Mabosi huko maofisini mkila msitusahau na sisi

Mabosi huko maofisini mkila msitusahau na sisi

Binti Magufuli

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2011
Posts
7,479
Reaction score
5,161
Mabosi shikamooni,

Mnakuwa kwenye mashirika makubwa tu, marupurupu yapo ya kutosha ila mnakula peke yenu....kwa nini mkila na vipofu mnawashika mikono?

Wataabikaji na wafanyaji kazi wa kweli ni sisi, ripoti zenu zinategemea sana sisi tulichokifanya yaani kwa maana nyingine wavuja jasho ni sisi.

Kwakweli kazi isiyo na marupurupu haina mzuka kabisa.

Mabosi ninajua mnapita hapa basi msile peke yenu. Jitahidini kuboresha na mazingira yetu ili na sisi tujione watu na sio watumwa.

Asanteni
 
Hicho wanachokula Maboss wako wanaiba? Hicho ndio unataka na wewe ugawiwe?

Hicho wanachokula maboss zako ni haki yao? Kinakuwasha nini kama wanakula stahiki zao.

Tunaomba kujua huo ulaji wa boss ambao unakuwasha kihvyo
 
Mabosi shikamooni,

Mnakuwa kwenye mashirika makubwa tu, marupurupu yapo ya kutosha ila mnakula peke yenu....kwa nini mkila na vipofu mnawashika mikono?

Wataabikaji na wafanyaji kazi wa kweli ni sisi, ripoti zenu zinategemea sana sisi tulichokifanya yaani kwa maana nyingine wavuja jasho ni sisi.

Kwakweli kazi isiyo na marupurupu haina mzuka kabisa.

Mabosi ninajua mnapita hapa basi msile peke yenu. Jitahidini kuboresha na mazingira yetu ili na sisi tujione watu na sio watumwa.

Asanteni
Tatizo wa chini na vidomo domo sana mkipewa laki moja mnahisi tumekula parefu bora tuwanyime tu ndo tulichoamua
 
Sipendii kitu inaitwaa " Bosi"[emoji57][emoji57]
 
Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake, ukiona huvipati hivyo vinono ongeza urefu wa kamba yako
 
Hamna aliyezaliwa kua boss....komaa nawe utakuja toboa
 
marahaba binti,

kama wewe unakubali 'kuliwa' kwani usipokubali kuliwa japo kidogo na wewe huli kabisaa( in mkwere voice) wee njooo tuu, sisi ma-'boss' hatunaga noma kabisa na mabinti, tutakula kidogo tuu
 
Back
Top Bottom