Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Jeshi la polisi mkoani Morogoro limelazimika kutumia mabomu ya machozi na mbwa kuwatawanya wananchi wa kata ya Kiwanja cha ndege waliofika katika kituo cha kutangazia matokeo ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata hiyo.
Hali hiyo imeibuka mara baada ya mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CHADEMA Salum Milindi kufika katika kata hiyo akiwa amenyanyua mikono juu na kutaka kuingia ndani ya chumba cha matokeo kwa mujibu wa sheria huku akizuiliwa na jeshi la polisi.
Mgombea wa udiwani kwa tiketi ya CCM Isiaka Sengo aliibuka kidedea kwa kupita mpinzani wake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Salum Milindi kwa kura 192 ambapo msimamizi msaidizi wa uchaguzi Shabani Duru amemtangaza Isiaka Sengo kuwa diwani wa kata hiyo.
Awali wakizungumza na ITV wasimamizi katika vituo wameeleza changamoto zilizo kuwepo ikiwa nipamoja na wananchi kutojitokeza kwa wingi.