Mabasi ya Luxury

Mabasi ya Luxury

Tanzania Mpya

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2012
Posts
252
Reaction score
145
Mabasi yanayoitwa luxury hapa Tanzania yanashangaza. Hayana hata huduma za tofauti! Viti ni vile vile vya kubana, ukivilaza unambinya mtu wa nyuma yako!

Angalau kenya ndani ya mabasi kama hayo wana huduma za internet (wi-fe), na viti special pale mbele (VIP) ambavyo bei yake ni kubwa kuliko vingine.

Hapa kwetu ni uswahili tu. Maana hawa jamaa wa Ubungo waongo sana, wakijua unataka luxury basi watakuambia "hili ndio lenyewe, full AC," lakini ukiwa njiani ndio utajua ukweli.

Hivi kuna vigezo vya serikali kwa basi kuitwa luxury?
 
mabasi y luxury yapo ! Nenda kapande Tahmeed utapata huduma zote hizo za luxury
 
panda najimunisa utajua habari yake kweli uko bongo bongest.
 
bora mm napenda chai maharage wenye vimini wananipa raha huku kwetu mabwepande
 
Hahaa enzi za mwalimu basi likiwa na mapazia ni luxury
 
Nadhani inachangiwa na sisi wenyewe kutokujua maana halisi ya luxury, ndio maana matajiri wananunua yutong siti za kubana ,hakuna choo wala friji wanatuambia luxury tunakubali kisa eti ni full ac ,hatujui wala hatujawahi kuona hizo luxury, nadhani Dar express alijaribu sana kutuletea word class luxury ,japokuwa naye alikuwa ananunua zile nafuu katika list. kwa uelewa wangu MARCOPOLO , IRRIZAR BUSSCAR SKS ni moja ya bodi mashuhuri za luxury bus nazo zina class zake , internationally huwezi ukawaambia abiria wako una basi luxury kama halina vifuatavyo

rear muonted engine( injini nyuma) -for on board noise reduction
Full air ride , front and rear air suspension -( busta)
two by two seat configuration
cofee pot
friji, choo ac ,heater n.k kuna mabasi mengine yana, gps navigation ,free wifi connectivity ,baadhi ya viti kuna extension kwa ajili ya kuchaji simu na laptop

lakini pili mamlaka husika haijaja na mkakati wa kuhakikisha kuwa kinacho tangazwa, ndio kitu mteja anapata, ingekuwa hivyo tusinge shuhudia watu kuvimba miguu wakati walipanda luxury bus

nawakilisha
 
Umesema ukweli sana mkuu, imenipanua mawazo. Sumatra nao wamelala, wafanyabiashara wanafanya wanavyotaka wanaendelea kuwadanganya abiria na kuwalipisha nauli kubwa kwa kisingizio cha luxury bus, yutong ya 2 x 2 only.
 
Huku bongo ukipaka rangi mpya gari yako unaruhusiwa kuiita luxury
 
Bongo ni uizi mtupu mimi naweza wapa credit kidogo dar express maana wanaonyesha kua na nia kufikia kutoa huduma za luxury hapa tz, lakini hawa wanaoleta yutong kisa ni 2 by 2 ndo waiite luxury ni makosa makubwa.
Mfano kuna hawa wanaojiita Green star wao eti dar-mby ni 35,000 kisa ni luxury tatizo ni humo ndani hakuna cha maana zaidi ya soda ya kopo na video tu huduma ambazo hata mabasi ya kawaida yanatoa sasa hua najiuliza huo uluxury wao uko wapi wakati dreva wao anatumia feni ya kawaida tu? Na gari ikisimama hilo joto lake sasa! Sumatra wake up!
 
Back
Top Bottom