leonaldo
JF-Expert Member
- Oct 26, 2014
- 2,583
- 3,181
Akiongea kwenye kipindi cha jambo leo TBC1 leo kwenye mahojiano maalum yaliyo kuwa yakiendeshwa na mtangazaji Shaban Kisu, aliyekuwa mbunge kupitia NCCR Mageuzi Mhe Machali Sanjari na Dr Yaredi Yakusa wamesema:
- Wameshangazwa na watu ambao kwa muda mrefu wamepambana kuhakikisha wizi uliokuwa unaendelea unakomeshwa, lakini sasa wamegeuka na wanataka ACACIA waachwe kwa madai ya kuogopa kushitakiwa.
- Wamshaangaa Mh Tundu Lisu kwa U turn ya aina yake aliyoionyesha baada ya hatua kuanza kuchukuliwa.Amtilia mashaka huenda amehongwa ili anyamaze kwani makampuni haya ni mabingwa kwa rushwa.
- Adai kuipiti mikataba ya MIGA na kugundua kuwa hakuna mahari ambapo mikakataba hiyo inampa mwanya na kumlinda muwekezaji anapokuwa mwizi ama mdanganyifu.
- Adai kuwa kwa sasa wanasheria na watetezi wa udanganyifu huu wako kwenye hatua ya ujinga na wanaelekea kwenye hatua ya upumbavu.
- Awaasa watanzania kusimama pamoja kutetea Mali zao na kuachana na hofu wanayo pandikiziwa.
- Asema ni heri kupambana Leo na kuihami Mali yetu inayopotea kwa gharama yoyoye na sio kuiacha iendelee kuondoka kwa kisingizio cha kuogopa kushitakiwa.