Machafuko ya Haiti: Bunduki kutoka Marekani Zafurika Port-au-Prince

Umkonto

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
2,102
3,615
Kuna nchi zina shida humu duniani jamani, mfano Hait.

1. Kwa jinsi intelijensia ilivyo kali ya US, je, kwa nini washindwe kudhibiti usafirishaji wa silaha kutoka US kwenda kuchafua hali ya hewa huko Hait?

2. Kwa nini Wahait wameng'ang'ania kuanzisha magenge ya kihalifu badala ya kujikita kujenga nchi yao ingawa haina rasilimali kwa sasa? Je, wameishavurugwa akili au wamekata tamaa ya kuishi humu duniani?

NB: Hii nchi ilipata uhuru mwaka 1804 ila mpaka leo mambo yao ni hovyo. Kipindi cha ukoloni wa Ufaransa Hait ilikuwa tajiri kupitia kilimo cha sukari, ila kwa sasa nchi ipo hoi, ardhi imechoka zaidi ya asilimia 50 haifai tena kwa kilimo na haina rasilimali za asili kama sisi Tanzania. Kama vipi Wahait warudi Afrika.

Habari Kamili;

Zaidi ya wiki mbili baada ya waziri mkuu wa Haiti kujiuzulu, kufuatia kuongezeka kwa ghasia huko Port-au-Prince, maelezo ya baraza la mpito la rais bado hayajafichuliwa.

Mojawapo ya changamoto ambazo baraza hili litalazimika kukabiliana nazo ni biashara haramu ya bunduki, ambayo imeyapa nguvu magenge ambayo yameteka mji mkuu.

Mwanaume mmoja aliyevalia fulana nyeusi na miwani ya jua anaongea kwa utulivu huku tukimuuliza hali yake. Lakini anaonekana kuwa na hasira anapotuambia ana ujumbe kwa Marekani.

"Bunduki zote hapa zinatoka Marekani, kila mtu anajua. Ikiwa Marekani inataka kukomesha hili, wanaweza kuifanya kwa urahisi!" Anasihi: "Tunaiomba Marekani itupe nafasi ya kuishi, itupe nafasi tu."

Kwa nchi ambayo haitengenezi silaha, ripoti ya Umoja wa Mataifa mnamo Januari iligundua kuwa kila aina ya bunduki ilikuwa ikifurika Port-au-Prince: bunduki zenye nguvu nyingi kama vile AK-47.

Hakuna idadi kamili kuwa ni silaha ngapi zinazouzwa Haiti kwa sasa. Ripoti ya Umoja wa Mataifa ilisema baadhi ya makadirio yanaiweka kuwa nusu milioni ya silaha halali na haramu kufikia 2020.

Iliripoti kuwa bunduki na risasi zilikuwa zikiingizwa kinyemela kutoka nchi kavu, angani na baharini kutoka majimbo ya Marekani kama vile Florida, Texas na Georgia.

Kumekuwa na visa vya kukamatwa silaha katika bandari kuu za nchi huko Port-au-Prince, Port-de-Paix na Cap-Haitien. Silaha haramu zimefichwa kwenye vyombo vya usafirishaji kati ya vinyago na nguo.

Mnamo Julai 2022, mamlaka ya Haiti ilikamata silaha nyingi na risasi 15,000. Zilikutwa kwenye shehena kutoka Florida kuelekea kanisa la Episcopal huko Haiti.

Umoja wa Mataifa pia ulibainisha matumizi ya viwanja kadhaa vya ndege vya siri vilivyojengwa kwa madhumuni ya kibinadamu baada ya tetemeko la ardhi lililoharibu mwaka 2010, ambavyo sasa havifuatiliwi.

Mapema mwezi huu, msemaji wa Umoja wa Mataifa, Stephane Dujarric, aliwaambia waandishi wa habari kuwa ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kwa magenge nchini Haiti ni "kunyamazisha bunduki".

Chanzo: BBC Swahili
 
Back
Top Bottom