mmoja yeye ukimwambia muvi moja kwa moja mawazo yake Anajua ni ya kikorea akikuta sio anaachana nayo hapo hapo.
Kama mheshimiwa angetaka kuwasaidia hawa bongo movie basi angeangalia namna ya kuzilinda kazi zao zisiibiwe ama kunakiriwa na maharamia (piracy) wa muvi ili kuhakikisha wananufaika vilivyo na kazi zao. Na pia angetafuta hata njia ya kuwapunguzia kodi ili wasibanwe na adha za sokoni.
Lakini kwa hatua hii aliyochukua hapo naweza kusema amechemka, maana anakwenda kudidimiza uchumi wa yule machinga anayelisha familia yake kwa biashara hii. Na uchumi wa hawa wanyonge ukianguka hata pato la taifa litapungua kwa asilimia flani kwasababu hawa machinga mfano waliopo soko la mwenge ama kariakoo wanalipa ushuru wa meza ama kodi ya pango.
Kama kuna washauri wa washauri wake naomba wakafikishe ujumbe huu kwake na wakatafute njia nyingine ya kuwasaidia hawa wasanii maana hii haina msaada wowote ule na badala yake inaleta tatizo lingine mtaani.
Na Enock Ally Skills
---------
Heshima kwenu,
Mara baada ya uteuzi, Waziri wa Habari, Sanaa Utamaduni na Michezo wakati huo Mh. Nape Nnauye, alipanga kuwafurahisha Bongo Movies. Alipita Kariakoo na kukamata CD zilizoitwa feki, zisizokuwa na muhuri/stamp ya TRA. Ilikuwa sahihi.
Baadaye akatoa maagizo kuwa CD za nje hazitakiwi kuuzwa, ziuzwe za Bongo tu, lengo ni kusaidia wasanii wa ndani. Zoezi hill liliambatana na kukamata CD zote za nje.
Msambazaji mkuu wa CD hizo kutoka China, mwenye duka na stop anayeuza kutoka Hotel ya Butterfly, alisombewa mzigo wote, akafunga duka, hakurudishiwa kitu. Maofisa wa wizara ya Nape walikuja tena na kukamata CD kwenye duka hill na kuwaambia wauzaji waweke stamp za TRA wakawaambia haiwezekani kwa kuwa mzigo unatoka China moja kwa moja. Wakalazimishwa waingie mkataba na watengenezaji.
Leo hii kulikuwa na zogo Kariakoo na wauza CD walifunga maduka juu ya suala hilo hilo. Ijulikane kuwa so watu wote hupenda Bongo Muvie kwa kuwa hazina quality kama za nje. Kulazimisha watu wanunue kitu wasichokipenda kwenye karne hii ni makosa.
Serikali inavunja sheria kufanya hivi. Wananyima umma haki yao na wanawatia hasara watu waliowekeza kwenye biashara hiyo. Biashara ya CD sio ya viroba. Sababu nyingine zitolewazo na wizara hazina mashiko.
Tuchangie