Mabango ya Lema, Arusha Mjini yaichanganya CCM

Mabango ya Lema, Arusha Mjini yaichanganya CCM

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,377
Reaction score
271,800
Ni kwa vile yameandikwa NYIE SIO WAPUMBAVU , NYIE SIO MALOFA , NYIE NI WANA WA MUNGU , SISI TUNAWAPENDA .
ni Lema tena 2015, CCM wilaya ya Arusha kupitia kwa katibu wake Feruz Banno imemwandikia barua msimamizi wa uchaguzi atoe amri yaondoshwe , kwa vile yana lugha ya uchochezi , linaripoti gazeti la mwananchi .

===============================


mabango.jpg

Arusha. Mabango ya mgombea ubunge Arusha Mjini kwa tiketi ya Chadema, Godbless Lema yamezua kizazaa baada ya CCM kutaka yaondolewe.

Mabango hayo yenye sura ya Lema yanayosomeka: "Nyie siyo Wapumbavu, Nyie siyo Malofa, Nyie ni wana wa Mungu, sisi tunawapenda, Lema tena 2015," yamebandikwa katika miti, kuta za nyumba na maduka na mengi yako katikati ya Jiji la Arusha.

Katibu wa CCM Wilaya ya Arusha, Feruz Banno alidai jana kuwa mabango hayo yana lugha ya uchochezi, hivyo, wanaandika barua ya kumwomba msimamizi wa uchaguzi atoe amri yaondoshwe.

Akizungumzia sakata hilo, Lema alisema Rais mstaafu Benjamin Mkapa ndiye aliwaita Watanzania wanaotaka ukombozi kuwa malofa na wapumbavu.

"Mimi nikiwa mbunge wao na mgombea kwa mara nyingine, ninawapenda sana wananchi wangu, ujumbe huo una lengo la kuwatia moyo tu na siyo uchochezi," alisema Lema.

Hata hivyo, msimamizi wa uchaguzi wa Arusha, Juma Idd alisema bado hajapokea barua hiyo ya malalamiko kutoka CCM.

"Kama wataileta tutatazama wanacholalamikia kama kina mantiki," alisema Idd.

Wakati huohuo, Lema amemsihi Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbroad Slaa kurejea ofisini kuendelea na majukumu yake kwani muda aliopumzika unatosha.

Lema alitoa wito huo wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi jimboni Karatu uliofanyika katika Uwanja wa Mbowe.

"Nakuomba sana Dk Slaa urudi tufanye kazi, heshima ya Chadema iliyonayo sasa, wewe una mchango mkubwa na hakuna sehemu ya nchi hii ambayo hujafika ili kuhakikisha wananchi wanapata mabadiliko ya kweli, kama mapumziko yanatosha," alisema Lema.

Alisema licha ya wito wa kumtaka Dk Slaa arejee ofisini kutolewa na watu kadhaa, bado kuna kundi dogo la watu lisilotaka kiongozi huyo arudi kwenye nafasi yake hiyo baada ya sintofahamu iliyotokea kutokana na ujio wa aliyewahi kuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na baadaye kuteuliwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chadema.

Lema aliwaambia wakazi hao kuwa katika mchakato wa Lowassa kuhamia Chadema, Dk Slaa alishiriki kikamilifu tofauti na inavyozungumzwa na baadhi ya watu. "Nawaomba ninyi wananchi ambao Dk Slaa alikuwa mbunge wenu wa kwanza baada ya kuanza kwa mfumo wa vyama vingi nchini, mumsihi arudi ofisini tuendeleze mapambano ya kuwakomboa Watanzania," alisema Lema.

Mbunge wa Viti Maalumu aliyemaliza muda wake, Cecilia Paresso aliiponda kauli iliyotolewa na mgombea mwenza wa CCM, Samia Suluhu Hassan kuwa watajenga barabara kwa kiwango cha lami kutoka Karatu hadi Mbulu.

Paresso alisema Serikali iliyopo madarakani imeshindwa kujenga barabara hiyo hata kwa kilometa mbili tu, zilizopo Mbulu Mjini kwa kipindi chote cha miaka mitano.

Chanzo: Mwananchi
 

Attachments

  • Lema.jpg
    Lema.jpg
    10.1 KB · Views: 1,169
Wamuondoleee aliyesema uanachama wa CCM kwanza .. kabla ya kuondoa mabango
 
hahaaa.. mbona sisi ni malofa bhana.. tushajikubali na mwisho wa ulofa wetu ni 25 october 2015
 
Ni kwa vile yameandikwa NYIE SIO WAPUMBAVU , NYIE SIO MALOFA , NYIE NI WANA WA MUNGU , SISI TUNAWAPENDA .
ni lema tena 2015 , ccm wilaya ya arusha kupitia kwa katibu wake feruz banno imemwandikia barua msimamizi wa uchaguzi atoe amri yaondoshwe , kwa vile yana lugha ya uchochezi , linaripoti gazeti la mwananchi .

Nataka Mukumbuke....kilicho mtoa IBILISI mbinguni ni KIBURI, jamani hawa watawala wana kiburi.....aliyetoa maneno hayo ana kiburi hebu tulitazame neno la Mungu juu ya hili......Isaya. 28:-14-16, mwenye masikio naasikie....
 
Nataka Mukumbuke....kilicho mtoa IBILISI mbinguni ni KIBURI, jamani hawa watawala wana kiburi.....aliyetoa maneno hayo ana kiburi hebu tulitazame neno la Mungu juu ya hili......Isaya. 28:-14-16, mwenye masikio naasikie....
ubarikiwe mkuu .
 
Baada yakufuatilia kampeni za Magufui na ccm, nimefanya utafiti wangu juu ya mwitikio wa Watanzania i na kugundua yafuatayo:-

Magufuli na ccm wamekwama vibaya kutokana na serikali ya ccm imekuwa ikifanya mateso ya Wazi kwa watanzania kwa miaka mingi bila kujali, huku ikitetea na kukumbait mafisadi na udharimu yakiwemo matumizi mabaya ya madaraka, uvunjaji wa haki za binadamu, ubadhilifu wa mali za uma na matumizi yasiyofaa ya raslimali za taifa.

Hivyo Watanzani wameamua kumwonyesha Magufuli na team yake kwamba wao si wapumbavu na wajinga kama wanavyowaita.

1. Kukosa hoja kwa ccm na kubaki kunakilil na kutelekeza hoja ya upinzania kama ufufufaji wa viwanga kikwemo General Tyre, ujenzi wa reli, ufufuzi wa ATC, Elimu bure nk.vimedhihirisha wazi ccm haina uwezo wa kuongoza kwa kuwahaina maono wala mipango sahihi ila inasubiri UKaWA waseme halafu ccm itekeleze. Kwa mantiki hiyo, ccm wanataka ikae chini, isubiri maelekezo kutoka serikali ya UKAWA nini cha kufanya.

2. Kila wakati wa kampeni ccm imekuwa na maneno mengi, ilani ndefu isiyoeleweka na ahadi kemkem lakini mwisho wake nchi imezidi kuwa katika uduni kuliko awali. Tangu uhuru hadi sasa imekuwa ikijibainisha kuwa na vita dhidi ya ujinga, umaskini na Maradhi vita ambayo haijawahi kushinda. Badala yake imezalisha adui wengine wakubwa ufisadi na rushwa hivyo kuzidi kuliangamiza taifa.

Watanzania wamechoshwa na maneno yasiyokuwa na vitendo ya ccm. Lakinii pia wamechukizwa na taiba za ccm kusema maneno mengi na kutenda kinyume chake hivyo kuwafanya Watanzania wawe wakimbizi katika nchi yao. Wameapa mwisho wa ulaghai huu ni 25 October.

3. Kuficha Identity ya chama chao na kumweka magufuli kwenye matangazo yao kunadhihirisha hila na kuwaogopesha Watanzania kwamba safari hii wakikosea wamchague chambo cha ccm Magufuli, watakwisha na Tz haitakuwepo tena usoni pa nchi kwa sababbu ufichaji huo wa ccm ni ishara ya kuficha uovu mkuu usiotakiwa kwa binadamu. Wanasema hawadanganyiki.

4.Ccm imeharibu uchumi wa Tanzania na kudunisha elimu, huduma zote za jamii na maisha ya Mtanzania huku ikikiri kwamba haijui kwa nini Wtanzania ni duni vile. Kitendo cha kuendelea kuwahadaa kwamba eti Ccm ileile kupitia magufli itainua uchumi, ni kuwazidishia maumivu kwa kuwatukana mara kwa mara kwamba ni wapumbavu na malofa.
Wanataka kuonyehs kwamba wao sioy Mapumbavu ingawa ccm imewafanya malofa ili iwatawale kwa kuwadangamiza milele.


5.Ahadi za milioni 50 kila kijiji bila utafiti wa kina na ufahamu wa matatizo yao ya msingi ni kuwanunua kwa peremende. Ccm ijiandae kuchinjiliwa mbali


6. Hasira za Watanzania zinazidishwa na timu ya ccm kubeba hoja ya ufisadi wakati mafisadi wamezaliwa na wanalelewa na ccm yenyewe. Kitedno cha Magufli kusingizia atafungua mahakama ya mafisadi, kinaleta chuki kubwa kwa watanzania dhidi ya ccm kwa sababu, ccm iko madarakani miaka yote. Hao mafisadi wamezaliwa na kulelewa katika serikali gani kiasi sasa wamekuwa wengi na wakutisha hadi waundiwe mahakama? wakati wanachipua an kuongezeka ccm na serikali yake walikuwa wapi kuchukua hatua? Kama wamekaa na mafisadi ndani ya chama choa na serikali yao, bila kuchukua hatua halafu leo wanalalama kwa wanachi, uko wapi uwezo wa ccm kuongoza nchi?

Katika orodha ya mwembe yanga, kulikuwa na watuhumiwa 11 wa ufisadi. Ameondoka Lowasa kumi na moja wamebaki ccm. Kama ccm haiwahadai watanzania kwa nini imnyoshee Lowasa na mmoja aliyeamua kubadilika na iwakumbatie 10 plus walioko ccm? Huu siyo uhuni kwa taifa?

Mahakama tangu lini iakwa ni kiwakzo ccha kuwashughulikia mafisadi kama siyo kuwafanya Watanzania wapumbavu na malofa? Mafisadi wa Richmond, Kiwira, Meremeta, Kagoda, Mtambo wa gas, Escrow, nk. ni lini mliwapeleka mahakamani kama serikali? Wananchi wanahoji, mahakama gani ilishindwa kuwahukumu kwa kukosa competence? Ni upungufu upi wa sheria umekwamisha hata ufafanuzi wa fedha zilizobebwa taslimu kutoka Stanbic kwenye scandal y a Escrow?


7. Wawakilishi wa wananchi UKAWA, walisimamia katiba ya nchi lakini ccm waliipinga kwa sababu ilikuwa inakomesha rushwa, ufisadi na matumizi mabaya ya madaraka. Katiba ya Wananchi ilikuw anasimamia na kulinda haki na utu wa Mtanzania. Lakini kwa kuwa huo ndio mtaji wa ccm walisimama hadharani wakiipinga na hata kufikia hatua ya kuchachakua matokeo ya kura za Zanzibar. Leo hii ccm itawaambia nini Wtanzania? Wamesema yote wanayakumbuka.

Watanzania sioy Wapumbavu. Wameapa kuingamiza ccm kwa kuwatesa, kuwaibia na kuwalaghai kwa maneno na vitisho kwa miaka zaidi ya 50, na mwisho wanapodai haki zao kuwaita wapumbavu na malofa.

Ccm na Magufuli wake wamekwama na kushindwa vibaya hata kabla hawajamaliza kampeni kwa kuwa kila wanalolifanya linaongeza maumivu na hasira za Watanzania.

Wameshasema Magufuli na ccm yote hawana hoja yoyote ya maana, hawana nia ya dhati wala uwezo wa kuleta mabadiliko yanayotakiwa na Watanzania kwa sababu Ccm yote ni wadau wa mateso ya Watanzania na anguko la uchumi wa taifa.

Wanaona ccm na magufuli hawana sababu ya kuendelea kupita pita kwa Watanzania kwa sababu Ccm ilishajipigia kampeni ya hapana kwa matusi yake na mateso yake kwa Watanzania.

UKAWA NDIYO CHAGUO LA WATANZANIA BILA KUJLI LOLOTE LISEMWALO WALA LIONEKANALO.

CCM KWA HERI.
 
hakika siasa za mh lema ni za kisasa mno!
 
Back
Top Bottom