Zakaria Lang'o
JF-Expert Member
- Apr 2, 2012
- 2,593
- 2,768
Mods naomba maoni haya yamfikie Mhe. Tundu Lissu kama mwanasheria na mpigania haki na utawala wa Sheria katika nchi yetu.
Kwa miaka mingi tangu ujio wa vyama vingi, Chama cha Mapinduzi kimekuwa kikiwatumia Mabalozi wa mashina ya Chama kwa shughuli za kiserikali isivyo halali. Mabalozi hawa ambao hawamo katika mlolongo wa uongozi wa serikali kikatiba na kisheria wamekuwa wakifanya yafuatayo isivyo halali:

- Kusikiliza kesi na mashauri katika maeneo yao huku wakijuwa wazi kuwa hawana mamlaka kisheria ya kufanya hivyo. Tabia hii imesababisha Chama cha Mapinduzi kupitia kwa mabalozi hawa kupoka mamlaka ya viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji.
- Kushiriki kuuza maeneo kwa kugonga mihuri yao ya shina katika karatasi za mauziano yanayofanywa na wananchi kinyume cha utaratibu. Miongoni mwa lawama wanazotupiwa viongozi wa serikali za mitaa, vitongoji na vijiji juu ya matumizi mabaya ya mihuri kwa hakika wahusika wakuu ni mabalozi waliojivika majukumu ya kiserikali kinyume cha utaratibu wa kikatiba na kisheria.
- Kutambuliwa na taasisi mbalimbali za kiserikali na za kibinafsi kama polisi, mahakama, mabenki n.k ni ishara mbaya ya vyombo vyetu kutojali kanuni za utendaji wa serikali, hivyo kusababisha mkanganyiko wa kuchanganya utendaji wa viongozi wa Chama cha Siasa na ule wa serikali. Inashangaza kwamba hata mahakama ambayo ndiyo inapaswa kusimamia sheria huweza kumwita balozi wa shina kuto