kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 18,098
- 17,448
Uhalibifu wa mazingira unaoambatana na ongezeko la ukataji wa miti, uchomaji wa makaa ya mawe, mkaa na mafuta jamii ya petrol kwenye magari, majenereta na mitambo ya kufua umeme (power stations), milipuko ya nuclear, kilimo cha kwenye mabonde makubwa na matumizi makubwa ya vipoza hewa (viyoyozi, mafriji, cold rooms) kunasababisha uzalishaji wa gesi (carbons, methane, cloroflorocarbons) zinazosababisha mabadiliko ya hali ya hewa duniani na Tanzania ikiwemo.
Baadhi ya madaliko mabaya sana kwetu ni kuongezeka kwa joto duniani (global warming) na tanzania ikiwemo na kupungua kwa tabaka la mawingu mazito (ozone layer), hivyo kusababisha kuongezeka kwa ujazo wa maji baharini kunakotishia kumezwa kwa fukwe na visiwa. Joto kubwa pia husababisha vimbunga, mafuriko, ukame mkubwa, mvua zisizotabirika lini, wapi na kiasi gani zitanyesha, kuungua misitu na nyika (wild fires) na magonjwa ya kigenetics, kushuka kinga ya mwili, uchovu mkubwa na kiyangayanga.
Hali hii inasababisha watu wanaoishi karibu na fukwe za bahari, maziwa na mito kote duniani kuwa hatarini kukumbwa na vimbunga na mafuriko makubwa mara kwa mara na watu wanaoishi karibu na misitu mikubwa kukumbwa na hatari ya moto wa misituni na nyika (wild fires).
Eee ndugu mwananchi sasa hivi sio ufahari tena kuishi karibu na vyanzo vya maji kama vile kando kando ya bahari, mito na maziwa. Maeneo hayo kwa sasa ni maeneo hatarishi, tusiyakimbilie kwa gharama kubwa.
Hata kama una kiwanja/nyumba huko Bunju, Ununio, kunduchi, Mbezi, Masaki, Mikocheni, Kigamboni, nk usisahau pia kutafuta kiwanja/nyumba mitaa ya kibaha, Kisarawe, Kimara, Buguruni, nk ambako mafuriko yatachelewa kufika. Hata nchi zilizoendelea sasa hivi watu wanakwepa makazi ya karibu na vyanzo vya maji. Yanayotokea Msumbiji, Zimbabwe na Malawi hivi sasa yametokea pia Asia, Marekani (Florida, Miami, nk) na Ukaya kando kando ya vyanzo vya maji ya bahari, mito na maziwa. Mwezio akinyolewa wewe ficha kiwembe na kimbia sana mbali.
Nunua viwanja kwenye maeneo hayo kwa bei ndogo saaana siku hizi kama ikibidi. Siku hiyo ikifika tajiri wa ununio atakuwa masikini na masikini wa Buguruni atakuwa tajiri.