Hivi miaka 30 iliyopita maeneo kama Ubungo na Mwenge au hata Sinza ya leo palikuwaje?Tanesco ndio wanapaswa kuweka mitambo yao pembeni ya mji sio mjini
Tanesco ndio wanapaswa kuweka mitambo yao pembeni ya mji sio mjini
Napongeza jiji na jeshi la polisi.
Sheria za nchi ni lazima zilindwe kwa gharama yoyote.
Wawaondoe kwani wamekuwa vitunguu!!!Wawaondoe tu na wawapeleke MACHINGA COMPLEX haina watu
na vile wana hasira za arumeru basi vijana wote ni adui
Napongeza jiji na jeshi la polisi.
Sheria za nchi ni lazima zilindwe kwa gharama yoyote.
Wanabodi,
Asubuhi hii FFU wamewatawanya wamachinga katika maeneo ya Ubungo mataa, Ubungo maji, stendi ya mkoa na wale wanaofanya biashara katika maeneo ya gridi ya taifa.
Mojawapo ya maeneo ambayo yameathirika ambayo nimeyashuhudia ni ile baa ya Standard ambayo ipo karibu na stendi ya mkoa. Baa hiyo imevunjwa katika eneo lake la mbele ikiwa ni hatua za utekelezwaji wa oparesheni hiyo.
Kuna magari ya FFU na askari kanzu yasiyopungua 30 ambayo yametanda maeneo hayo ya Ubungo. Pamoja nayo yapo mawashawasha mawili ambayo yanasubiri kufanya kazi pale itakapohitajika.
Kwa ujumla hali bado ni shwari na machinga wengi wameingia mitini kwa sasa japo kuna kajikundi kadogo ambacho bado kanajibizana na askari pale maeneo ya mataa. Kajikundi hako kana mabango mawili ambayo yanasomeka:
"Haya ndiyo maisha bora kwa kila mtanzania?"
"Nyie mnasaini posho mnakula, siye tunakufa na njaa".
Oparesheni hii inafuatia matangazo yaliyokuwa yanatolewa na Tanesco, Tanroads na Manispaa ya Kinondoni ya kuwaondoa watu wanaofanya shughuli katika maeneo ya gridi ya taifa, chini ya njia za umeme na katika hifadhi ya barabara.
Kwa mujibu wa Tanesco, Tanroads na Manispaa ya Kinondoni ilitakiwa wafanyabiashara hao wawe wameondoka katika maeneo hayo kufikia tarehe 01.04.2012 la sivyo wangeondolewa kwa nguvu.
NB:
Kwa wale akina Tomaso: Sikuweza kupata picha kwa sababu kamchina kangu hakana uwezo wa kuchukua picha.
unapofikiria kuwaandalia maeneo utambue nature ya biashara ya kimachinga, usije kuishia kujenga machinga complex kwa mamia ya mamilioni halafu likawa makazi mazuri ya popo.
na vile wana hasira za arumeru basi vijana wote ni adui
Polisi wa Tanzania katika kazi wanazopenda kuzifanya, na huzifanya kwa ufanisi mkubwa sana ni hii ya kuwapiga wamachinga.
Utashangaa wamejaza mabomu ya machozi, risasi za moto na magari ya washawasha kama vile wanakwenda vitani. Pamoja na hasira za kugaragazwa Arumeru, serikali ina hasira za wanaubungo kuikataa ccm na wanatambua kwamba vijana wanazidi kuikataa.
Well, ni wazo zuri kuwaondoa katika hayo maeneo hatarishi lakini wamewaandalia maeneo ya kuwahamishia? kwani magufuli na tanesco hawajui kwamba hao watu wako hapo ili kujitafutia rizki zao!? kwanini wasiwaandalie mahali muafaka pa kufanyia biashara kabla ya kutumia maguvu kuwahamisha?
Kwa kweli hili eneo limegeuka kwua hatari sana. Inashangaza kwua mamlaka zimechukua muda mrefu sana kuwaondoa watu pale. KIla ninapopita, hasa nyakati za jioni siachi kusali kuwa lolote baya lisitokee, maana likitokea, maafa yatakayopatikana hayatasimulika kirahisiNaamini ilikuwa muhimu zaidi kuiondoa pale grid ya taifa ya umeme, simbion na power plant ya gas ya songas. yale maeneo ni ya makazi na yana watu wengi sana. tuangalie mbali siyo chini ya transforma tu.