Machafuko yanoyohusisha dini yananiskitisha ila ushiriki wa jf unaniskitisha zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Machafuko yanoyohusisha dini yananiskitisha ila ushiriki wa jf unaniskitisha zaidi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tafakuru, May 29, 2012.

 1. T

  Tafakuru Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Dec 9, 2011
  Messages: 84
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  Hello wanajamii

  Nmefungua habari mchanganyiko hapa JF, kunirahisishia upatikanaji wa habari za leo kwa ujumla wake. Nnastaajabishwa kukuta nusu ya thread zinavichwa vya habari vyenye kupoa kidogo na habari kamili kuwa ni ya kichonganishi, kichokozi na za kuchochea ghasia na wachangiaji wake kutoa maneno ya kibaguzi, kashfa, kutoheshimiana na uchokozi. Kwa mfano ebu fuatilia mazungumzo na habari nzima za wana JF katika habari zifuatazo kwenye kurasa hizi sehemu ya habari mchanganyiko

  Je unamfahamu siri nzito ya sheikhe alhaj rashid abubakar,
  Hivi kuna shetani wa kike?
  Vitabu vya Makamba sr. hawa ni wageni waalkwa uwiano umekaaje? Toa Maoni,
  Mkombozi Bank;Ni sahihi kutumia Mpemba ktk tangazo la biashara ?
  Habari zote hizi zimejaa kutupiana maneno ya kashfa na kujenga chuki tena ya kimtizamo wa kidini.

  JF nnawafamu vizuri sana kiofisi na kinnje ya ofisi, mnauongozi mzuri na moderators active kabisa. Ivi ni kuna uwezekano kwamba habari hizi nyinyi zinawabariki???? Ivi kuna uwezekano habari hizi hamjaziona???? Ivi kuna uwezekano huu ndo utakua msingi mzuri wa kupata followers wengi kurahahisisha biashara zenu??? Ivi ni kunauwezekano hapakua kuna thread zingine ambazo zingeleta manufaaa zaidi kwa umma??? Ivi kuna uwezekano, once mmepost thread hamzifatilii tena kuangalia yanayojiri????? Ivi kuna uwezekano thread ikishaanza kuchangiwa hamuezi kuitoa iwapo haina mwelekeo chanya???Ivi kuna uwezekano hamkubashiri yanayoweza kuletwa na thread hizi. Hakika majibu karibu yote hapo ni HAPANA
  Nnakila sababu ya kuwaunganisha JF na kuligawa hili taifa kwa misingi ya manufaa binafsi. Ni ukweli usiopingika, maoni yote yanayoonekana hapo ni hali halisi ya vichwa vya watanzania tulionao. Hii haimaanishi JF nanyi kuwa catalyst ( kichocheo)/ uwanja halali wa ujangili huu

  Nnashauri, tufanye mambo kwa misingi ya umoja na upendo na sivinginevyo. Usalama wa taifa unatutegemea sana sisi wenyewe tunavojiendesha. Kuna uwezekano sisi ni waoga sana wa machafuko na kupigana hali inayoweza kuleta dhana hakuna lolote linaloweza kutokea, ila, tusisahau Tanzania sio hot pot kwamba tunajifungia kwenye temperature yetu wenyewe. Kuna ushahidi wa kila aina kuonesha mipaka yetu ilivowazi kuliko hata sisi tulivoifungua ovyo ovyo; nnataka kusema kuna watu wanaonufaika na mikanganyiko ya kidini inayoanza kujitokeza. Yaweza kuwa, wanasiasa, magaidi, wafanyabiashara, mataifa ya nje, kikundi cha watu wachache apa nchini na makundi mengine mengi tu ya watu. Tushirikiane kuitokomeza hali ya kichonganishi sisi kwanza.
  Usalama wa taifa, ningependa kuwaona mnafanya kazi zaidi

  Mungu ibariki Tanzania na watu wake

   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Hawa Usalama wa Taifa inabidi wakaanze na WEzi wa EPA na wabadhirifu wa mali za Umma, kisha waende ZNZ kutuliza ghasia na kuwa kamata waliochoma moto Makanisa na kuharibu mali.

  Kisha itakuwa sahihi kwa kuingilia mijadala iliyopo hapa  MIZAMBWA
  NABII MTARAJIWA!!!
   
Loading...