Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,387
- 3,481
Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Njombe Kimefanikiwa kushinda uchaguzi wa serikali za Mitaa katika vijiji 377 kati ya 381 Mitaa 81 kati ya Mitaa 82 na Vitongoji 1819 Kati ya 1832 Vilivyopo mkoani hapa sawa na asilimia 99.7.
Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Siasa Uenezi na Mafunzo CCM Mkoa wa Njombe Josaya Luoga imesema kazi nzuri waliyoanza kuifanya tangu uchaguzi uliopita wa 2019 imewajengea imani kubwa na kusababisha wananchi kuwachagua tena kwa kishindo ikiwa ni ishara ya kwenda kufanya vyema katika uchaguzi mkuu ujao.
Luoga amesema katika nafasi za wajumbe mchanganyiko wa serikali za vijiji 3710 CCM Imepata wajumbe 3698 jambo linaloonesha kuwa chama hicho kinakubalika zaidi na kuaminika katika Jamii.
Kutokana na Ushindi huo Chama Cha Mapinduzi kimepongeza jitihada za wananchi kukiamini chama hicho na kuwataka kwenda kushirikiana vyema na viongozi waliowachagua katika kujiletea maendeleo.
Luoga amesema katika nafasi za wajumbe mchanganyiko wa serikali za vijiji 3710 CCM Imepata wajumbe 3698 jambo linaloonesha kuwa chama hicho kinakubalika zaidi na kuaminika katika Jamii.