Shayu
Platinum Member
- May 24, 2011
- 608
- 1,658
Maadili ni kama kingo za mto na binadamu ni mto. Unaweza kufikiri madhara ya mto unapofurika na kingo zake kuharibika au uhai wa mto pasipo kingo Ni nini madhara yake.
Ni dhahiri kabisa hautokuwa na mwelekeo maalum, Utaleta madhara makubwa kwa binadamu, mimea na hata mifugo na wanyama wengine.
Kwahiyo maadili yanatuelekeza sehemu tunapotaka kwenda na yanatukinga dhidi ya uharibifu.
Maadili ni muhimu sana katika ujenzi wa taifa. Maandeleo ya kiuchumi hayawezi kuwepo pasipo maadili. Hata yakiwepo hayawezi kulindwa.
Hatuwezi kuwa na jamii zenye mpangilio mzuri pasipo maadili.
Maadili ni kitu ambacho kipo ndani ya binadamu kinachomwelekeza kati ya sahihi na potofu.
Taifa lazima lijengwe katika misingi ya maadili ndipo maendeleo ya kiuchumi yatapokuja, maadili ni msingi wa kwanza katika taifa.Lazima tujenge maadili ya watu wetu, lazima tujenge maadili ya familia zetu na vijana wetu, lazima tujenge maadili ya viongozi.
Hatutaweza kulilinda taifa letu liendelee na kukua kwa vizazi vingi pasipo kuweka mkazo katika maadili ya watu wetu.
Tunaweza kusema maadili si muhimu, tuwafundishe watoto wetu elimu ya kawaida tu, wafike chuo kikuu wapate ujuzi wao, wakipenda starehe kupita kiasi tuwaache, wakiwa wazinzi na walevi tuwaache, mimi sifikirii kijana mwenye tabia za namna hii unaweza kumpa majukumu akawa mwaminifu, akawa mchapa kazi hodari nk, ni lazima tuangalie upya maadili na nidhamu za watu wetu, hatuwezi kujenga chochote bila nidhamu na bila maadili.
Mkandarasi ambaye tumemfundisha kwa fedha zetu, hatokuwa na maana kwetu kama tukimpa kazi anachakachua, siku chache inaharibika . Elimu yake itakuwa haina maana. Kimantiki amefundishwa ajenge barabara na awe mwaminifu, ili barabara zetu zidumu na tuzikabidhi kwa vizazi vyetu vijavyo, kimsingi ni kujiibia sisi wenyewe, sisi sote ni taifa moja na dhumuni letu ni kujenga taifa hili kwa faida ya vizazi vyetu vijavyo, tunaweka rehani baadae yetu na ya watoto wetu kwa ujinga wa kutokufikiri na kuelewa sisi ni wamoja na jukumu letu ni kulilinda na kulijenga taifa hili na vizazi vyetu.
Kunyanyuka na kuanguka kwa tawala yeyote ile, kunategemea sana misingi ya kimaadili na kinidhamu ya taifa hilo, pasipo nidhamu taifa lolote haliwezi kupiga hatua kimaendeleo, taifa lisilo kuwa na nidhamu ni kama mbegu zilizomwagwa shambani bila mpangilio mzuri haziwezi kuzalisha chochote, mimea itaota na kufa, utakuwa na watu upande mmoja wanajenga taifa na wengine wanaiba kile tunachokijenga, hivyo hatutasimamisha kitu chochote, utazaa raia wasiojua majukumu yao kwa taifa lao , utazaa watu wabinafsi na mantiki yote ya sisi kuishi kama taifa itafutika, ambayo ni kushirikiana sisi kama binadamu katika undugu na matatizo yanayotukabili, kufanya juhudi za pamoja ili maisha yetu yawe rahisi zaidi na yenye ubora zaidi.
Elimu na sheria vina nafasi kubwa sana katika kujenga maadili ya jamii, katika mwelekeo ambao tunautaka na katika kubadilisha tabia za watu, ili kujenga raia wema na kuunda taswira ya taifa tunalolihitaji na kulinda utaratibu na muundo mzima wa taifa. Pasipo sheria hatuwezi kuwa na kitu kinachoitwa taifa.
Ni kama yai na gamba lake, taifa lisipotii utawala wa sheria kuna uwezekano mkubwa taifa hilo kusambaratika. sheria ndizo zinazolinda taifa na ni jukumu la kila raia kuzitii kwani tumejiwekea sisi wenyewe kupitia wawakilishi wetu bungeni na nyingine ni sheria asilia zinazolinda mahusiano yetu kama binadamu, tumeunda vyombo vya kutunga na kutekeleza sheria hizo, tumeunda mahakama, polisi na bunge, lengo letu ni kujenga jamii bora yenye nidhamu na utaratibu, amani yetu itakuwepo ikiwa vyombo hivi vitafanya kazi yake kikamilifu na kwa uaminifu Na kwa mashirikiano bila kuangalia vyama bali vikisukumwa na uzalendo na hamu ya kuona taifa hili likiendelea, lazima tutambue sisi ni watu wamoja na lazima tuwe na malengo kama taifa.
Kwa akina baba wa taifa hili watambue kwamba wao ni sehemu ya utawala wa taifa hili, wana majukumu ya kulea familia zao katika maadili bora, ni ukweli kwamba asili ya taifa huanza na familia inayotokana na mwanamke na mwanamme, unakuja ukoo, kabila na kuendelea, sisi tumejumuika makabila tofauti kufanya taifa hili , ni lazima tuwe wamoja katika malengo yetu na kauli zetu, ni lazima tujue tunahitaji nini katika dunia hii. Tulee watoto wetu katika maadili bora tukishirikiana kama wazazi ili kuweka misingi imara ya taifa letu, tutakapo kuja pamoja katika malengo yetu ndipo tutakapofanikiwa katika kila jambo tutakalofanya, wazee wote wa taifa hili lazima wajue wanawajibu wa malezi kwa vijana wa taifa hili , wawe wamewazaa au hawakuwazaa tutakapo walea watoto wetu kwa pamoja ndipo tutakapofanikiwa na taifa letu litanyanyuka, hatutaweza kusikia neno ufisadi katika taifa hili tena.
Katika makabila mengi tulikuwa na mfumo unaoendana na rika, vijana walikuwa na wajibu wa kuangalia wadogo zao, wazee walikuwa na wajibu wa kuwaangalia vijana, tulikuwa na ushirikiano mzuri kati ya jirani na jirani, hivyo kupelekea mtaa kuwa ushirikiano mzuri, tukiwa na ushirikiano mzuri kati mtaa na mtaa tutakuwa na ushirikiano mzuri kati ya kitongoji na kitongoji na kuendelea, taifa huundwa kutoka chini ngazi ya familia hadi juu, uimara na ubora wa familia una nafasi kubwa katika kujenga taifa imara.Mfumo wetu wa uongozi ni muhimu katika ujenzi wa taifa imara na kujenga jamii ya watu wastaarabu.
Wazazi lazima wawafundishe watoto wao umuhimu wa taifa hili kwao na umuhimu wa historia yetu kama taifa. Ni wapi tumetokea, nini matumaini yetu na dhamira zetu kama Taifa. Ni lazima tujue ni vitu gani vimetuunganisha sisi kuwa taifa. Lazima tujue umoja wetu ni jambo la msingi kabisa katika ujenzi wa taifa imara. Sisi wote kwa pamoja tumeweka dhamana zetu kwa serikali ili waratibu na kututengenezea mifumo mizuri itakayoturahisishia maisha yetu kuwa mazuri zaidi na bora.
Hatutaweza kutoka hapa tulipo kama hatutakuwa wazalendo na wenye jitihada katika kuona taifa letu linabadilika na kuwa lenye kujitegemea na lenye heshima miongoni mwa mataifa mengine. Naamini tukifanya jitihada ili kuondoa taifa hili hapa lilipo tunauwezo mkubwa sana wa kuushangaza ulimwengu. Ni kujipanga kwetu na utayari wetu wa kulitumikia taifa hili Ambalo wazazi wetu wameishi kwa miaka mingi.
Ni lazima tujue mwelekeo wetu, Ni lazima tujue nini tunahitaji kama taifa na dhamira yetu ya kuwa wamoja ina malengo gani. Mimi naamini kwa dhati kabisa kuwepo kwetu pamoja kama taifa sio kuondoa umaskini bali kuleta heshima yetu na kuweka rekodi katika dunia katika ufanisi wetu, jitihada zetu, maarifa yetu na uwezo wetu wa kuleta mabadiliko katika ulimwengu. Naamini kama tukiwa wamoja na wenye kupendana, wenye jitihada katika malengo yetu mafanikio kwetu yatakuja kama mafuriko. Tunauwezo wa kuleta mabadiliko katika uvumbuzi na katika nyanja yeyote hakuna kikwazo zaidi yetu sisi wenyewe.
Hatujaamua kuondoa Umaskini, hatujawa serious katika kuleta mabadiliko, tukiwa serious kutaka mabadiliko tunayoyahitaji tutafanikiwa. Hili taifa litabadilika miaka sio mingi kama tukitia jitihada zetu na maarifa yetu katika kila nyanja kwa uaminifu na ukweli wa roho kuleta mabadiliko kwaajili yetu na vizazi vyetu.
Sioni kwanini sisi ni maskini, sioni kwanini sisi ni ombaomba zaidi ya kutokuwa tayari kwetu, kuleta heshima yetu na mabadiliko katika taifa letu wenyewe. Nimesema mara nyingi ni watu wanaoleta mabadiliko katika nchi kwa jitihada zao na busara zao kuona maisha yao yanaboreka. Watu wanauwezo wa kubadili jangwa na kuwa paradiso lakini ni watu hao hao wanaweza kuwa na kila maliasili bado wakawa mafukara kwasababu ya ujinga na uvivu.
Katika historia ya dunia, Taifa ambalo wametumia muda mwingi kutafuta maarifa na kuvumbua mara zote limekuwa taifa linalotawala mataifa mengiine, ni muhimu kwetu kujishughulisha sana katika kutafuta maarifa kwa juhudi zetu zote kwa faida ya Taifa letu na kizazi chetu ili tujenge taifa imara.