Point yako ni nzuri sana, lakini hukuifanyia utafiti kwani hiyo inawezekana katika nchi ambazo wasiokuwa na kazi ni 10-15%. Kwa maneno mengine umeleta nadharia uliyosoma Ulaya bila kuitafsiri katika mazingira ya Afrika au Tanzania kama ukipenda.
Katika nchi kama Tanzania ambayo ina watu wasio na kazi mpaka kufikia 35% hiyo nadharia haifanyi kazi. Kwa vile suala la elimu sio la kungoja, ndio maana seriukali ikaja na mtindo- kama huna kazi basi pata kazi ya kujenga shule, vyatua tofali na kujenga na serikali kwa kutumia hizo kodi ndogo itajazia pale pesa inapohitajika.
Mkisoma ulaya, pindi mnaporudi nyumbani mnakazi kubwa sana ya kutafsiri hayo mliyoyasoma katika mazingira mnayofanyia kazi, vinginevyo elimu mliyosoma ni kazi bure.
Kuna uhusiano gani kati ya maisha ya watoto hawa na serikali iliyoko madarakani? kama tungekuwa tuna uhusiano wa aina hii Dar-es-Salaam ndio wangekuwa wa kwanza kuikataa CCM.. but guess what? watachagua madiwani wengi wa CCM, wabunge wengi CCM na usishangae JK akipata kura nyingi Dar!!!
Kuna uhusiano gani kati ya maisha ya watoto hawa na serikali iliyoko madarakani? kama tungekuwa tuna uhusiano wa aina hii Dar-es-Salaam ndio wangekuwa wa kwanza kuikataa CCM.. but guess what? watachagua madiwani wengi wa CCM, wabunge wengi CCM na usishangae JK akipata kura nyingi Dar!!!
Ni propaganda!! Na kama sio propaganda basi ni kuendeleza na kuukubali uvivu.
Ukweli Tanzania ya leo hii wanafunzi wanalia na ukosefu wa walimu sio mijengo na madawati. Kijijini kwetu kila mtoto akiingia darasa la kwanza ni lazima aje na dawati lake. Kama baba unaweza kumchongea kiti na meza ya kukaa nyumbani mtoto wako, kwanini ushindwe kumtafutia kiti cha kukaa mtoto wako pale shule anapotumia zaodi ya masaa 7, siku 5 kwa wiki.
Eti ninawapenda watoto wangu, ni lazima utafsiri neno kupenda kwa vitendo. Sina huruma na hawa watu hata kidogo, lazima wachangie katika elimu kama hawana pesa basi ni misuli yao ndio inahitajika.
kwa nini kila mwanafunzi akianza shule ya msingi au sekondari aende na dawati. Na siku ukimaliza std 7 au form 4 hauruhusiwi kuondoka na dawati lako. Siku hizi walimu wameona ndio pakupatia dili unapewa form imeorodhesha dawati na malipo yake hapo pembeni. Mtu unajiuliza shule imekuwepo miaka zaidi ya 10 madawati yamekwenda wapi na wanafunzi wamekuwa wakipeleka madawati kila mwaka????
Na ni familia ngapi huko majumbani wanaketi kwenye viti au meza na sio kwamba hawataki lakini wanaona ni bora chakula kuliko kununua meza na viti, mambo ya vipaumbele ambayo viongozi wetu wameshindwa kutumia akili zao walizopewa bure na mungu pamoja na kujienjoy na elimu za bure mpaka phd lakini ni sawa na bure tu hakuna mpangilio wa kipi kije kwanza na kipi kifuate na kipi hakina umuhimu. Kwao wao wanaanza na the least important on the list. This is not the way to go hata nyumbani kwako mwenyewe lazima uwe na vipaumbele sembuse a whole nation.
ELIMU BORA
CHAGUA CCM
CHAGUA KIKWETE
Amina kubwa sana na mapenzi ya BWANA na yatimie.Ha ha ha haaaaaa, tuliahidi elimu bora tumetekeleza!!! inasikitisha sana. Bahati mbaya hao watoto moyoni wanasema asingekuwa yeye hata hapo wasingekaa. Mungu wangu na Mungu wa Watanzania wote nakuomba utufunulie kuujua ukweli tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu. Tuwachague viongozi ambao watatuongoza kwenye maendeleo ya kweli. Tazama wana wako hapo juu wanavyopata shida, Mungu ni imani yangu shida hizi wanazopata si kwa mapenzi yako Baba uliye juu, ila ni kwa kosa la watu wako ambao kwa sababu ya vipande vya khanga, fulana, kofia, pilau na pombe wakalewa wakawapa madaraka ya kuongoza nchi yako watu wasiokuwa na uwezo. Ndiyo maana ninakuomba sasa ukageuze mioyo yetu ukatuelekeze kutenda yaliyo mema kwa kufanya kucahgua viongozi wenye uwezo wa kutenda na siyo kunena, wenye uwezo wa kuthubutu na siyo kuota tu. Ameni
Peremende au wanasubili kupata MARELIA na Kipindupindu huoni hapo pembeni! Daaaa halafu eeeti wanapewa MBU NET za nini!? kuna watu ambao hawajui mahitaji ya watanzania! Ndiyo maana bagamoyo ipo kama ilivyo!Hawa hata zile peremende hawakupata
ELIMU BORA
CHAGUA CCM
CHAGUA KIKWETE
Hata SOMALIA walioko vitani miaka na miaka sio hivi...!
ELIMU BORA
CHAGUA CCM
CHAGUA KIKWETE