Mabingwa watetezi leo: Simba Vs Toto African

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
Mabingwa watetezi
Simba, leo wanashuka
kwenye Uwanja wa
CCM Kirumba, Mwanza
kuivaa Toto African (ndugu wa damu na timu ya Yanga) katika mechi ya Ligi kuu ambayo
inatarajiwa kuwa na
ushindani mkubwa
kwani Simba inashuka uwanjani baada ya kufungwa bao 1-0 na Kagera Sugar katika mchezo uliopita na kubaki nafasi ya tatu, ikiwa na pointi 34.
Simba watakuwa
wakipigania ushindi ili kuongeza hali ya utulivu
ndani ya klabu yao, ambayo inaonyesha kuchechemea katika Ligi kuu ya Tanzania Bara.

TIMU SUPPORTERS:
- Gamaha
- christmas
- brave one
- mimi
- ndetichia
- Masuke
- PrN-kazi
- kelao
- Cynic
- KYALOSANGI
- Crashwise
- Omonto
- rmashauri
- bemg
- Mkolokotiatanas
- jambia
- Busurwa
- kmbwembwe

Na wadau wote wa Msimbazi

============================
Mwananchi: Simba kuzuiwa hotelini mjini Bukoba:
Wachezaji wa timu ya Simba kwa mara nyingine walizuiwa kutoka hotelini kutokana na uongozi kushindwa kulipa Sh6.5 milioni za gharama za hoteli ya Smart mjini Bukoba.
Gharama kubwa za hoteli hiyo zinatokana na baadhi ya viongozi kubeba wanachama wao katika safari yao ya Kanda ya Ziwa ili kuwalinda wasiondolewe madarakani. “Timu ilikuwa iondoke saa 10 alfajiri kwa basi kwenda Mwanza, lakini mpaka saa sita ndiyo iliruhusiwa kuondoka baada ya kulipa deni hilo, yaani ni aibu tupu!

CHANZO: Mwananchi
 
na leo pia azam fc tupo uwanja wa mabatini hii gemu itakuwa laiv kupitia starTV so stay tuned..
 
Mabingwa watetezi a.k.a "wazee wa chekechea" leo wanaongezewa maumivu Kirumba. Pamoja na methali nyingi za busara kama "sumu haijaribiwi kwa kuonja" na "kima cha maji hakijaribiwi kwa kuingiza miguu" wao wanajifanya kichwa ngumu kuwajaribu chekechea wengi kwa mkupuo. Time will tell.
 

nitake ladhi mkuu #teamAzamfc hapa..
 
nimeikuta somewhere mtandaoni...
 
Go Simba go, usione Simba kalowa ukafikiri ni nyau. Simba team funga Toto 3-0 ili washuke daraja kabisa Yanga B hao, yani ni kama kile chama kinachoitwa CCM C
 
nitake ladhi mkuu #teamAzamfc hapa..

Akutake radhi nini, kwamba weye siye mmoja wa girls was LIBOLO? Huyu aliyeku-expose ni Simba, anatakusingiziaje huku akijua fika wewe ni mmoja wao walioliwa na LIBOLO? Come on, cut the bull!

You can fool some people some time.....malizia mwenyewe.
 
Ndio napata ugali wangu na kitimoto hapa nyegezi ili niwahi game kirumba mnyuama akiuliwa
 
Ndio napata ugali wangu na kitimoto hapa nyegezi ili niwahi game kirumba mnyuama akiuliwa

Mkuu mie nagonga ugali na mbuzi choma hapa Msamvu baada ya hapo naelekea Jamhuri Stadium kushuhudia Yanga ikiishusha daraja Polisi Morogoro, kesho nakuja huko Zoo kusherehekea ushindi wa Toto na Yanga.
 
Wakuu hii mechi inaanza saa ngapi, yanga karibuni sana na habari za LIBOLO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…