Mabango ya kusifu utumishi wa viongozi (Samia & Magufuli)

Mabango ya kusifu utumishi wa viongozi (Samia & Magufuli)

Promise Land

Member
Joined
Aug 13, 2017
Posts
37
Reaction score
45
Tangu kuanza kwa awamu ya tano mwaka 2015 alipoingia madarakani aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na kisha kupokea Samia Suluhu baada ya kifo cha mtangulizi wake, tangu wakati huo kumekuwa na mabango mengi sana kwenye kila Kona ya barabara na hata matangazo kwenye vituo vya redio na televisheni yakisifu kile kinachodaiwa kuwa ni utendaji wao mzuri.

Mimi najiuliza mbona awamu zolizopita hapakuwa na haya mapambio na hali ya maisha na uchumi wa nchi ulikuwa vizuri zaidi ukilinganganisha na wakati huu? Na ni kwanini serikali hii inapenda kumtaja Rais kama mtoaji wa fedha za miradi ilihali wanajua fika kuwa ni jasho na kodi za watanzania?

"KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA" Hawana lolote walifanyalo, nia yao ni kushinda uchaguzi na kubaki madarakani na ndiyo sababu ya kwanini hawaacha kujiweka kwenye mabango kila uchao.
 
Hilo bango hapo chini ndio stahiki ya Magufuli, ndio kazi zake hizo.

screenshot_20230316-012242-jpg.2553815
 
Binadamu kweli umezaliwa na unasali kanisani au msikitini unamfanyia mtu mwingine kihivi sijui wakiona wanajisikiaje roho za hivi hata wanamzidi shetani
 
Mimi binafsi nimechoshwa na hivi vituko vya kusifia sifua raisi kutoa hela as if zinatoka mfukoni mwake ili hali ni haki na jasho la wananchi wa JMT.

Imekuwa kero sana kwenye TV na redio namna ambavyo kila wizara,mkoa,wilaya,Taasisi n.k kurusha vipindi kwenye vyombo vya habari ya kuwa Samia kile” samia hiki”

Ifike hatua watanzania tuwe serious na maisha hatakama yamekuwa magumu sana.

Tazama wakenya walivyo komaa kisiasa na kifikra, ila mivijana ya Tanganyika imekuwa ya hovyo.

Personally i declare interest kuwa nakataa kuwa miongoni mwa vijana waliodumaa kifikra na kushinda kwnye majukwaa mbalimbali kuwa “mama mama mama” niko nasaka hela

ushauri, Tuweke jitihada kwenye kupata katiba mpya na si ujinga
 
Tangu kuanza kwa awamu ya tano mwaka 2015 alipoingia madarakani aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na kisha kupokea Samia Suluhu baada ya kifo cha mtangulizi wake...
Rais Samia Suluhu amegusa maisha ya watanzania wengi na ndio maana unaona kila mtu anamzungumzia na amefanya maendeleo haya ndani ya muda mchache tu katika uongozi wake acheni tumsifie jamani maana kuna watu walihisi hataweza lakini ameweza na amevuka malengo miradi inakamilika kwa wakati uchumi unaendelea kupaa acheni tumsifu Mama anaupiga mwingi kila sekta
 
Maendeleo gani amefanya?Kwa Sababu kuna mfumuko wa bei na miradi ya sasa hivi ni ya magufuli.
 
Rais Samia Suluhu amegusa maisha ya watanzania wengi na ndio maana unaona kila mtu anamzungumzia na amefanya maendeleo haya ndani ya muda mchache tu katika uongozi wake acheni tumsifie jamani maana kuna watu walihisi hataweza lakini ameweza na amevuka malengo miradi inakamilika kwa wakati uchumi unaendelea kupaa acheni tumsifu Mama anaupiga mwingi kila sekta
Maendeleo! Vilio vya ugumu wa maisha vinasikika kila Kona ya mitaa ya nchi hii wewe unasema maendeleo? Yapi hayo embu yaainishe hapa, tozo +tozo+tozo vitu bei juu, bado unimba kwaya na ngonjera za aina ileile?
 
Mimi binafsi nimechoshwa na hivi vituko vya kusifia sifua raisi kutoa hela as if zinatoka mfukoni mwake ili hali ni haki na jasho la wananchi wa JMT...
Kuna Bango linasema Mama hana Mbambamba daahh
 
Tangu kuanza kwa awamu ya tano mwaka 2015 alipoingia madarakani aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na kisha kupokea Samia Suluhu baada ya kifo cha mtangulizi wake, tangu wakati huo kumekuwa na mabango...
Taasisi za umma zinatumia mabilioni ya walipakodi kumtangaza na kumsifia rais. Huu ni uchawa na upumbavu uliopitiliza.

Niliacha kusikiliza radio one kwa usumbufu wa matangazo ya kila mara ya "nukuu za rais..." Ukiona kiongozi anayelazimisha kusifiwa, jua ni dhaifu, hakuamini na hafai
 
Hilo bango hapo chini ndio stahiki ya Magufuli, ndio kazi zake hizo.
Daah...kwa kweli hili jambo me lilinipa huzuni saaana. Niliumia mno huyu mtu kufanyiwa ukatili wa namna hii. Mungu amemuweka hadi leo na mzima wa afya ili aoneshe ukuu wake mbele ya wanadamu.
 
Tangu kuanza kwa awamu ya tano mwaka 2015 alipoingia madarakani aliyekuwa Rais wa Tanzania John Pombe Magufuli na kisha kupokea Samia Suluhu baada ya kifo cha mtangulizi wake, tangu wakati huo kumekuwa na mabango mengi sana kwenye kila Kona ya barabara na hata matangazo kwenye vituo vya redio na televisheni yakisifu kile kinachodaiwa kuwa ni utendaji wao mzuri.

Mimi najiuliza mbona awamu zolizopita hapakuwa na haya mapambio na hali ya maisha na uchumi wa nchi ulikuwa vizuri zaidi ukilinganganisha na wakati huu? Na ni kwanini serikali hii inapenda kumtaja Rais kama mtoaji wa fedha za miradi ilihali wanajua fika kuwa ni jasho na kodi za watanzania?

"KIZURI CHAJIUZA KIBAYA CHAJITEMBEZA" Hawana lolote walifanyalo, nia yao ni kushinda uchaguzi na kubaki madarakani na ndiyo sababu ya kwanini hawaacha kujiweka kwenye mabango kila uchao.
 
Mimi binafsi nimechoshwa na hivi vituko vya kusifia sifua raisi kutoa hela as if zinatoka mfukoni mwake ili hali ni haki na jasho la wananchi wa JMT...
Unaweza ukajirekodi ukieleza hayo uliyoandika hapo kisha ukatuma mitandaoni, naimani njia hiyo itasambaa sana na ujumbe wake unazingatiwa kuliko hivi tunavyoishia kuandika tu humu inaishia kubaki tu humu humu.

Kipindi cha Magufuli nakumbuka kuna mtu aliwahi kufanya hivyo alimchana sana Magufuli, kama hatuwezi kufanya kama Kenya basi hata njia hiyo pia tunashindwa?
 
Na ni kwanini serikali hii inapenda kumtaja Rais kama mtoaji wa fedha za miradi ilihali wanajua fika kuwa ni jasho na kodi za watanzania?
1. Kwa wananchi ni uji uliopitiliza. Hawajitambui kwamba fedha inayojengea miradi ni jasho lao, hata mikopo watalipa wao.
2. Kwa viongozi (wanasiasa) ni unafiki wa kiwango cha juu kabisa. Ni kujikomba.
 
Back
Top Bottom