Mabere Marando awania Uspika kupitia CHADEMA

imetulia tukiwa na spika toka upinzani.. ndio demokrasia hiyo..
 

marando hafai kabisa kuwa spika ni mtu wa majungu na ndie aliechangia kwa kiasi kikubwa kusambaratika kwa upinzani miaka ile ya 90 wakati alipokuwa na mgogoro wa kugombea madaraka yeye na lyatonga mrema!
Pili ni msaliti mkubwa kwa upinzani wakati wapinzani walikuwa na chaguo lao la mbunge wa afrika mashariki cha kushangaza huyu marando alipigiwa debe na ccm na kuibuka mshindi!!!

Sasa kama yeye ni miganaji mbona alisambaratisha nccr na baadae kukimbilia chadema tena karibia na uchaguzi?
Kama alikuwa na hamu yauspika kwanini hakugombea ubunge ktk jimbo la uchaguzi ili apate ridhaa ya wananchi na ndipo aje kugombea uspika lakini anangojea kapu maalum!!!
 

Jamani Uspika sio lazima uwe MBUNGE ni Mtanzania yoyote umri 18
Pia Marando mmedai ni UWT mm bado namfagilia ana msimamo na Nchi yake ila Superman NA WENGINE nawaelewesha chaguo la Chama chochote huwa ni mtu mmoja kabla ya kuingia Mjengoni CCM wamehaanza kuingia ----- wanakutana na kumchagua mmoja (Sita Samweli) atashinda tu na hata Mjengoni atashinda na wapinzani watampa.
Jamani tupo wiki hili haliishi mtawasikia Wabunge wote wameungana na kumshinikiza SPIKA awape mashangingi na Posho
Kwani kipindi kilichopita 2005 - 2010 wapinzani ndio waliokuwa wakali kupata posho na magari mpaka 2008 Slaa pekee aliechomoa Leo haohao wana Mashamba ekari 500 huko Kigoma wamenunua kwa Wananchi na kuwauzia wageni kwa dola mara 10 zaidi je hao sio mafisadi ei kila mtu anautaka uSpika
Wakishahutubiwa na Rais hawatarudi na chochote majimboni kwani mafungu hawana na vikodi vya Halmashauri si vya mwaka huu. Uchaguzi umeisha tunyamaze tunaparuana wao wanaafuna mbuzi mnadani na watoto
anaebisha tukutane wiki ijayo mtawaona wanavyo-labua pamoja
 
Duh kama ni hivyo kaka unga kilo shi 400 sukari ya mtibwa 500
 
Strategy nzuri, hii itawafanya Mafisadi kufikiria mara mbili kabla ya kumpitisha mgombea wao na wakijichanganya tu kumwachia mzee wa vijisenti agombee basi wameumia saana tu!. Maana hata CUF hawatampigia kura ng'oo.
 
Tuombee CCM wasimpitishe Sitta; bali wampitishe Chenge. Hapo Marando bila kigugumizi atachukuwa Usipika kwa ulaini.
 
It is possible bunge lina viti kama 323 hivi hadi sasa wapinzani wana kura(viti) kama 100 bado kama 50, mavuvuzela yakijichanganya kama yalivyoanza kuzomeana kwenye vyombo vya habari yanagawa kura zao kwa chuki wakitahamaki tayari kumekucha.

Hawawezi kujichanganya, CCM kama chama wanapeleka jina moja wakiwa na msimamo wa chama wa kumuunga mgombea wao mkono.
 
Over all the comment nimeipenda ya kelli alivyomtoa Mrema wa TLP kwenye Orodha ya wapinzani, truely wasihangaike nae zaidi anaweza kuwapotosha tuu wenzake wa kambi au kutumika kuidhohofisha kambi ambayo kimtazamo ni makini sana.

Lets wish for the impossibles to be possible na Marando kuwa Spika, wanaweza kuuza kiti ilikupooza makali ya upinzani dhidi ya kura walizochakachua majimboni na za uraisi kwani kuna tetesi kuwa Chenge amechakachua kura jimboni kihalali hakushinda
 
Hongera Marando kwa uamuzi huo, hata kama utashindwa utasema nilijaribu lakini sikufanikiwa.
Lakini pia wana JF waliokuwa wanamsema Zitto mbona kaamua kujitangaza kugombea nafasi ya KUB hapa mbona kimya? Mbona sioni zile comments kwamba ampishe Mbowe na blah blah nyingine? Why kwa wengine sawa na wengine tatizo? Kwamba Marando anahistoria nzuri saana kumzidi Zitto ndio maana anaaminika atafanya vyema endapo atakuwa Spika ila Zitto ni CCM? Nimeiandika hii ili kuweka kumbukumbu sawa na kuwashauri wengi wetu tuache siasa za kizandiki na ghiliba.
 
Natamani Hamad Rashid wa CUF angesima kwa upinzani, jamaa anweza kuwa spika makini sana
 
ni marando kupitia Chadema, ana jazba, hasira na hamaki. hawezi kuwa spika wa bunge letu hili.
atanaweza kupitisha misaada ya hasira na kutuingiza taifa ktk mitafaruku hasa kwa majirani zetu

Kwani kazi ya spika ni kupitisha misaada tena? najua ulitaka kusema miswada lakini kwasababu unayoandika ni crap, ukajikuta hata unakosea. Naona mnasherekea ushindi wa chakachua kwa vificho kuogopa aibu!
 
kwa hiyo unamtaka chenge?nani kati ya chenge wako na marando anayeweka maslahi ya taifa mbele?
 

Kumbukumbu ndogo jamani. Mnamjua Mabere Marando nyie? lol. And CCM runs on loyalty.
 
Malaria Sugu saa hizi ikifika saa 9 anakuwa JEY KEY WA UKWELI
 
cuf hawana uzalendo kihivyo na bara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…