VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,007
Nilikuwa kimya kwa muda kidogo kujadili siasa ili nipate nafasi ya kutafakari juu ya 'mabomu ya CHADEMA'. Lakini,nakosa cha kujadilisana.Vitu viko wazi sana. Ni hivi,ulipotokea mlipuko wa bomu kwenye mkutano wa kufunga Kampeni za Udiwani za CHADEMA,viongozi waandamizi wa CCM walisema kuwa CHADEMA imejilipua yenyewe Arusha ili kujipatia umaarufu.
Eti,CCM iliibana mbavu CHADEMA kule Arusha katika kampeni na hivyo,ili kuvuruga uchaguzi huo,CHADEMA waliamua kujilipua. Bado nakumbuka kauli ya Mwigulu Nchemba,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara kuwa CHADEMA walijilipua wenyewe Arusha! Kauli hiyo aliitoa Bungeni Dodoma. Mwigulu Nchemba alipaa haraka toka Arusha hadi Dodoma kuwahi kutoa kauli hiyo Bungeni.
Kwa wafuatiliaji wa siasa za Arusha na ambao tulikuwepo angalau siku chache Arusha wakati wa kampeni hizo,tulimuona Mwigulu Nchemba'MUONGO'. Na matokeo ya kata nne Arusha yakatulindia uchambuzi wetu. Tukabakisalama. Mwishoni mwa juma lililopita,bomu lingine lililipuka katika mkutano mwingine wa CHADEMA katika eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam. Ikasemwa kuwa lililipuka mikononi mwa Polisi.
Polisi 'wakajitetea' kuwa walikuwa nalo wakati wakilinda amani eneo la mkutano. Kulikuwa na haja ya mabomu sehemu ya kulinda amani? Nani ataamini kauli ya Polisi wetu kirahisi wakati kuna kumbukumbu ya Arusha? Kama watanzania,tukamezea.Lakini tumeweka kwenye kumbukumbu zetu. Mabomu haya si yakupuuzia. Tujiulize,nani anafanya mambo haya kwa chama hiki-CHADEMA? Lengo ni nini hasa? Na tujijibu akilini mwetu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam