Ndugu wana jamvi, katika duru mbalimbali baada ya kikao cha kawaida cha kamati kuu ya CHADEMA, ishu inayozungumzwa zaidi ni uchaguzi na upangaji safu ya juu ya uongozi wa chama kwenye uchaguzi ujao wa chama 2013.
Nafasi ya Mwenyekiti>
1.Freeman Aikaeli Mbowe - katika duru mbalimbali bado anapewa nafasi kubwa kuendelea na nafasi yake. Kiumri, uzoefu, uongozi thabiti bado CHADEMA inamuhitaji KAMANDA wa Anga (kama wanavyoenda kumwita) aendelee kukongoza kwa miaka mingine mitano.
Tishio alikuwa ndugu Zitto Z. Kabwe mbye kw kutambua mchango wa Freeman Mbowe na athari za uamuzi wa kuamua kugombea safari hii ameamua hatagombea.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti.
Yapo Majina mengi yanatajwa kubwa upepo unavuma kwa kasi kwa Prof. Abdallah Jumbe Safari, mtu anayefahamika kwa misimamo yake thabiti, anaeichukia CCM kwa dhati. Yupo tayari kumkosoa yeyote kistaarabu bila kujali nafasi yake.
Tishio yaonekana bado Prof. Safari ni mgeni ndani ya siasa za CHADEMA.
Pongezi kwa mzee Arfi kuamua kupisha wengine.
Nafasi ya Katibu Mkuu.
wapenda mabadiliko ndani ya chama wanaona ni vyema Dr Wilbroad Peter Silaa yamfaa sasa kupumzika au kupisha damu mpya ili kuendeleza mapambano kwa kasi kubwa zaidi na Ndugu Silaa aende kuwa mwenyekiti wa baraza la wazee
majina yanayo tajwa sana ni
1. Zitto Zubeir Kabwe
2. Tundu Antiphas Mughwai Lissu.
Ndugu Zitto Zubeir Kabwe kutokana na aina ya siasa anazozifanya sasa inampa wakati mgumu kukikwaa cheo hiki kw kiasi fulani amepoteza imani kwa wanachama wenzake na anaonesha anasimamia zaidi malengo binafsi dhidi ya yale ya chama.
Ndugu Tundu Lissu - ni kiongozi mwenyew msimamo mkali anaonekana yupo tyari kusimamia nidhamu ndani ya chama bila upendeleo.
kwa vyovyote TUndu Lissu anaweza kukikwaa cheo hiki.
Naibu Katibu Mkuu
1.Bara (Tanganyika) - Ndugu Zitto Z. KAbwe anatajwa kuendelea katika nafasi yake.
2. Visiwani (Zanzibar) - zipo tuhuma za kupwaya kwa Naibu wa sasa Ndgu Yusuph Hamad japo mbadala wake haujaonekana kwa sasa,
Chadema ina kazi zaidi kujipanga Zanzibar.
kwa maoni zaidi ndugu John J Mnyika ameonesha kaimudu zaidi nafasi yake ya uenezi
Tutarajie mabadiliko ya 50/50 kwa sura za Kamati kuu na viongozi w mikoa potential kisiasa - Mwanza, Mbeya, Arusha, Kilimanjaro na Shinyanga.
Lengeri.
Kuna ukweli fulani hapa. Ila Zitto anafaa kuwa katibu mkuu wa CHADEMA.
mkuu acha majungu na umbeya. Zitto bado ni jembe.Zitto anaendesha siasa za kuua chama ili binafsi afaidike. Hafai kwa nafasi yoyote.
Ninauhakika hiyo POST imetoka LUMUMBA,ukiisoma ina maana moja tu ya kumtoa Dr slaa nje ya ulingo wa siasa wakati yeye ndiye anayeang'aa kuliko mwanasiasa mwingine yeyote wa upinzani na hata ndani ya chadema..Dr slaa anakubalika kuchukuwa cheo chochote ndani ya chadema na nchi.CCM bwana wanamuogopa sana Dr slaa kiukweli ukiangalia ndani ya ccm hakuna mtu yeyote atakaye mtoa Dr slaa kwenye mbio za kuingia Ikulu..ndiyo maana kila aina ya mbinu inatumika kumuweka Dr slaa mbali na mbiyo hizo za Ikulu.ngoja tuone ni mda tu utakao sema Dr slaa njia ya kuingia ikulu inaonekana kuwa wazi kwake,sababu ndani ya ccm kwakweli hakuna kiongozi yeyote anayeaminiwa na Watanzania wengi kulinganisha na Dr slaa.
Angalia mleta mada anakwambia ZZK haaminiki kwenye nafasi ya katibu mkuu lakini anaaminika kwenye nafasi ya N/katibu mkuu,why??? nawaombeni wanamageuzi wa kweli tukomae sana huku kwenye mitandao hawa jamaa wameshajua kuwa huku kuna nguvu kubwa ya ushawishi,wanabadilisha ID kila siku na kutuchanganyia habari.DR SLAA FOR PRESEDENT.
:target:HATA MIMI MILIPOKUWA NASOMA THREAD YA MLETA THREAD NIMENUSA HARUFU YA LUMUMBA KWANI HATA HUKO KWENYE KIKAO CHA KAMATI KUU YA CDM HICHO KITU HAKIKUWEMO HATA KWENYE MENGINEYO. NAFIKIRI LENGERI AMUAMASISHE NAPE KUSOMA MADA YAKE ILI HATIMAE ATIE CHAKE MFUKONI KWAN AMESHAINGIZA CKU.Ninauhakika hiyo POST imetoka LUMUMBA,ukiisoma ina maana moja tu ya kumtoa Dr slaa nje ya ulingo wa siasa wakati yeye ndiye anayeang'aa kuliko mwanasiasa mwingine yeyote wa upinzani na hata ndani ya chadema..Dr slaa anakubalika kuchukuwa cheo chochote ndani ya chadema na nchi.CCM bwana wanamuogopa sana Dr slaa kiukweli ukiangalia ndani ya ccm hakuna mtu yeyote atakaye mtoa Dr slaa kwenye mbio za kuingia Ikulu..ndiyo maana kila aina ya mbinu inatumika kumuweka Dr slaa mbali na mbiyo hizo za Ikulu.ngoja tuone ni mda tu utakao sema Dr slaa njia ya kuingia ikulu inaonekana kuwa wazi kwake,sababu ndani ya ccm kwakweli hakuna kiongozi yeyote anayeaminiwa na Watanzania wengi kulinganisha na Dr slaa.
Angalia mleta mada anakwambia ZZK haaminiki kwenye nafasi ya katibu mkuu lakini anaaminika kwenye nafasi ya N/katibu mkuu,why??? nawaombeni wanamageuzi wa kweli tukomae sana huku kwenye mitandao hawa jamaa wameshajua kuwa huku kuna nguvu kubwa ya ushawishi,wanabadilisha ID kila siku na kutuchanganyia habari.DR SLAA FOR PRESEDENT.