Mabadiliko ya Lowassa na Magufuli yapi ni sahihi?

Mabadiliko ya Lowassa na Magufuli yapi ni sahihi?

Mwangaza

Senior Member
Joined
Feb 26, 2008
Posts
198
Reaction score
64
Wanabodi,

Wagombea wawili wa urais wamekuwa wakiahidi mabadiliko. Tunagalie kwa kina dhana halisi ya mabadiliko kwa hawa watu.

Lowassa ameahidi mabadiliko kwa kufanya yafuatayo:-

1.Kurudisha katiba ya warioba
2.Kutoa elimu bure mpaka chuo kikuu
3.Bima ya afya
4.Hospitali kila wilaya
5.Posho kwa wenyeviti vijiji/mitaa

Magufuli anahidi mabadiliko kwa kufanya yafuatayo:-

1. Kufungua mahakama ya mafisadi
2. Kutoa Elimu bure mpaka kidato cha nne
3. Kununua meli mpya 3
4. Kutoa millioni 50 kila kijiji
5. Kujenga mabarabara

Ukiangalia dhana hasa ya mabadiliko hakuna hata moja linaweza kufanikiwa kwa ufanisi hapo bila KUBADILISHA KATIBA KWANZA.

Katiba ikibadilishwa ikarudishwa katiba ya wananchi, ile ya tume ya Jaji Warioba, tutapata haya:-

1. Gharama za uendeshaji wa serikali zitapungua kwa zaidi ya 50%, kwa sababu mawaiziri, naibu na makatibu wao watapungua, wabunge watapungu, wajumbe wa baraza la wawakirishi watapungua, n.k.

2. Tutarudisha madaraka kwa wananchi-hivyo wataweza kuwawajibisha wabunge wazembe na mafisadi,watendaji wazembe na mafisadi,na hata mawaziri wazembe na mafisadi.

3. Tuongeza uhuru wa mahakama-maana jaji mkuu hatateuliwa na rais.
---Kufungua mahakama ya mafisadi wakati mahakama hazina uhuru,ni sawa na kuwa na TAKUKURU yenye kibogoyo kama hii.

4. Mawaziri, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa..watakuwa watumishi wa wananchi sababu hawatakuwa wateule wa Rais.

5. Mgombea binafsi ataruhusiwa bila masharti magumu kama yalivyo kwenye katiba ya Chenge. Hii itaongeza demokrasia na kuhoji utendaji wa serikali.

6. N.k. n.k.

Tumeona nchi nyingi zimepata mabadiliko ya kimaendeleo baada ya kwanza kubadili katiba mbovu iliyopo, kwa mfano Kenya, Marekani, n.k.

HATUWEZI KULETA MABADILIKO BILA KWANZA KUBADILI KATIBA HII MBOVU.

Magufuli amedandia treni kwa mbele, mabadiliko anayosema HAYAWEZEKANI

NAUNGANA NA Mh LOWASSA AMBAYE ATALETA KATIBA YA WANANCHI... NDIPO TUTATAPATA MABADILIKO YA KWELI.
 
katiba kwanza, hizo mahakama ataundaje kama hazimo kwenye katiba??. CCM BANA JANJA SANA LAKINI TUMESHAGUNDUA JANJA YAKE,
 
kama ccm haitangazi msimamo wake wa kuibatilisha katiba hawana sera wala mabadiliko,,hizo sera anazoahidi wangombea wote walipita na kuwa maraisi wameahidi zaidi ya hayo nini kimefanywa?.ni ngonjera tu za majukwaani
 
Back
Top Bottom