Machinga SACCOS wamdhulumu dalali

Machinga SACCOS wamdhulumu dalali

hosen mmakonde

Senior Member
Joined
Oct 13, 2014
Posts
139
Reaction score
79
Wakuu Habari....
Naombeni msaada Wa kufikishiwa Ujumbe kwa mtu yoyote ambaye yupo karibu na uongoza Wa Gazeti la MACHINGA na MACHINGA Saccos

Machinga Saccos wamenidhulumu haki Yangu, tuliingia Makubaliano ya kuwatafutia ofsi ambayo ndio wanaitumia mpaka Sasa ipo mtaa Wa idrisa Magomeni.

Makubaliano yalikuwa Laki 6 lakini wao wakanipa Laki 2, Lakini kila nikifatilia ananizungusha na huu Sasa Ni mwezi Tano hataki kunilipa deni langu , simu hapokei Tena na akipokea ananipa vitisho kuwa Taasisi inamikono ya Viongozi wakubwa hivyo anaweza kunifanya kitu kibaya.

Najiuliza Kama kiongozi Wa MACHINGA Saccos na gazeti la MACHINGA umefikia hatua ya kunidhulumu na huku unaaminiwa kukaa na hela za wanachama itakuwaje Sasa, Zitakuwa Salama???

Lakini Mbaya zaidi unatumia platform ya Saccos na Gazeti lenu kutajwa na raisi ndio imekuwa Ngao kwenu.

kunitishia kunifunga na kunibambikia kesi kisa Machinga Saccos ni ya Watu wakubwa na nifunge Mdomo Wangu la sivyo atanishughulikia.

Stonyamaza mpaka haki Yangu niipate na kinachofata ntaanza kwenda kwa hao wakubwa zako na kupeleka malalamiko yenu na popote mtapokuwa ntawasili.
 
Sajili biashara yako, ingia mikataba ya kisheria
Ila jamaa Wana roho ya kikatili Sana
Just imagine Mtu Kama Mimi ambaye najikwamua kiuchumii kwa kuwapatia Wateja Wangu sehem Nzuri wao wananilipa kwa kunitapeli jasho langu
 
Itakuwa ngumu kupata haki yako kwa kuwa hakuna ushahidi , utapoteza pesa na muda na mwisho wa cku utaonekana umewadhalilisha , itabidi uwalipe na uwaombe msamaha kuwa makini sana hapo sema ulikosea mahali
 
Siwapendi madalali, ah , kazi gani ulipwe 600k.
Ni bahati mbaya tu lukuvi na JPM hawapo vyenginevyo? Mlikuwa mnaenda sawa tu.
 
Siwapendi madalali, ah , kazi gani ulipwe 600k.
Ni bahati mbaya tu lukuvi na JPM hawapo vyenginevyo? Mlikuwa mnaenda sawa tu.
Kama hutupendi usiwe unatushobokea ukihitaji Nyumba utafute mwenyewe
 
Ila hii taasisi itakuja kuyumba sana siku za mbeleni imekuwa ni kama tawi la CCM viongozi wake wengi ni wanasiasa na sio machinga halisi. Wanatumika kama mtaji wa kisisasa kama alivyofanya Simba wa Yuda wa bodaboda na machinga.
 
naona kabisa no future kwenye hi taasisi, kwanza wamejaa matapeli yani kama unaweza kumtapele dalali ambaye amekutafutia eneo la ofsi tena ambalo lina kuingizia kipato kwa miaka yote leo umuone ana maana kwa kweli wanakosea sana
 
Wakuu Habari....
Naombeni msaada Wa kufikishiwa Ujumbe kwa mtu yoyote ambaye yupo karibu na uongoza Wa Gazeti la MACHINGA na MACHINGA Saccos

Machinga Saccos wamenidhulumu haki Yangu, tuliingia Makubaliano ya kuwatafutia ofsi ambayo ndio wanaitumia mpaka Sasa ipo mtaa Wa idrisa Magomeni.

Makubaliano yalikuwa Laki 6 lakini wao wakanipa Laki 2, Lakini kila nikifatilia ananizungusha na huu Sasa Ni mwezi Tano hataki kunilipa deni langu , simu hapokei Tena na akipokea ananipa vitisho kuwa Taasisi inamikono ya Viongozi wakubwa hivyo anaweza kunifanya kitu kibaya.

Najiuliza Kama kiongozi Wa MACHINGA Saccos na gazeti la MACHINGA umefikia hatua ya kunidhulumu na huku unaaminiwa kukaa na hela za wanachama itakuwaje Sasa, Zitakuwa Salama???

Lakini Mbaya zaidi unatumia platform ya Saccos na Gazeti lenu kutajwa na raisi ndio imekuwa Ngao kwenu.

kunitishia kunifunga na kunibambikia kesi kisa Machinga Saccos ni ya Watu wakubwa na nifunge Mdomo Wangu la sivyo atanishughulikia...
Stonyamaza mpaka haki Yangu niipate na kinachofata ntaanza kwenda kwa hao wakubwa zako na kupeleka malalamiko yenu na popote mtapokuwa ntawasili...
Hicho ni kilinge cha ulaji kwa idhini ya 'wakubwa' tatizo wamekabidhiwa washamba kukisimamia..USIKUBALI KUPOKWA HAKI YAKO..Pambana mpaka walkulipe
 
Una TIN namba y mlipa kodi? Tuanzie hapo kwanza
 
Potezea.
Unaweza ukafanywa kitu ambacho ukishafanyiwa ni Siri yako Ila watakao kufanyia watatangaza na kusambaza picha za tukio.
Yote hayo juu ya laki nne hela ambayo haitoshi hata kuhonga?
 
Back
Top Bottom