Katika kipindi cha karibuni, tumempoteza rafiki yetu, ndugu yetu, kipenzi chetu Gabriel Raphael Kamukara, maisha yake yakichukuliwa kwa ukali na ukatili wa risasi za majambazi akiwa ametokea kupata huduma za kibenki ndani ya Mlimani City complex.
Siku chache baada ya tukio hilo, kuna habari za mwananchi mwingine mwenye makazi yake maeneo ya Salasala naye amepoteza maisha katika mazingira yanayofanana kabisa.
Taarifa zinazotolewa na vyombo vya ulinzi zinaambatanisha tahadhari kwa wananchi wanaotumia comlex hiyo, kwanba wasitoke na pesa taslim kiwango kikubwa kiasi cha 'kushawishi' majambazi. Matukio niliyofanya kumbukumbu hapa ni yale ambayo yanahusu jamaa wa karibu, lakini matukio ya namna hii yamekuwa ni ya kujirudia na ni mengi kiasi cha kutia mashaka.
Mwono wa kwanza;
Hivi tukitafakari kibiashara, biashara yote kwenye hii complex ipo hatarini kwa kiasi gani? kwa maana ya kusababisha watu wakaacha (kususia) maduka, mabenki n.k, na biashara yoyote inayohusu Mlimani City? Je wenye biashara wanaridhika na hii publicity na reputation maarufu (infamous) inayozidi kushamiri?
Mwono wa pili;
Vyombo vya ulinzi na usalama vinashauri watu kutochukua na kutembea na fedha nyingi kutoka kwenye mabenki. Vyombo vya kifedha hutoa huduma kwa namna mbalimbali, ambapo tunaamini kila mteja atumie kwa utashi wake, pesa yake aliyoipata kihalali kwa jasho lake... na katika nchi yake iliyo na uhuru na amani ya mfano kwa nyingine nyingi. Je hii siyo kejeli kwa mfumo wa uhuru wa kutafuta na kutumia mapato yetu?
Mwono wa tatu;
Hivi inawezekana kweli vyombo hivi vya ulinzi na usalama (polisi, usalama wa taifa n.k. ) vipo, na matukio yaliyo kama mstari kwa kufanana yanatokea, na maelezo ya ufafanuzi na maelezo ya kutosheleza hayatolewi, na matukio yanaendelea hata kesho pengine tukasikia lingine,; imeshindikana kabisa raia wema kulindwa dhidi ya hawa wenye ma bodaboda ambao wapo palepale na wnafanya hiyo kazi kwa mazoea bila hofu?
Je, inakubalika sasa kusema kwamba itangazwe hali ya hatari Mlimani City na maduka na bishara zote zifungwe kwa sababu ulinzi hautoshi au haupo???
Maisha hayabadilishiki (irreplaceable); kwa masikitiko makubwa natoa pole kwa wote walioguswa na matukio yote yanayohusiana na Mlimani City, na kujaribu tu kuuliza swali kwa wanaohusika, wanaridhika na hali ya usalama ya jiji hili, haswa sehemu hii ya Mlimani City. Machozi ya wapendwa walioachwa ghafla kwa mshangao yawaisheni, wanaohusika wawajibike ili damu ya ndugu zetu iliyomwagika isiende bure.